Uchaguzi 2020 Tunaingia kwenye Uchaguzi Mkuu tukiwa tunakumbuka tambo hizi

Kwenye mishahara na maslahi ya watumishi imekuwa changamoto. Wamepitia mengi sana ktk kipindi hiki ambayo ni vigumu sana kuyasahau, tangu kutumbuliwa, madaraja na wastaafu.

Cha ajabu pamoja na zote shida still polisi wataichagua ccm ili iendelee kuwanyima haki zao
 
"Nimekuteua, nakulipa mshahara, nimekupa gari ole wako jimboni kwako utamtangaze mpinzani (JPM)". Hili ndili kiboko yao kwa maana hawa walioteuliwa ndiyo wasimamizi wakuu wa uchaguzi. Uchaguzi mkuu ujao hautakuwa uchaguzi bali ni uchafuzi. Mimi sitapiga kura!
We baki nyumbani tulindie nyumba,sie tukamfurushe mkoloni arudi kwao kwa kura kwanza then mengine yatafata
 
Mk
Kamatakamata/kuteka na kuwajeruhi hata kuwaua wapinzani wake wa kisiasa, wanaharakati na waandishi wa habari. Kuwapa kesi za UHUJUMU UCHUMI. Magufuli hafai

#LISSURAIS2020
Mkuu una uhakika na hashtag yako au unaandika tu ili nawewe uonekane umechangia uzi!?😁😁
 
Sasa mkuu jamaa kachangia point we tena unamtukana hivi unafikiri kumtukana mchangiaji ndo utaiondoa NEC iliyopo!?, Umetukana kwavile jamaa kaongea ukweli!?, Acheni matusi chadema mnajiharibia ninyi wenyewe☹️
ushindi wake hautakuwa realistic kwa kuwa NEC ni mali yake, ivyo kauli yako ni sawa na kujisifia kuwa umeua wengi baada ya kupiga bomu mochuari, bweha mla kuku wewe
 
Wakati tunasubiri kipenga kuanza uchaguzi mkuu, tuliojsliwa kusoma alama za nyakati tunakumbuka Tambo hizi:

1. Sikuchaguliwa ili niongeze mishahara (Rais JPM)
2. Sikuleta tetemeko la ardhi na kwa Nini kila janga Ni lenu (JPM)
3. Nataka Bei ya sukari iteremke Hadi sh. 1800 (JPM )
4. Nataka Tanzania iwe Kama Dubai (JPM)
5. Nitawapiga mashangazi zenu viboko mkiniletea upuuzi (JPM)
6. Jeshi litabangua korosho hata kwa meno (JPM)
7. Nitashughulika na wahujumu uchumi hata awe mke wangu (JPM)
8. Nimekuteua, nakulipa mshahara, nimekupa gari ole wako jimboni kwako utamtangaze moinzani (JPM)
9. Nijenge shule halafu upate mimba, siwezi kusomesha wamama (JPM)
10. Mpinzani hawezi kukanyaga serikali yangu (JPM)
11. Million 50 kila Kijiji (JPM)
12. Hakuna mahala popote nilipozungumzia katiba wakati wa kampeni (JPM)
Tuchambue Ni wapi rahisi alifanya vibaya na wapi alifanya vizuri. Kwa Yale maxuri
1. Ununuzi wa ndege kwa cash
2. Ujenzi SGR bado unaendelea
3. Ujenzi uwanja ndege chato na upanuzi viwanja vingine vya ndege
4. Kukuza na kujaza wanyama hifadhi ya Burigi
5. Kuthibiti mapato ya nchi
6. Deni la taifa kuongezeka
7. Kupaisha taifa kuingia uchumi wa mwisho wa Kati
8. Kudhibiti na kuwaondoa wananchi kuhusu ugonjwa wa Corona
9. Kutokupandisha mishahara ya watumishi lakini kuweka nidhamu kazini
10. Kutoa fedha on the sport kusaidia wenye uhitaji na kugharimia miradi iliyokwama
11. Slogan ya viwanda cherehani 4 tayari kiwanda. Hapa kazi tu
12. Kuwavutia wapinzania kuhamia CCM kuunga juhudi
13. Kutokusafiri nje ya nchi kuokoa fedha
14. Kuongoza kwa kutumbua na kufanya teuzi
15. Kuzunguka nchi nzima kuzindua na kufungua miradi mikubwa
16. Ujenzi wa mahakama kuu kila mkoa
17. Msimamo mkali juu ya siasa za nje
18. Kupita bila kupingwa kwenye chama chake kuwania kiti Cha urais.

Nadhani Tuanze Sasa mjadala
Sawa
 
Back
Top Bottom