Tunahitaji majumba ya sinema!!!!!!!

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,708
Reaction score
1,733
Mpaka miaka ya kama themanini hivi nchi hii palikuwa na majumba ya kuonesha sinema kama Avalon, New Chox, Empire, Empress, Drive In n.k. kwa Dar es Salaam na mikoani pia palikuwapo majumba hayo kwa majina tofauti kama Diamond Talkies la Tabora n.k. Kilivokuja kimbunga cha CD na DVD basi utaratibu mzuri wa kuangalia sinema hasa ukiwa na familia ukaisha. Wenzetu Ulaya nasikia bado yapo. Majumba hayo (nasikia) yalikuwa yanamilikiwa na Tanzania Film Company (TFM), sijui kama ipo hivi sasa na palikuwa na burudani kwelikwli hasa mwisho wa juma. Jamani si wote wanapenda kuangalia sinema za CD na DVD nyumbani, wito wangu kampuni hii iturejeshee burudani hiyo kwenye majumba hayo kwani mengi bado yangalipo.
 
Na lile pale Moshi stendi pale..panaitwa bora!!!
 
moshi yalikuwepo mawili moja la pale stendi likiitwa plaza na jingine lilikuwa jirani na tanesco likiitwa abc.

Yaaa ABC siku hizi panaitwaje tena...aarghhh ngoja nkumbuke...sijui ndo mr. price?? Kuna cinema hall ila viti vyake sasa...!!!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…