Tunahitaji viongozi wenye maono

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Swali jingine muhimu ambalo linaweza kuwa mwongozo ni kujua kwanini tunaelimisha watu wetu, Kama lile swali la mwanzo nililouliza kwanini sisi ni taifa? Ni swali la kimsingi katika kutengeneza agenda ya nchi. Kwanini sisi ni taifa? tuko pamoja kwa malengo gani? We must define ourselves to know our destiny.

Tusipolijua hili tutakuwa tunajiendea tu na taifa letu litakuwa halina mwelekeo maalum. Ufunguo wa taifa lolote lile ni elimu inayotoa kwa watu wake, na elimu hiyo lazima itolewe kulingana na agenda , dira na mwelekeo ambao taifa linataka kuchukua. Kwahiyo dira ya taifa ndio inayoamua aina ya elimu inayopaswa kutolewa. Sio kutoa toa elimu kiholela ni westage of resources. So we must choose our path hatuwezi kuendelea tukiwa na many paths. A scattered mind can not achieve anything.

Tunapaswa kujua aina gani ya taifa tunalotaka kulijenga na kutengeneza elimu yetu kulingana na mwelekeo huo. Elimu isiyo kuwa na dira haiwezi kunyanyua Taifa lolote. Elimu lazima iendane na maono ya kitaifa. Elimu ya kutafuta mkate haijawahi kusaidia taifa lolote. Na haiwezi kuproduce any quality intelligence.

Elimu ya kutafuta mkate ni elimu ambayo imejengwa kibanafsi mtu anaenda kusoma ili apate ajira na kupata mkate wa kila siku na haina malengo yoyote ya kitaifa bali faida za kibinafsi tu. Utaifa sio priority. Au haumo akilini mwa mtu.

Haina malengo ya kutatua changamoto ambazo jamii inazo, haijaelekezwa huko, imeelekezwa kwenye mkate. Hatuwezi kuvuka kwa aina hii ya elimu na fikra.

Tunahitaji akili zinazofikiri kuhusu kutatua changamoto zinazotukabili ili taifa hili lisonge mbele. Na lengo la msingi la elimu yetu iwe kutengeneza akili na watu wenye uwezo wa kutatua changamoto zinazotukabili na sio kutoa elimu mkate. We need aina hii ya watu creative ambao hawako driven by personal gain bali mabadiliko.

Ukweli ni kwamba hakuna taifa litakalo tuogopa kama hatuna uwezo wa ku create vitu. Tukifikia uwezo wa kuzalisha vitu wenyewe na kujitegemea macho ya wazungu yatakuwa juu yetu. Ni technologia pekee inayofanya taifa kuwa imara, uwezo wa kutawala mazingira yanayokuzunguka. Kwetu sisi bado ni mdogo kwasababu ya uwezo wetu mdogo wa inventions. Na hii nguvu lazima tuwe nayo na sio kununua tu vitu tuwe na uwezo wa ku create.

We are poor sababu ya uwezo wetu mdogo wa inventions. Na kwasababu hiyo tumekuwa ni soko la produce za mataifa mengine. Na hii haifurahishi sana. Na hakuna siku ambayo malighafi zetu zitatufanya kuwa matajiri pasipo kuwa na uwezo wa kuzibadili kuwa mali. Kwasababu kitu kilichofanya raw material kuwa na thamani ni invention. Ni logic tu walio invent magari na machine watapata faida zaidi ya wenye petroli. Kwasababu bila invention zao petrol isingekuwa na thamani. Kinachofanya petrol kuwa na thamani ni inventions. Kwahiyo tusiangalie sana kuhusu maliasili kuliko akili za watu wetu.

Akili ni muhimu zaidi hata kwenye management ya maliasili zenyewe. Kama watu wako ni wapumbavu hata hizo maliasili hawatoweza kuzimanage achilia mbali ku invent vitu. Watu watajilia maliasili za bwerere. Kwasababu ya udogo wa fikra za watu. Kama akili za kufanya invention hatuna je hata hzi za ku manage resources zetu tunawezaje kuzikosa? Ambazo hizi zinaweza kutupa mkate tu na ahueni ya maisha? Lakini sio POWER kwasababu power belong to those who invent things.

Taifa sio lengo lake kumuelimisha mtu kwa faida zake binafsi bali kwaajili ya lengo ambalo taifa linataka kufikia, kwaajili ya vision ambayo taifa linayo. Na kutokana na hiyo vision taifa linapaswa kusomesha watu wake kulingana na hiyo vision ili kuifikia na si kwaajili ya malengo binafsi. Nasema tena na watu wa serikali wanisikie tutakuwa maskini milele tukiwa na aina ya fikra tulizonazo na tutaridhisha umaskini huo kizazi hadi kizazi hadi tubadili fikra zetu. Lazima kuwe na harmonization katika ya malengo ya kibinafsi na yale ya kitaifa. Lazima kuwepo na proper balance. Watu wasiwe wabinafsi zaidi au wasijinyime zaidi.

Lakini kutumikia taifa lako iwe ni wajibu wa kimsingi wa kila raia na elimu yetu lazima ijenge aina hiyo ya uzalendo. kama taifa hili likiwa halipo mioyoni mwa watu wake na watu wake wakiwa wanaongozwa na malengo binafsi tu na ubinafsi wao tutawezaje kuendelea?

Kwa aina ya elimu tuliyonayo hatuwezi kutengeneza watu wenye creative mind ambao kwa kutumia akili zao wanauwezo wa kutatua changamoto zinazokabili taifa.

Hatuwezi kuendelea kwa aina hiyo ya fikra. Kwahiyo tunahitaji watu ambao kila wakati wanafikiri kuhusu taifa na jinsi gani ya kutatua changamoto zinazotukabili with the devoted heart. Na tusijidanganye elimu ni ya msingi sana katika maendeleo ya nchi yeyote ile na elimu inapoharibika msingi na mwelekeo wa taifa uharibika. Kwahiyo focus kwenye elimu inapaswa kuwa kubwa kuliko eneo jingine lolote lile. Lazima izalishe watu ambao wana ufahamu wa kutosha, maadili na nidhamu ya kutosha, wanaojua wajibu wao kwa taifa na jamii inayowazunguka, Wenye maarifa ya kazi ya kutosha ili waweze kukuza uchumi wa taifa lao, kiujumla kujenga raia bora wenye faida kwa taifa ambao tabia zao zimechujwa na kuwafanya wenye uwezo kufanya maamuzi sahihi kwa taifa lao. Hatuwezi kuendelea kama tuna watu ambao hawana uwezo wa ku manage akili zao vizuri na kuziongoza kwenye mwelekeo wenye faida.

Katika maisha haya tunachagua mwelekeo wetu iwe taifa ama mtu mmoja mmoja. Kwa taifa viongozi ndio wanaochagua dira yetu. kwahiyo inategemea akili zao na busara zao. Na maendeleo yetu kama taifa inategemea wana maono ya namna gani kwahiyo kuendelea au kutokuendelea kunategemea aina ya viongozi na akili zao.

So mwelekeo wetu kama taifa unategemea viongozi tulionao wao ndio manahodha wetu wanaoongoza meli yetu. Wanauwezo wa kutufikisha pazuri au pabaya. Wao ndio incharge sisi raia hata tuwe na mawazo mazuri kiasi gani hatuwezi fanya chochote. but truly our destiny depend on our leaders. Wao ndio wanaotunga sera na ku enforce laws. Sera nzuri au mbaya, sheria nzuri au mbaya inategemea na quality ya intelligence za viongozi. So tunahitaji viongozi ambao wanauwezo wa kufanya good decisions kwa sababu mwelekeo wetu unategemea hilo. So our destiny depend on the vision of our leaders.

Kama tukiwa na viongozi wasio na vision na wapiga porojo na ambao wako kwenye uongozi sababu ya mkate na ambao maadili yao hayo refined tujue hatutafika popote. Kitu tunachohitaji ni uongozi wenye dira na dira hiyo lazima ishuke chini kwa wananchi kupitia kwenye elimu yetu na kushape watu wetu kulingana na malengo ya kitaifa. Na kujenga umoja katika malengo ni jambo ambalo halipingiki kama tunataka taifa hili liendelee. Truly tunahitaji kiongozi ambaye ata treat ubinafsi in a every harsh way na kulirudisha taifa katika utaifa.
 
Kiongozi wa NKorea, nafikiri babu wa huyu kiduku. Aliulizwa na waandishi wa habari kuwa nchi yake imewezaje kujitegemea licha ya magumu na vikwazo?

Akajibu kuwa elimu yao ndiyo imewawezesha hivyo. Akasema kuwa kwenye elimu yao ya chuo kikuu. Humanity sciences ni 30% ya wanafunzi wote. Na asilimia 70 ni natural sciences.

Siku moja tuliingia matatizoni na UN baada ya kusemekana tumetoa mafundi Nkorea kuja kututengenezea ndege za jeshi.

Hapa kwetu na nchi nyingi za Africa ni tofauti kabisa. Hizi humanities ni muhimu sana, ten sana lakini si kwa wingi uliopo kwenye nchi zetu. Hizo zinaandaa sera na mipango, lakini utekelezaji unahitaji natural sciences.

Hivyo basi, ni kweli tunahitaji elimu inayoendana na maono ya nchi na inayotatua matatizo yetu, mambo ya kufanya ili kufikia hapo ni mengi. Msingi uanzie chini ila Kila mkoa unastahili kuwa na technical university na medical university. Unaweza una ni vingi ila kitakwimu nchi yetu ni moja ya nchi inayozalisha wataalamu wachache duniani.
 
Kiongozi wa NKorea, nafikiri babu wa huyu kiduku. Aliulizwa na waandishi wa habari kuwa nchi yake imewezaje kujitegemea licha ya magumu na vikwazo?
Akajibu kuwa elimu yao ndiyo imewawezesha hivyo. Akasema kuwa kwenye elimu yao ya chuo kikuu. Humanity sciences ni 30% ya wanafunzi wote. Na asilimia 70 ni natural sciences.
Siku moja tuliingia matatizoni na UN baada ya kusemekana tumetoa mafundi Nkorea kuja kututengenezea ndege za jeshi.

Hapa kwetu na nchi nyingi za Africa ni tofauti kabisa. Hizi humanities ni muhimu sana, ten sana lakini si kwa wingi uliopo kwenye nchi zetu. Hizo zinaandaa sera na mipango, lakini utekelezaji unahitaji natural sciences.

Hivyo basi, ni kweli tunahitaji elimu inayoendana na maono ya nchi na inayotatua matatizo yetu, mambo ya kufanya ili kufikia hapo ni mengi. Msingi uanzie chini ila Kila mkoa unastahili kuwa na technical university na medical university. Unaweza una ni vingi ila kitakwimu nchi yetu ni moja ya nchi inayozalisha wataalamu wachache duniani.
Maarifa yanapaswa kutafutwa popote na kutumiwa kwa manufaa ya nchi.
 
Back
Top Bottom