Tunahitaji mfumo mpya wa kijasusi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji mfumo mpya wa kijasusi?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by mluga, Dec 8, 2011.

 1. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Miaka 50 ya Uhuru: Tunahitaji mfumo mpya wa kijasusi

  Godfrey Dilunga

  TAKRIBAN miaka 17 iliyopita, Januari mwaka 1994, aliyekuwa Rais wa Urusi, Boris Yeltsin, aliunda upya Shirika la Kijasusi nchini humo, maarufu kama KGB (Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti).

  KGB (Kiingereza; Commitee for State Security )ni kati ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani yaliyopata kutambulika hivyo. Mwaka 1983 kwa mfano, Jarida la Time liliripoti kuwa shirika hilo ni bora zaidi katika kukusanya taarifa za kijasusi.

  Wakati Yeltsin akiwa madarakani, KGB ilikuwa chini ya Wizara ya Usalama ya Urusi. Uamuzi huo wa kuvunja wizara na shirika hilo lenye rekodi ya ubora duniani linatusogeza katika swali la msingi; je, kwa nini Yeltsin alichukua uamuzi huo?

  Kwa nini aliamua hivyo tena akipuuza rekodi kongwe na bora ya shirika hilo? Maelezo yaliyotolewa nyuma ya uamuzi huo ni kwamba; shirika hilo halikuweza kukabili changamoto za mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa kama alivyotaka Rais.

  Kwa lugha nyingine, KGB ilikuwa kikwazo kwa Rais Yelstin kuongoza nchi kwa kasi aliyoitaka hususan mabadiliko ya msingi kiuchumi na kisiasa.

  Ingawa katika kueleza sababu za uamuzi huo Yeltsin pia alikuwa na ‘hasira' binafsi, lakini angalau pia ndani ya uamuzi wake aligusa mambo ya msingi kwa maslahi ya nchi yake.

  Ndiyo, Yeltsin alikuwa na ‘hasira' binafsi pia na hasa pale alipopata kueleza kuwa kati ya sababu za uamuzi wake huo dhidi ya KGB ni pamoja na shirika hilo kwa kushirikiana na Wizara ya Usalama, kutompa taarifa kamili za uchaguzi.

  Alidai KGB na Wizara ya Usalama kwa pamoja walishindwa kumpa taarifa kamili juu ya uwekezano wa chama cha Liberal Democratic (LDP), kupata ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika Desemba 12, mwaka 1993.

  Pengine kwanza tuelezane baadhi ya kazi za msingi za KGB ambazo ziko bayana katika machapisho mbalimbali ya masuala ya ulinzi na usalama na labda, kwa kuzingatia kazi hizo, Yeltsin aliona kuna tatizo na hivyo mabadiliko yalihitajika.

  Mbali na jukumu la kupambana na mitandao mizito ya uhalifu, KGB ilikuwa na majukumu mengine ambayo ni kukabili mbinu za majasusi wa nchi nyingine ambao huingia Urusi kwa malengo maalumu.

  Malengo hayo maalumu ni pamoja na kutaka kujua siri za nchi hiyo ambazo zinaweza kutumika na nchi nyingine hasimu kusababisha maafa au kuyumbisha Urusi (wakati huo Umoja wa Kisovieti).

  Ili tuelewane vizuri zaidi kuhusu eneo hilo mahususi kimajukumu (nchi moja kufanya ujasusi dhidi ya nchi nyingine), nirejee mfano wa tukio la Aprili, mwaka 1999, wakati Marekani ilipofanyiwa ujasusi na China ambayo kupitia kwa ‘jasusi' wake waliiba teknolojia kutoka maabara ya Marekani.

  Ilikuwa hivi; Aprili, 1999; Marekani (kupitia shirika lake la ujasusi CIA- Central Intelligence Agency) ilikuwa ikiendelea na uchunguzi dhidi ya wizi wa taarifa za siri kuhusu masuala ya nuklia, kwenda China.

  Aliyekuwa Waziri wa Nishati wa Marekani, Bill Richardson, Aprili 28, mwaka huo alithibitisha kuwa, Wen Ho Lee, mwana-sayansi wa kichina (jasusi?) aliyekuwa akifanya kazi katika Maabara ya Taifa la Marekani ya Los Alamos, amefukuzwa kazi tangu mwezi uliopita (Machi).

  Alifukuzwa kwa tuhuma za kuiba siri hizo na kuzituma kwao China. Katika ‘wizi' wake, Wen Ho Lee, alifanikiwa kusafirisha kiwango kikubwa cha takwimu (data) kutoka kompyuta za Marekani zenye kiwango cha juu cha ulinzi.

  Tukio hili lilikuwa zito katika masuala ya usalama Marekani na Aprili 21, mwaka 1999, maofisa ujasusi wa Marekani walifanya tathmini na kutoa taarifa kwa Rais na Bunge (Congress).

  Katika taarifa hiyo walikiri kwamba China imefanikiwa kunasa data kuhusu silaha za nyuklia na kwa hivyo, China ipo rasmi katika ujasusi dhidi ya Marekani.

  Kama nilivyoeleza awali, huu ni mfano tu kwa hiki ninachoeleza kuhusu uamuzi wa Yeltsin kuvunja KGB na moja ya majukumu ya KGB kuwa ni kudhibiti majasusi wa nchi nyingine wanaoingia katika nchi yao.

  Majukumu mengine ukiondoa hilo na mfano niliotumia, ni pamoja na kuhakikisha ulinzi wa nchi, kuendesha oparesheni maalumu za kijasusi, kudhibiti huduma za mawasiliano baina ya Rais na Serikali na masuala mengine nyeti.

  Baada ya uamuzi huo wa Yeltsin kuvunja KGB, itakumbukwa kuwa msemaji wake (Rais) kwa wakati huo, Viacheslav Kostikov, alitoa ufafanuzi kuhusu hatima ya majasusi ambao ‘kibarua' kimefikia mwisho.

  Kostikov alieleza tu kwamba wafanyakazi waliokuwa wa Wizara ya Usalama watahamishiwa katika idara nyingine za Serikali na baadhi ya majasusi watahamishiwa katika shirika jipya litakaloundwa kwa vigezo maalumu.

  Pengine kama ilivyokuwa kwa Rais Yeltsin, hata hapa Tanzania kwa sasa kuna viashiria dhahiri hatuna mfumo imara wa kijasusi na kimsingi, tunahitaji marekebisho makubwa ambayo kimsingi ni sawa na kuweka mfumo mpya.

  Sijui kwa kina kuhusu masuala yetu ya kiusalama (kijasusi) lakini ni dhahiri kuna udhaifu wa mfumo wetu huo. Udhaifu huu unadhihirika katika baadhi ya michakato ya kitaifa, hasa masuala ya uchumi.

  Mfumo wetu wa utafutaji taarifa nyeti hauna tija na kimsingi una mianya inayoruhusu nchi kudanganywa au kutapeliwa kirahisi mno hata na kampuni kubwa za kimataifa.

  Baadhi wanaamini mfumo wetu bado ni imara isipokuwa taarifa hizo nyeti, mara kwa mara hazitumiki ipasavyo au hupuuzwa kabisa. Hoja hii ni nyepesi mno na binafsi siamini hivyo.

  Mfumo wa kiusalama ambao una mianya inayotoa fursa kwa taarifa zake nyeti zilizokusanywa kwa njia hatari na gharama kubwa kutotumika hata kama zinabeba maslahi ya nchi, huo ni mfumo dhaifu.

  Mfumo wa namna hiyo unapaswa kuvunjwa au kufanyiwa marekebisho makubwa. Mfumo wa kiusalama lazima si tu uwe na uwezo mkubwa wa kusaka taarifa nyeti kwa njia yoyote (halali au kinyume chake), lakini pia unapaswa kujijengea mazingira ya kuhakikisha matumizi bora ya taarifa hizo kwa maslahi ya nchi.

  Kwa mfano, kama kweli tunao mfumo imara wa kukusanya hizo taarifa kwa nini yameibuka madudu mwengi kwenye mchakato wa ubinafsishaji?

  Hata ukiangalia michakato mingine muhimu kwa taifa ‘mikono' ya kitapeli umeshindwa kudhibitiwa, kwa nini? Ni dhahiri mfumo wetu ni dhaifu isipokuwa swali la kujiuliza; je, udhaifu huo uko kwenye eneo gani mahsusi?

  Je, ni eneo la ukusanyaji taarifa au ni matumizi ya taarifa husika? Au vyote viwili? Ndani ya maswali haya, ufumbuzi muhimu unaojitokeza ni kwamba; tunahitaji mfumo imara zaidi wa kiusalama nchini na hasa kwenye eneo la uchumi na siasa kama ilivyo kwa Urusi ya Yeltsin kwa wakati ule.

  Mfumo ambao si tu utakusanya taarifa kwa mujibu wa mahitaji lakini pia taarifa hizo zitajengewa mazingira ya lazima ili kutumika kwa manufaa ya nchi. Hakuna sababu ya kuendelea kuwa na mfumo ambao utekelezaji wa taarifa zake unategemea upeo wa kiongozi mkuu pekee, ingawa pia natambua Rais ni taasisi.

  Tujenge mfumo ambao ingawa utahitaji wanasiasa, wachumi, wahandisi, wanasheria na wanataaluma wengine lakini kamwe usiwe na maslahi ya moja kwa moja na makundi hayo wakati wote. Kwa sasa, inawezekana mfumo wetu umefungamana zaidi na utashi wa baadhi ya wanasiasa kuliko utaifa.

  Tunahitaji kujenga mfumo mpya imara wa kiusalama ambao utakuwa karibu na taaluma zote nyeti lakini hautafungamana na maslahi ya taaluma hizo wala wanataaluma husika.

  Hii itasaidia kujenga mwelekeo wa taifa katika mazingira halisi ya mwelekeo wa dunia na si mazingira ya utashi wa wanataaluma au wanasiasa husika.

  Kwa bahati mbaya, mfumo wetu wa sasa umejenga hisia kwa umma kwamba umetekwa na wanasiasa na zaidi, ni mfumo uliowekeza zaidi katika siasa kuliko eneo la uchumi. Chombo chetu hiki lazima ‘kicheze' vilivyo na kwa ustadi ‘disco' la dunia kuhusu uchumi na siasa.

  Hisia kwamba mfumo wetu wa kiusalama ni dhaifu zina ushahidi. Pale tulipopaswa kudhibiti au kuchukua hatua kabla, tumeshindwa kufanya hivyo na hatimaye kufikwa na madhara yasiyo ya lazima.

  Matapeli ‘wasiojaa hata mkononi' wanaingia popote na kufanya wizi wa mali za umma. Wengine wanafanya hivyo wakijiita wawekezaji wa kimataifa ambao baadhi ya makuwadi wao ni wanasiasa au wataalamu wetu ‘mashuhuri' nchini.

  Kama tunafeli kudhibiti masuala yaliyoko ndani ya uwezo wetu tutawezaje kupanga na kutekeleza mipango ya kupata taarifa nyeti kutoka kwa mataifa mengine ili tujenga taifa bora zaidi katika ushindani wa kidunia?

  Kwa nini hata wale wanaojifunza au kuchipukia kwenye utapeli wa kimataifa (wawekezaji), Tanzania iwe sehemu yao ya mazoezi?
  Katika mwaka huu wa 50 tujiulize na kutafakari je, tunasababu ya kuendelea kuwa dhaifu ndani ya nchi yetu na hata nje ya nchi? Kama jibu ni hapana, basi sehemu ya kuanza kufuta udhaifu huo ni kuimarisha au kujenga upya mfumo wetu wa kiusalama. Happy birthday Tanganyika.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tumeshapiga kelele sana kuwa Nyakati zimefika sasa Tanzania ibadilike, tunaitaji kuwa na shirika la KIJASUSI lugha ngumu, au kwa lugha laini shirka la usalama wa Taifa. Kwa ukweli tulipofika tunahitaji shirika jipya la kisasa lenye watu wenye uwezo wa kuendana na kasi mpya ya dunia hii inayokimbia kwa kasi kubwa.

  Ni wakati Mwafaka Watanzania wakamiliki shirka ambalo Watanzania watakuwa na taarifa kamili la kujua kazi za shirika lao ni zipi,lakini wasiojua linatekeleza kwa nani na muda gani.[kwa kuwa kazi za kijasusi ni kaziz za siri]. Ni vema sasa Watanzania wakawa na shirika ambalo watajua kuwa uarifu mkubwa,uhujumu wa uchumi, rushwa, uhaini na matendo amengineyo yote yanayohusu usalama wa raia na kama mmmoja mmoja au kundi au Taifa kwa ujumla una jicho la tatu ambalo kazi yake ni kukusanya profile za kila mmoja wetu.

  Linatakiwa shirika lenye picha ya utaifa na sio picha ya chama au kikundi cha watu. Shirika ambalo watu wake wanakula yamini [Kiapo] kulilinda Taifa, watu wake, na Mali asili zake zote, wakati wowote na saa yoyote ile. Shirika ambalo walioajiliwa kwake wawe ni watu wenye uadilifu [integrite] na welevu [Intellegency] wa hali ya juu katika nyanja zifuatazao

  1: Uchumi
  Katika Nyanja hii ambayo kwa sasa ndio hujuma nyingi za kuatarisha usalama wa Taifa ziliko lala kwa kiwango kikubwa sana. Kulingana na dhama na nyakati za sasa.
  - Tunahitaji walinzi waelevu wenye ufahamu mkubwa sana wa maswala ya uchumi ndani na Nje ya Nchi. Ambao watajua mbinu za kiarifu zenye nia ya kuhujumu Taifa kupitia sekta ya uchumi na wao pia kutoa ushauri makini ni kipi kifanyike kupambana na adui anaekuja kuhujumu Taifa kutoka ndani au nje ya Taifa.
  - Tunahitaji wasomi na wanausalama waliofunzwa kupredict future ya uchumi kulingana na taarifa zao za kiusalama walizokusanya.
  - Tunahitaji walinzi ambao dakika zote masikio yao na macho yao yanawaza na kuota mbinu na mikakati ya kutulinda sisi Watanzania na kuibua tafiti za kisasa yani za kitaalamu zaidi zitakazo wasaidia wao kujenga na kuunda maliasili watu kwenye sekta ya uchumi na kutoa taadhali ya tishio lolote linalotishia uvunjifu wa amani kupitia sekta ya uchumi.
  - Tunahitaji shirika ambalo litawajibika kwa mujibu wa UKWELI [FACTS] na sio majungu ya nani anaogopeka Serikalini. Manake anaeogopeka leo Serikalini kesho anaweza kuwa ndiye adui number moja wa TAIFA.

  Tufike sehemu tuseme basi kuwa TAIFA lahitaji mfumo wetu wa kisasa wenye kuzingatia mazingira ya kitanzania na uafrika. Watu watakao kuwa tayari kuunda mikakati ya kulisaidia TAIFA kuinuka kiuchumi. Watakaoibua na kubuni mbinu kuu za kuinua uchumi kupitia ushauri kwenye Serikali.

  2: Ulinzi wa Taifa

  Hapa tunahitaji aina mpya ya walinzi ambao watakuwa macho kulinda Taifa,watu wake, na mali zake. Hapa ni sehemu ambayo walinzi wake watakuwa na changamoto za kuahakikisha wanakusanya Taarifa za ulinzi ndani na Nje ya Nchi. Teknolojia imekuwa ulinzi kwa sasa unahitaji maarifa ya kutumia mitandao kutoa taarifa na kukusanya taarifa. Mbinu na mikakati yetu iwe ni ile ya kisasa yenye muda mkubwa wa kufikilia zaidi usalama wa TAIFA kwenye pande angle nyingi na sio angle ya ulinzi wa viongozi na bali ni TAIFa kwa ujumla wake.

  3: Siasa

  Tuwe na shirika linaloangalia siasa kama njia tu, na sio msingi imara wa kulinda TAIFA, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa kuwa ndio UTAIFA wenyewe. Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Tunatakiwa Shirika ambalo alitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa.

  4: Fedha
  Ni wakati mwafaka wa kuwa na shirika lenye maarifa na mbinu zote zenye uwezo wa kubaini michezo mibaya dhidi ya TAIFa kupitia kofia ya kifedhaTaifa linaitaji watu wenye welevu kutambua hujum za kitaifa kwenye mazingira ya kifedha, mfano michezo hiyo ni kama Pesa halamu [Money Laundering], wizi, udanganyifu, utapeli na matumizi mabaya ya fedha ya umma kwenye wizara na mashirika ya umma na sehemu nyingine yeyote ile hata sekta binafsi ambako Serikali yetu ina interest zake.

  5: Afya
  Pia huku nako taifa laitaji watu makini kujua taarifa za kiafya za Taifa na watu wake, kuahakikisha uwepo wa Taarifa nyeti juu ya usalama wa watu wetu na mali ya asili yetu. Afya ni kitu cha msingi kwa mwanadamu yeyote yule. Hivyo ulizni wetu kama Taifa ni vyema pia tukazingatia AFYA. TAIFa lenye watu wagonjwa ni kuhatarisha amani na usalama wa TAIFA,

  6: Elimu
  Elimu ni siraha kubwa sana, ikitumika vizuri elimu uleta mapinduzi ya fikra, hivyo TAIFA linaitaji Wanausalama wabunifu na wenye maono kwenye sekta ya elimu. Watakaotoa mwongozo wa elimu sahihi itakayo tumika kujenga na kuinua Taifa.

  7: Madini na Malia asili

  Sekta hii kwa kuwa ni nyeti tunaitaji ulinzi makini na wenye upeo mkubwa,kupambanua maarifa na utekelezaji wenye kukinga,kujenga na kutetea malia ya asili ya TAIFA.

  8: Sekta ya Utamaduni
  Ni vyema ujio wa Shirika hilo ukaja na maarifa yenye kujenga na kutetea Utamaduni wa Mtanzania. Ni sehemu hizi ni mwanya kutumika vibaya kuhalibu jamii. Na hivyo shirika litakuwa ni jicho la jamii na jicho la jamii linaona mbali.
   
 3. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 618
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  nimekuwa nafuatilia sana report zinazoachiliwa na CIA. Inaonesha CIA wanaijua dunia kuliko dunia inavyojijua. NIkaanza kufuatilia mashirika ya Kimarekani ya usalama - Police, FB!, secret service zao unakuja kujua kumbe mfumo wa ulaya unafanana.Eneo kubwa linalofanana ni kwamba mfumo wao wa usalama hauingiliwi na wanasiasa. Ikishafikia habari ya usalama ni wananchi na mali zao! Sasa sisi Tanzania mfumo wetu wa usalama ukoje? Je? ni shirika gani linashika usalama wa tanzania bila kuingiliwa na wanasiasa? halafu tunaweza kweli kuchunguza nchi zingine kwa manufaa yetu?
   
 4. Tanzania Mpya

  Tanzania Mpya JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 248
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Nafikiri wewe mwenyewe una jibu mh, kwamba siasa zetu uchwara zimeingia mpaka sehemu nyeti, badala ya kulinda nchi na raia wao wanalinda kikundi cha watu na chama fulani. Hao hata wauze nchi hutasikia taarifa za kiintelijensia lkn wewe iba kuku utawasikia wamepata taarifa za kiintelijensia! Hapa Tz hakuna chombo cha usalama kisichotumiwa vibaya kwa maslahi ya mwanasiasa fulani. Si unakumbuka kina gen Shimbo? Akina Hosea, DCIA Manumba? tunahitaji kuwa na utawala wa sheria.
   
 5. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 618
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Kama serikali haina mpango wa kuimarisha usalama wa nchi, na sisi tunaona kabisa usalama wetu uko mashakani suluhisho ni nini? tulalamikie nini ili wafanye nini? je? ni rahisi kiasi gani kutenganisha siasa na usama wa nchi?
   
 6. d

  dav22 JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mmhh suali la utata hili...thoough katika kuchambua na kusoma historia ya baadhi ya haya Mashirika nayo yanaathirika na kuingiliwa na Siasa but wanakuwa very serious kwenye Ishu critical na mambo kama haya ya Ufisadi mkubwa wa hapa Bongo kule mbele yangekuwa tayari yameshakuwa solved na watuhumiwa kufikishwa mbele ya sheria kitambo sana
   
 7. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  kuna kitengo cha wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho hadi sasa kiko free from politics ni CMI (central military intelligence)..., lakini upande wa foreign assets ndo wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi yenu hiyo...,

  Hawa wamegawanyika..., kuna wanaofanya kazi kufatilia mienendo na tabia za maofisa na askari ndani ya vikosi hata nje,

  kuna wakusanya habari za ndani ya nchi zenye maslahi na jeshi, mfano kuna watu kazi yao ni kusoma magazeti daily, magazeti ya ndani na hata ya majirani au kuangalia tv, au kushinda kwenye mitandao kama humu, pia kuna ambao kazi yao ni kunasa mawasiliano ya jirani zenu...,

  na kuna foreign assets.., wanaishi na kukaa nje...., kuna wanaotumwa for a specific mission na kuna wanaokaa tu huko kukusanya taarifa yoyote ambayo ina maslahi na usalama wa nchi.., na wapo ambao ni infiltrated kwny majeshi jirani na serikali za jirani

  hawa ndo wamebaki kuwa pillar ya nchi from outside threats

  Ila ile cream ilokua trained russia, israel, cuba ndo inastaafu..., wamebaki wale mnaowafundisha pale mikumi
   
 8. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  kwa marekani..., cia through nsa ndio foreign policy makers, rais wao atake asitake atafata recomendations zao

  kwa mfano russia's fsb, israel's mossad au british mi-6..., ndio foreign policy makers wa nchi zao..., ila mind you, kwenye baadhi ya nchi kuna seperation of duties.., kuna agencies zinazofanya kazi za usalama wa ndani.., hapa ndo tatizo la interference za politics zinapoingia hasa kwa intel agencies zisizoweka weledi mbele.., nadhani umeona secret service walolala na malaya kule colombia kilichowatokea..., wote wamefukuzwa kazi, haijalishi ametumikia muda gani..., principles, integrity and proffesionalism first...,
   
 9. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 618
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Inamaana basi Tanzania huwa hatupendi kujifunza. sote tunafahamu kwamba mwanzo wa ukoloni ulitokana na taarifa za wapelelezi. haijalishi walikuja kama wafanyabiashara au viongozi wa dini. MAFIA ingawa ni genge la kihalifu lakini lilitanuka sana kutokana na kuwa na mfumo mzuri wa taarifa za mtu(hasa mbovu ili waweze kum - blackmail).kwani ujasusi huwa ni kwa ajili ya usalama tu? mimi naamini pia ni pamoja na kujua mahali gani patatunufaisha kiraslimali. Kwa mfano naamini ilipaswa tuwe na data za kutosha juu ya sudani ya kusini (yaani kwa mlengo wa biashara). lakini nashangaa URAFIKI WETU NA MAKABURU UNATOKANA NA INTELIGENCY ZETU AU ZA KWAO? JAMANI KAMA JUZIJUZI TULIWAZUIA KUTAWALA A.KUSINI LEO WATASHINDWA NINI KULIPA KISASI?
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Naomba nitoe angalizo.
  Naona watu wanatolea mifano kwa kuitaja sana CIA. Kwa taharifa yenu Intelligence agency ambayo ni high efficiency na kiwango zaidi Duniani ni ile ya Pakistan, ISI.
   
 11. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Una uhakika?? ISI wangejua long before CIA osama alipokua.., na what about suicide bombers in karachi..,

  ISI wangejua operation ya kumuua osama kabla hata ya tukio lenyewe through intel comm interceptions...,

  Be careful na sources za data zako..,
   
 12. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,940
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  Pakistan!!!!!!sasa ukisema ya Pakistan je ile ya Israel utaigrade vipi?!
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani nina uhakika 100%. Mnaweza mka'google au mkatafuta source zenu zozote mnazoziamini.
  MOSAD ya Israel ni ya pili, CIA ni ya nne.
  Bofya hapa: Top 10 Best Intelligence Agencies in the World - 2011
  Au hata humu:
  10 Best Intelligence Agencies in the World
  Angalizo lingine, Muache ubishi jifunzeni kwanza.
   
 14. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 618
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Mhu! ni vigezo gani vinazingatiwa? mimi nadhani ni MI6 ya uingereza!
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  MI-6 ipo katika top 10 ila haijaifikia ISI.
  Vigezo vinavyozingatiwa ni vingi sana mkuu.
   
 16. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona wamerakani walienda kumchukua Osama Bin Laden na kumuua bila ya wao kujua??? Je CIA taarifa walizipata wapi? Hebu jifunze kuunganisha dots bana!
   
 17. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Brother, umeing'ang'ania misheni ya Osama tu!
  Unaijua kiundani lakini habari za ishu ya Osama?
  Nakushauri tafuta kwanza info na sio kuangalia mambo kijuu juu tu na kusikiliza story za watu.
  nimekupa links hapo juu uone lists za best Intelligence agency na nikakushauri google na wewe ujionee lakini naona kumbe hupendi kusoma? au kwa sababu websites zenyewe zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza?
   
 18. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimezisoma bwana ishu siyo kiingereza nakijua sana tu..haya ni maneno ya Internet usije dhani hizi categories zimewekwa na taasisi fulani ya intelijensia ni interests za watu tu kufanya uchambuzi kama huo na kuweka kwenye internet, ndiyo maana kwenye chuo nilichosomea Masters ukiweka reference ya material kuwa umeipata kwenye net imekula kwako!
   
 19. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sikulijua hilo. Kiukweli mimi sijawahi kufanya research juu ya hilo bali huwa nasoma vitabu na internet ndio napata hizo data.
  Anyway, I appreciate ulichosema.
   
 20. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 618
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Kaka nimeona. Nadhani uko sawa. ukiangalia harakaharaka utagundua kigezo kikubwa ni hali ya usalama. kwa mfano ukiangalia Israel, Pakistan na India ambao ndio wanaongoza hali zao za usalama ni tete sana. Australia ambao wanashika namba 10 unaona kuwa wamejikita kwenye masilahi yao ya kiuchumi zaidi (na hasa ni sector ya madini). CIA wao wako kila mahala lakini usiri wao wa habari sio mzuri ingawa wanawezeshwa kuliko agency yoyote duniani. Swali la ziada, Hivi hii dhana ya kuwa na mpelelezi anayeongoza (kama inavyopenda kuwekwa kwenye sinema na vitabu vya hadithi) huwa ni ya kweli? kwa mfano james bond, willy Gamba, Joram kiango n.k je? ni kweli huwa kuna mpelelezi anayeongoza kati ya wenzake na kujichukulia umaarufu?
   
Loading...