Tunaisubiri "salary slip" ya Rais kama tulivyoahidiwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,860
Wiki hii inayoanza kesho tunataraji haitapita bila Raisi kutekeleza ahadi yake ya kuitoa salary slip yake hadharani kuthibitisha kiwango cha fedha anacholipwa kama mshahara (shilingi 9.5 kwa mwezi) baada ya yeye kurejea Dar/Ofisini.

Nakumbusha tu.

Ahadi ni deni.

"Ujamaa" una gharama zake hasa kwa dunia ya leo-kuuishi ni kazi,kuuishi ni changamoto.
 
Ukipewa salary slip unaomba bank statement , ukipewa bank statement utaomba tena transition alimuradi kupinga tu.

Teh teh teh!
 
Wiki hii inayoanza kesho tunataraji haitapita bila Raisi kutekeleza ahadi yake ya kuitoa salary slip yake hadharani kuthibitisha kiwango cha fedha anacholipwa kama mshahara (shilingi 9.5 kwa mwezi) baada ya yeye kurejea Dar/Ofisini.

Nakumbusha tu.

Ahadi ni deni.

"Ujamaa" una gharama zake hasa kwa dunia ya leo-kuuishi ni kazi,kuuishi ni changamoto.
Naona karibu utawehuka. Eti tunangoja salary slip; wewe na nani, kwani huna kazi nyingine ya kufanya?
 
Jamaa kesha rudi toka mapumzikoni Chato na Rwanda na kesho yupo ofisini ni vyema akatimiza ahadi yake asisisubiri mpaka kelele ziwe nyiiingi ili aitoe.
 
~~>Kujua Mshahara wa Raisi si kipaumbele chetu kwasasa..

~~>Tunahitaji maboresho ktk huduma za Kijamii, Upatikanaji wa Ajira, Kupunguza Rushwa n.k
 
Labda slip itengenezwe kwa ajiri ya maonyesho tu , marais kawaida hawalipwi kila mwezi Bali ulipwa mshahara Wa
miaka 5 kwa mkupuo
pindi anapomaliza mhura
wake, ukizingatia rais uudumiwa kila kitu sasa apewe mshahara kila mwezi Wa kazi gani.
 
Acha kujipendekeza!
 
Hilo nalo neno,litaondoa utata tena itoke ikulu sio clouds TV au radio.
 
Wiki hii inayoanza kesho tunataraji haitapita bila Raisi kutekeleza ahadi yake ya kuitoa salary slip yake hadharani kuthibitisha kiwango cha fedha anacholipwa kama mshahara (shilingi 9.5 kwa mwezi) baada ya yeye kurejea Dar/Ofisini.

Nakumbusha tu.

Ahadi ni deni.

"Ujamaa" una gharama zake hasa kwa dunia ya leo-kuuishi ni kazi,kuuishi ni changamoto.
Salary Slip nadhani sasa nasi tuachane na siasa hizi za maigizo ambazo ccm wanataka kutupeleka.
Sasa hivi tuunganishe nguvu (kama wafanyavyo Kenya na SouthAfrica) kwenye hizi kashfa zinazodidimiza nchi.
Kuna kutaka ukweli na hatua kuchukuliwa kashfa za NSSF, wizi wa Jeshi la polisi ambako hata waziri katajwa na prince mstaafu. Kashfa za UDA na wahusika wake na huu ujangili usioisha ambao tunaambiwa wapo wahusika ndani ya Bunge.
Hizo nchi nilizotaja kama kuna kashfa kwa kiongozi watu wote wanapiga kelele hadi anaondoka, tuliona Jaji mkuu Kenya na sasa tunaona ya Zuma huko SA.
Hizi sarakasi za mshahara, posho, sijui maslahi ambavyo vyote vipo kisheria tukivipa kipaumbele huku nyuma hawa wakora wanatumia nafasi kufisadi na kuiba kama hawana dini. Ukichunguza mijadala hiyo ccm wanaipenda sana ili kuwatoa watu kwenye track
 
  • Thanks
Reactions: 911
Masharti ya kazi ya Rais Sheria ya 1984 Na.15 ib.9 43.-

(1)
Rais atalipwa mshahara na malipo meingineyo, na atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au posho, kadri itakavyoamuliwa na Bunge, na mshahara, malipo hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho, vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii...

source:http://www.tanzania.go.tz/egov_uplo... JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA.pdf
============================================================
Nilikuwa napitia katiba nikutana na hili.
 
Back
Top Bottom