Tunaikaribisha uber jiji la Mwanza

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,618
2,000
Uber ni Kampuni ya magari ya taxi ndogo, kati inayosafirisha watu kwenye maeneo mbali mbali katika Jiji la Dar es Salaam. Kila ninapofika Dar es Salaam usafiri wangu kwa asilimia kubwa natumia Uber. Gharama za uber kwa wanaoielewa ni gharama nafuu sana. Niwape tu mfano, kwa usafiri wa uber toka Buzuruga mpaka kKituo cha reli ya kati ni kama Tshs.3,000 LAKINI ukitumia usafiri wa taxify ni kama Tshs.6,000. Mfano mwingine ukitoka sinza mpaka Railway station ni kama Tshs.7,000 wakati taxi za kawaida ni kama Tshs.20,000. Binafsi nimeona kuwa usafiri wa uber kama wangekuwa hapa Mwanza ni nafuu sana kuliko Taxify. Kule Dar es salaam kwa sasa taxify hawapati wateja kwa sababu ya gharama zao na hata magari ya taxi za kawaida muda siyo mrefu yatatoka barabarani. Kama mdau nawakaribisha sana Mwanza ili kuwe na ushindani na wateja wapate unafuu katika usafiri. Karibuni sana kwenye Jiji la Mwanza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom