Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,291
- 2,466
Kwa wale wasomaji na wafuatiliaji wa maandiko matakatifu watajua kisa cha Yohana mbatizaji, yule aliyetumwa kuandaa njia katika kusubiri ujio wa Masiha, yani Yesu Kristo.
Herode alikuwa mfalme wakati huo. Naye alitokea kumpenda mke wa ndugu yake, akamfunga nduguye na kumchukua mkewe aliyeitwa Herodia. Herodia alikuwa na binti mdogo mrembo.
Wakati ule wa Herode, Yohana akijua kuwa mfalme hakutenda sawa, alichukua fursa hiyo kumsema mfalme kuwa kitendo alichofanya cha kumchukua mke wa nduguye si chema machoni pa Mungu na wanadamu. Mfalme pamoja na Herodia hawakuwa wakipendezwa na mambo aliyokuwa alisema Yohana juu mfalme. Herode aliamua kumfunga jela.
Turudi kwa Herode na Herodia. Ikawa mfalme aliandaa karamu kubwa na kuwaalika watu wengi mashuburi. Katika karamu yule bintti mdogo wa Herode alipewa fursa ya kuwaburudisha wageni. Naye alicheza mbele ya wageni kwa umahiri mkubwa. Ndipo mfalme alipohamasika sana na kumuahidi binti yake kuwa chochote atakachoomba, hata kama ni nusu ya ufalme wake atampa.
Binti alitoka akaenda kwa mama yake kuomba ushauri. Herodia kwa kuwa alikuwa na chuki na Yohana akaona ndio sehemu pekee ya kumkomoa. Basi akamwambia bintie amwambie baba yake ampatie kichwa cha Yohana kwenye sinia.
Mfalme alifadhaika sana. Hakutegemea hilo. Kwa kuwa alishaahidi kuwa atatoa chochote, hakuwa na jinsi. Walitumwa askari kule gerezani wakamkata Yohana kichwa kisha kikaletwa mbele ya mfalme na binti akakabidhiwa...
Turudi kwetu Tz. Rais amekuwa anafanya mengi. Kweli tunayaona. Mazuri kwa mabaya. Rais anajua anaongoza taifa ambalo lina itikadi tofauti kwa wananchi wake. Alipata dhamana ya kuongoza kwa kuwa ilotokea tu ikawa hivyo. Taifa lilipofikia lilihitaji mwokozi. Taifa linahitaji uratubu mpya wa mfumo. Mfumo uliopo tunasema umeshafikia maturity stage. Lazima ufe! Hakuna kuvua gamba maana gamba linaishia kiunoni tu.
Rais anajaribu ku dilute mfumo kwa kuteua watu wasio wa chama chake kwenye mfumo wa chama tawala. Tunajua uwezo wa vyama vilivyopewa mbeleko na rais. Ni kama hadaa. Watanzania hawataki hivi vitu rahisi kiasi hiki. Wanataka mapinduzi. Wanataka maamuzi magumu, japo wanayafanya ila zinatokea songombingo.
Wananchi wanataka Bunge huru. Wanataka uhuru wa vyama. Wanataka tume huru ya uchaguzi. WANATAKA KATIBA MPYA. Wanataka kichwa cha Yohana. Kinyume na hapo ni sawa na kujitekenya na kucheka mwenyewe. Hayo mambo manne ndio msingi wa Taifa lijalo. Utakumbukwa kwa hayo. Hutakumbukwa kwa flyovers wala standard gauge.
Wako wanaosema kuwa Nyerere alituletea uhuru wa kisiasa, na wewe unatuletea uhuru wa kiuchumi. Kupambana na makinikia si huo uhuru. Kukamua wananchi kodi hadi macho kutoka pima si huo uhuru. Kaa nao hao wawekezaji chemba, tena tumia wataalamu wako wafanye hizo kazi. Si kuna think tank nchini? Si ni ile tume ya mipango? Wape uhuru watu hao. Wape uhuru wapinzani wakueleze mambo mazuri. Waruhusu wakukosoe. All in all... Kichwa cha Yohana, mzee.