Yofav
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 4,156
- 7,416
Hizo ni baadhi ya picha za kabla ya mvua.
Baada ya mvua kidogo tuu matokeo ni haya hapa⬇️
Kinachouma na kusikitisha kabisa ni kwamba hili Daraja lipo karibu kabisa na office ya serikali za mitaa lakini viongozi wa hapo hawaoneshi kabisa kuoina issue hiyo kama changamoto licha ya kuwa imekuwa kero kwa wananchi wa eneo hilo kwa kuwabidi kuzungukia katika njia ya jirani ambayo ni maalumu kwaajili ya Tain/Rail way na hii ndiyo njia pekee ambapo wananchi wote waishio Tabata Kisiwani huitumia kuingia na kutokea mtaani.
Kwa akili zangu za haraka inaonekana sehwmu hii ingeshafanyiwa marekebisho ila ni dhahiri kwamba kuna viongozi wanaokwamisha hilo.
Ni aibu sana kuona sehemu ambayo ipo ndani ya wilaya ya Ilala kuwa ya hovyo namna hii huku ikihesabiwa kuwa ndani ya Jiji.
Naomba kero hii iwafikie viongozi husika wa eneo hili maana hata huyo mbunge toka achaguliwe inaonekana hamna kitu anachokifanya maana kama kweli anaelewa nini anafanya basi hili Daraja ambalo ndo kama mlango wa kuingia na kutokea kwa wananchi wake angeliacha katika hali hii hadi awamu inapinduka.
Shame.