Kwanini wewe shida yako hasa nini embu kuwa analitiko na sio mpiga majungu. Hoja yako DHAIFU sana, haina changamoto wala Vision. Weka mfano. So far JPM anafaa kwa mazingira yetu ya penda dezo. Embu tuambie chama gani sasa utakipa madaraka na sera zake katika mazingira yetu ya Tz. Tatizo tungeanza kudeal na Mentalität mbovu kama zako na watz wengi kuhisi chama au mtu ndo ataibadili Tz. Play your part, fanya kazi, lea watoto wako katika msingi wa utu na kujua umuhimu wa kufanya kazi hata kma kulima nyanya. Hakuna duniani nchi iliyofika juu kwa KUWA NA viongozi wa kucheka cheka na wananchi wapenda maneno mengi na mipasho. Soma historia njoo hapa tuambie. SIASA ZETU BADO NI ZA NITAPATA LINI NAFASI NILE. AND WALA ITS NOT ABOUT CCM ITS ABOUT ME AND YOU. HATA CCM NDANI WANAJIBADILISHA NA NYIE MNABAKI NA JINA BADALA YA KUANGALIA MATOKEO NA MAELEKEO. PAMBANISHA SERA ACHA MASIMULIZI YA VIBANDA VYA KAHAWA. TUONYESHE VISION YAKO.
Kasome historia ya Singapore na Malaysia ndiyo utajua kwa nini kwa hizi siasa za CCM, hatuwezi kufika popote.
Failure of the organization is failure of the management.
Tanzania tumeshindwa kupiga hatua kuelekea kwenye maendeleo ya kweli kutokana na kuukosa uongozi unaofaa. CCM wanajua, Rais anajua, na kila mwenye akili anajua.
Kama tungekuwa na viongozi wenye upeo, dhamira, utashi, hekima na uzalendo, wangeruhusu mifumo ya demokrasia na utawala bora vifanye kazi ili siku moja tuwapate viongozi wenye uwezo wa kuwaongoza Watanzania katika njia iliyo sahihi ya kuyafikia maendeleo yanayohitajika.
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa kuwa nq utawala wa kimabavu au kidikteta. Watu wanaitaja China, nchi ambayo kwa miaka mingi watu wameishi kwenye umaskini mkubwa, walisaidiwa tu na uwingi wa watu na ukubwa wa nchi kuweza kutekeleza miradi mikubwa lakini maisha ya mwananchi mmoja mmoja yakiwa duni kabisa.
Kuanzia miaka ya 2000 mpaka sasa, China imepiga hatua kubwa, nayo ni baada ya kubadilisha sera zake nyingi, na hivyo kuvutia uwekezaji mkubwa wa mataifa ya nje. Bila huo uwekezaji, China bado ni duni. Na China haiwezi kukubali kuondoa uwekezaji wa nje, ndiyo maana hata Rais wao mara nyingi yupo Ulaya na America kutafuta uwekezaji.
China, kila mwaka inapata uwekezaji wa nje unaofikia dola bilioni 70. Leo, sisi kwa kukosa uongozi wenye uelewa na maono tunaamini kuwa China ndiyo itakayofanya uwekezaji mkubwa nchini mwetu.
Katika Dunia nzima, mitaji mikubwa ya uwekezaji ipo America, Europe na Australia. Ni uwekezaji mkubwa kutoka mabara hayo, ndio ulioibadilisha South Korea, Brazil na China. Huo ndiyo ukweli, upende au uchukie.