mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 12,268
- 9,159
Nimeguswa sana na msiba wa Fidel Castro Odinga,hakika nimepata majonzi makubwa ,Fidel Odinga alikuwa ni mtu wa watu na mtoto wa mujini kweli kweli,pamoja na hadhi ya babu yake , baba yake , ukoo na utajiri wake wa kutisha daima hakulewa sifa na wakati wote alikuwa karibu na watu wa matabaka tofauti,rika mbalimbali,kabila tofauti,na aliweza kutumia fedha zake kuwasaidia watu wa aina mbalimbali bila kuangalia kabila,cheo,au mpinzani wa babake n.k.
Na wote tumeona pia kuwa pamoja na kuwa baba yake alikuwa na tofauti za kisiasa na na rais na Uhuru Kenyatta huyu kijana alikuwa ni rafiki mkubwa wa Uhuru na hata Ruto.Ni kijana mdogo ambaye aliweka nyuma dhambi kubwa ya Kenya ambayo ni ukabila.
Pia Fidel alikuwa ni rafiki wa watu masikini alitumia fedha yake kuwasomesha watoto wenye shida wengi tu,aliweza kuwa karibu na masikini wa Manzese (Kibera,Mathare).
Fidel aliwekeza kwenye ukarimu na sio kwenye fedha,na hakika kwa kuonyesha jinsi alivyokuwa anapendwa na ndicho Wakenya wamekifanya kwenye kumuaga Fidel.
Naweza kukiri kwamba sijawahi kuona msiba uliovuta hisia za watu na kuagwa na watu wengi kama Fidel na si Wajaluo tu bali watu wa makabila mbalimbali.
Na kifo cha Fidel kiwe ni funzo kubwa kwa watoto wa viongozi na matajiri ambao hujali zaidi pesa zao na maisha yao kuliko kuwasaidia wasio na uwezo.
Tumeona watoto wengi wa wanasiasa wa hapa Tanzania jinsi wanavyokuwa jeuri kwa kutegemea vyeo vya wazazi wao na utajiri walio nao kuwasema watu ambao ama wanapingana na wazazi wao kisiasa au mitizamo ya kisiasa.
Je, ni wangapi ambao huwatembeleawenye shida huku Manzese,Mburahati,Keko,Tandika na kwenye makazi duni mengine?
Je, ni nani ambaye angalau anatoa sehemu ya utajiri wake kuwasomesha watoto masikini?
Ndugu zangu Fidel aliwekeza kwa watu na ndio maana ameagwa kwa maelfu huko Kenya,Fidel hajaagwa hivyo kutokana na baba yake bali kutokana na yeye mwenyewe kuwapenda watu kwa moyo mmoja,alikuwa habagui alikuwa hashindi tu O'bay,Masaki,Upanga.Naamini kifo cha Fidel ni mwanzo wakuwaleta Wakenya pamoja.
Mwisho tujifunze kuwa siasa sio ugomvi wakati sisi akina yakhe tukitukanana humu kuhusu nani anafaa urais hao ambao tunawashabikia ni watu ambao ni marafiki kifamilia,wamesoma pamoja na hata watoto wao wamesoma,wamecheza pamoja na hata dili wanafanya pamoja.
Tumeshuhudia rais Uhuru akisema Fidel alikuwa ni rafiki yake wa karibu na si uongo,hata mtoto wa dadake Uhuru alikuwa wakati fulani mchepuko wa Fidel,hawa wanakunywa whisky pamojanna hata picha zinasema tumemuona rais Uhuru,Ruto na wanasiasa wengine walivyoungana katika huu msiba.
Wakati huu ni wakati wa kusherehekea maisha ya Fidel kama alivyosema baba yake,Fidel amefanya yake makubwa katika umri wake mdogo,basi yatupasa na sisi wengine kuiga yale mazuri aliyoyafanya Fidel.
Fidel aliwekeza kwa watu na watu nao wanamuaga kwa heshima kipenzi chao Fidel,wema unalipa jamani na kielelezo cha wema wa Fidel ni jinsi anavyoagwa .
RIP Fidel.
Cc Ab-Tichaz ,pole .