Mkuu hakuna mpepelezi anayeongoza kama akina Jack Baur na kina Wily Gamba, Joram Kiango n.k.Kaka nimeona. Nadhani uko sawa. ukiangalia harakaharaka utagundua kigezo kikubwa ni hali ya usalama. kwa mfano ukiangalia Israel, Pakistan na India ambao ndio wanaongoza hali zao za usalama ni tete sana. Australia ambao wanashika namba 10 unaona kuwa wamejikita kwenye masilahi yao ya kiuchumi zaidi (na hasa ni sector ya madini). CIA wao wako kila mahala lakini usiri wao wa habari sio mzuri ingawa wanawezeshwa kuliko agency yoyote duniani. Swali la ziada, Hivi hii dhana ya kuwa na mpelelezi anayeongoza (kama inavyopenda kuwekwa kwenye sinema na vitabu vya hadithi) huwa ni ya kweli? kwa mfano james bond, willy Gamba, Joram kiango n.k je? ni kweli huwa kuna mpelelezi anayeongoza kati ya wenzake na kujichukulia umaarufu?
Naomba nitoe angalizo.
Naona watu wanatolea mifano kwa kuitaja sana CIA. Kwa taharifa yenu Intelligence agency ambayo ni high efficiency na kiwango zaidi Duniani ni ile ya Pakistan, ISI.
Kama serikali haina mpango wa kuimarisha usalama wa nchi, na sisi tunaona kabisa usalama wetu uko mashakani suluhisho ni nini? tulalamikie nini ili wafanye nini? je? ni rahisi kiasi gani kutenganisha siasa na usama wa nchi?
Mkuu Mpingauonevu, maswali yako yameibu maswali mengi kichwan mwangu hasa juu ya uwezekano wa kuwa na utawala wa sheria/intelijensia isiyo na chembe ya siasa katika dunia yetu hii ya tatu hasa Tanganyika tulio fundishwa kuishi kindugu, kusaidiana na kuhurumiana, tuliofundishwa misemo na methali za kuvutia(zimwi likujualo halikuli likakwisha, heri shetani uliyemzoea kuliko malaika usiyemjua nk.). Itanipa shida kukuweka kwenye kitengo wewe nisiyekufaham usije ukaniharibia mipango yangu. Kama ina wezekana, inawezekanaje kufanya tofauti na matakwa ya aliyekuweka katika kitengo ikiwa sote twajua kuwa mkuu wa kitengo cha upekuzi/ujasusi/intelijensia (whatever you call it) hupointiwa? Aina ya demokrasia tuliyonayo sisi wa dunia ya3, pia inanipa shida kuamini kuwa hii kitu inawezekana kwa sasa hapa kwetu.
Nimezisoma bwana ishu siyo kiingereza nakijua sana tu..haya ni maneno ya Internet usije dhani hizi categories zimewekwa na taasisi fulani ya intelijensia ni interests za watu tu kufanya uchambuzi kama huo na kuweka kwenye internet, ndiyo maana kwenye chuo nilichosomea Masters ukiweka reference ya material kuwa umeipata kwenye net imekula kwako!
Huwezi kuimarisha ulinzi wakati watu wanaingia nchini kiholela ati kwa sababu tu ni member wa EAC. Subirini matokeo yanakuja very soon.
kuna kitengo cha wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho hadi sasa kiko free from politics ni CMI (central military intelligence)..., lakini upande wa foreign assets ndo wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi yenu hiyo...,
Hawa wamegawanyika..., kuna wanaofanya kazi kufatilia mienendo na tabia za maofisa na askari ndani ya vikosi hata nje,
kuna wakusanya habari za ndani ya nchi zenye maslahi na jeshi, mfano kuna watu kazi yao ni kusoma magazeti daily, magazeti ya ndani na hata ya majirani au kuangalia tv, au kushinda kwenye mitandao kama humu, pia kuna ambao kazi yao ni kunasa mawasiliano ya jirani zenu...,
na kuna foreign assets.., wanaishi na kukaa nje...., kuna wanaotumwa for a specific mission na kuna wanaokaa tu huko kukusanya taarifa yoyote ambayo ina maslahi na usalama wa nchi.., na wapo ambao ni infiltrated kwny majeshi jirani na serikali za jirani
hawa ndo wamebaki kuwa pillar ya nchi from outside threats
Ila ile cream ilokua trained russia, israel, cuba ndo inastaafu..., wamebaki wale mnaowafundisha pale mikumi
nimekuwa nafuatilia sana report zinazoachiliwa na CIA. Inaonesha CIA wanaijua dunia kuliko dunia inavyojijua. NIkaanza kufuatilia mashirika ya Kimarekani ya usalama - Police, FB!, secret service zao unakuja kujua kumbe mfumo wa ulaya unafanana.Eneo kubwa linalofanana ni kwamba mfumo wao wa usalama hauingiliwi na wanasiasa. Ikishafikia habari ya usalama ni wananchi na mali zao! Sasa sisi Tanzania mfumo wetu wa usalama ukoje? Je? ni shirika gani linashika usalama wa tanzania bila kuingiliwa na wanasiasa? halafu tunaweza kweli kuchunguza nchi zingine kwa manufaa yetu?
Mbona wamerakani walienda kumchukua Osama Bin Laden na kumuua bila ya wao kujua??? Je CIA taarifa walizipata wapi? Hebu jifunze kuunganisha dots bana!
wapi? ulikosomea masters Rukwa? walikueleza reference za net hazifai?? inaonekana bado haukumuelewa mwalimu wako mkuu........muulize tena!!! wengine tunafundisha vyuo vikuu humu!
Rukwa? Nina MBA kaangalie chuo cha 4 africa kwa ubora kwa MBA na cha kwanza Tanzania ndiko nilikosomea mimi....
mkuu ni utaratibu gani unaotumika kuwapata hao majasusi?
Pakistan!!!!!!sasa ukisema ya Pakistan je ile ya Israel utaigrade vipi?!
wapi? ulikosomea masters Rukwa? walikueleza reference za net hazifai?? inaonekana bado haukumuelewa mwalimu wako mkuu........muulize tena!!! wengine tunafundisha vyuo vikuu humu!
hii iko conc sana hebu tuone wadau wanasemaje?japo naweza amini kwani niiliwahi kuwa kule kipindi cha uchaguzi walisema hawana nia na muungano kwani hata nyanya walikua wanapata za kopo toka arabuni.mimi nina swali kwa intelijens kabisa, ni kweli eti kuwa hizi harakati za miamsho ya kiislamu zanzibar yenye nia ya kuvunja muungano na kuunda jamhuri ya kiislamu, eti harakati zote zinafanyika iran ili zanzibar pahala bila uchafu wa kimagharibi kama utalii, ulevi, nk, kweli?