Tunahitaji chama kipya?

Tunahitaji chama kipya?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,092
Reaction score
43,265
Najiuliza kama kuna watu wameanza kuwa kama mimi; vyama vyote vya kisiasa vilivyopo nchini haviwezi kutupatia kile tunachohitaji kama taifa.

Siyo CCM, CHADEMA, CUF au TLP ambacho kilivyo sasa kinaweza kuwa tumaini la Watanzania.

Je, kuanzisha chama kingine ambacho kitatoka kwa wananchi na chenye ajenda ya mabadiliko ya kweli na kikiongozwa na watu wenye mwelekeo wa mabadiliko na wasioogopa political confrontation na ambacho hakitasita kufanya what is necessary to restore law and order and a constitutional rule kitaweza kuwa na nafasi.

Chama ambacho mrengo wake itakuwa ni kuhakikisha kuwa hakuna kurembuliana macho na mafisadi tena wala kuufafanua ufisadi bali kuushughulikia moja kwa moja.

Chama ambacho kitalenga kuleta mabadiliko ya kimfumo na kimuundo wa serikali yetu ndani ya miaka mitano ya kuingia madarakani kikibeba ajenda ya mabadiliko ya kweli (kikatiba, kisiasa, na kiutendaji) huku kikiwashughulikia kama simba mkali wale wote ambao wamelifikisha taifa letu hapa ikiwemo kutaifisha mali zao, kuwasweka jela na wale ambao ni vigogo wa ufisadi "kunyongwa" kama wanavyofanya huko China!

Chama ambacho hakitawabembeleza wawekezaji kama wakwe zetu!

Au ndiyo tubanane mumu kwa mumu huku tukiulizana "kajamba nani'!
 
Usitegemee toka kwa NDIVYO TULIVYO.... Ukiweza kuelewa Wadanganyika na jinsi wanavyofikiria mkuu wangu chukua glass ya maji kunywa upoze koo. Ni swala ambalo haliwezekani na ndio maana tumekuwa hapa.
 
Mzee Mwanakijiji,

Tatizo sio vyama bali ni watu, tatizo ni Watanzania ambao wengi ni wababaishaji, wezi, mafisadi.

Tunayoyasema hapa JF hatuyaamini kabisa.

Kama kuna watu wanataka kuleta mabadiliko, tayari tuna vyama vingi, ingieni kwenye hivyo vyama na anzeni mapambano kuanzia chini.
 
Watanzania wakibadilika kifikra basi vyama hivyo hivyo vilivyopo vya upinzani (vikiengezeka vizuri) vitafaa mradi vitakuwa disciplined na watu ambao wamebadilika kifikra.Kama vichwa vya Watanzania wengi vitaendelea kuamini kuwa CCM ndo nambari wani hata kama hakina jipya...basi tunaweza kuwa na vya zaidi ya 300 kama Congo kinshasa...na itakuwa Katibu wa Chama kimoja ni Mwenyekiti wa Chama kingine...

Watanzania wabadilike kifikra na kila kitu kitabadilika...Obama alipokuja na "Change Policy" aliwakuta Wamarekani tayari wameshabadilika kifikra na walikuwa tayari kwa chama au system nyengine ambayo itakwenda sambamba na fikra zao mbadala...hawakuhitaji chama kipya bali kile ambacho kitakua tayari kukubaliana na fikra zao...

Watanzania wabadilike...CCM ya jana si ya leo.
 
Usitegemee toka kwa NDIVYO TULIVYO.... Ukiweza kuelewa Wadanganyika na jinsi wanavyofikiria mkuu wangu chukua glass ya maji kunywa upoze koo. Ni swala ambalo haliwezekani na ndio maana tumekuwa hapa.


unajua I'm getting to that point kwa kweli... tuwaache watawale.. hadi tuchoke
 
Mzee Mwanakijiji,

Tatizo sio vyama bali ni watu, tatizo ni Watanzania ambao wengi ni wababaishaji, wezi, mafisadi.

Tunayoyasema hapa JF hatuyaamini kabisa.

Kama kuna watu wanataka kuleta mabadiliko, tayari tuna vyama vingi, ingieni kwenye hivyo vyama na anzeni mapambano kuanzia chini.

hiyo nayo ni option nzuri sana; lakini katika hivyo vyama ni kipi kitakuwa tayari kukubali ajenda ya mabadiliko?
 
Nafikiri tusitafute vyama tutafute watu waliobadilika kimawazo...walio tayari kubadilika..hata tukianza na wawili...
 
Watanzania wakibadilika kifikra basi vyama hivyo hivyo vilivyopo vya upinzani(vikiengezeka vizuri) vitafaa mradi vitakuwa disciplined na watu ambao wamebadilika kifikra.

Watanzania hawawezi kubadilika fikra kwani fikra walizonazo zinawafaa katika mazingira haya ya kifisadi.

Kama vichwa vya Watanzania wengi vitaendelea kuamini kuwa CCM ndo nambari wani hata kama hakina jipya...basi tunaweza kuwa na vya zaidi ya 300 kama Congo kinshasa...na itakuwa Katibu wa Chama kimoja ni Mwenyekiti wa Chama kingine...Watanzania wabadilike kifikra na kila kitu kitabadilika...

Nimejaribu kuamsha mapambano ya kifikra lakini matokeo yake mgongano unaoendelea ni wa kibinafsi zaidi kuliko wa kifikra. Karibu wanasiasa wetu wote wana fikra zinazofanana!


Obama alipokuja na "Change Policy" aliwakuta Wamarekani tayari wameshabadilika kifikra na walikuwa tayari kwa chama au system nyengine ambayo itakwenda sambamba na fikra zao mbadala...hawakuhitaji chama kipya bali kile ambacho kitakua tayari kukubaliana na fikra zao...Watanzania wabadilike...CCM ya jana si ya leo.

kwanza nani atatokea kuwa Obama wetu!
 
Nafikiri tusitafute vyama tutafute watu waliobadilika kimawazo...walio tayari kubadilika..hata tukianza na wawili...

kwa jinsi watu wamepiga kura tena kuichagua CCM daliili ya uwepo wa watu hao katika nchi yetu is almost zero! Watanzania wamefikia mahali pa kuridhika na maisha wanayoishi na siasa zilivyo zinaendeleza mawazo hayo hayo.

WAliotuangusha katika haya ni vyama vikubwa viwili cha CHADEMA na CUF. Vyama hivi ningekuwa na uwezo ningefuta katika historia yetu na viongozi wao kuwatupa katika kisiwa cha usahaulifu tuanze upya kwani vinasimama leo hii kama kikwazo thabiti na dhahiri cha mabadiliko tuyatakayo!
 
Mzee Mwanakijiji,

Tatizo sio vyama bali ni watu, tatizo ni Watanzania ambao wengi ni wababaishaji, wezi, mafisadi.

Tunayoyasema hapa JF hatuyaamini kabisa.

Kama kuna watu wanataka kuleta mabadiliko, tayari tuna vyama vingi, ingieni kwenye hivyo vyama na anzeni mapambano kuanzia chini.

Swadakta..
tatizo ni mimi na wewe.nilikuwa kijijini hivi karibuni hayo tunayoongea hayapo kabisa,ukiwa fisadi kijijini kwako wewe ni KING/QUEEN.wao neno fisadi kwao halipo kabisa. ukienda huko na msururu wa magari ya kifisadi na mwingine aende na pikipiki ya kukodi wilayani mtapokelewa tofauti kabisa.!!

Kwa hiyo hatuhitaji chama chochote sisi wapenda mabadiliko tuingie humohumo tuwaondoe hao waliopo tuwa-replace na wenye uzalendo. hii mijadala tunayoifanya hapa watu wanaiona.

Nilipokuwa hapo Dar niliusikia mjadala wa nani anamiliki JF mi nilikaa pembeni nawasikia na ni watu wa kawaida sana ,Dada mmoja akipendezwa sana na Mzee Mwanakijiji. Tukaze buti Msg zinafika....mzee mwanakijiji ungekuwa wa kwetu sasa una wake kumi kwa jinsi akina dada wanavyokuulizia.......
 
Chama kinaweza kufunguliwa kama hatua ya kwanza,cha muhimu kwanza ni mabadiliko ya mfumo mzima wa kisiasa.

Tuangalie yale yaliyovikwamisha vyama vingine then from there we can see where we should go and or what we shall do.Vyama vingine vya kisiasa kunyanyaswa na chama chenye kushikilia dola ni tatizo ambalo ni sugu,ni tatizo ambalo moja kwa moja linafuta ile dhana ya demokrasia ya kweli inayotakiwa itokane na utawala wa vyama vingi,sijawahi kusikia USA eti Democrats wakiwa madarakani basi wanaweza kutumia polisi kuwanyanyasa Republicans,ama any federal institution kwa madhumuni ya kutokuwatendea haki wanachama wasiokuwa Demokrats...

Tujue sasa kama tumekubaliana na vyama vingi basi mazingira nayo yawe ni ushahidi wa hilo. Wakati ni wazi kuwa tunayaiga mataifa ya magharibi,bado hata hivyo huwa tuna versions zetu za hayo tunayoyaiga,mfano ni ubepari kugeuzwa na kuwa ufisadi,na hiyo version ya demokrasia yetu ambayo ni maslahi ya mafisadi hao.
 
Mzee Mwanakijiji,

Tatizo sio vyama bali ni watu, tatizo ni Watanzania ambao wengi ni wababaishaji, wezi, mafisadi.

Tunayoyasema hapa JF hatuyaamini kabisa.

Kama kuna watu wanataka kuleta mabadiliko, tayari tuna vyama vingi, ingieni kwenye hivyo vyama na anzeni mapambano kuanzia chini.

Tatizo ni vyama yaliyotokea uchaguzi wa CUF kwa Professor Saffari kukashifiwa au Chadema Zitto Kabwe kuzuiliwa nani anaweza kuviamini vyama hivi kienyeji tu?TLP uchaguzi wao walitaka kugombea wakavuliwa uanachama.

Kibanda alikuwa mkali kama Mbogo sababu kubwa ni mkate wa Tajiri yake kuhatarishwa.uchaguzi wa vijana umeahirishwa hadi miezi sita ijayo sababu Mgombea wa kaskazini alikosa nafasi.

nani Mwenye akili timamu anaweza kujiunga huko Chadema kwenye mazingira kama haya? Zitto ana miaka 16 ndani ya Chadema haaminiwi.jee Mkandara anaweza kuaminiwa?

Hivi karibuni imeletwa Taarifa kuwa Maaskofu wako nyuma ya DR.Slaa /Chadema ambaye alikuwa katibu mkuu wao kwa miongo kadhaa nani atajiunga kwenye chama ambacho hakina maaamuzi ya kikatiba zaidi ya vizee vinne tu?
 
Kule Australia kulifanyika mashindano ya mbio za mbwa. Katika ya mashindano sungura akakatiza kwenye njia za mbio na mbwa wote wakasahau mashindano na wakaanza kumfukuza sungura.

Now: Kwenye uanzishaji wa vyama vya siasa Tanzania kuna nia nzuri tu kama vile mashindano ya mbio za mbwa. Lakini kuna kitu kinaitwa ruzuku ya serikali kwa vyama vya upinzani (sungura).
 
Vyama vyote vya upinzani TZ vina kasoro ambazo ni rahisi kuzi-spot na kutoweka imani kwa wananchi. Hii itafanya tugaragazwe na CCM mpaka tukome, Njia ni kuwa na chama kipya ambacho kitakua na developments framework kwa watanzania. Hata hao wanaojiita wapiganaji unaweza kuta wemgine wanaham yakuamia upinzani, ila wakiona structure ya vyama vya upinzani wanaamua kubaki CCM

Angalia Prof safari alivyo aibika, nani yupo tayari kwenda TLP? CHADEMA no comment.
 
Kule Australia kulifanyika mashindano ya mbio za mbwa. Katika ya mashindano sungura akakatiza kwenye njia za mbio na mbwa wote wakasahau mashindano na wakaanza kumfukuza sungura.

Now: Kwenye uanzishaji wa vyama vya siasa Tanzania kuna nia nzuri tu kama vile mashindano ya mbio za mbwa. Lakini kuna kitu kinaitwa ruzuku ya serikali kwa vyama vya upinzani (sungura).
u r damn right
ukiangalia critically UPINZANI wetu na shida CCM wanazotupa utaamua kukaa kimya tu ufanye mambo yako, usomeshe wanao na kusaidia wazazi wako na kuomba mungu akusaidie bass.
 
Mwanakijiji, hilo kwa sasa halitakiwi. Tuna vyama vingi vya siasa, tena vingi kupita tunavyohitaji, hakuna kipya kitakachokuwa na jipya.

Cha muhimu kwetu ni kuwa tunatakiwa kuwaonesha hawa wanaoongoza vyama na serikali kuwa hatutaki ujinga, kama ingewezekana tuwachape viboko kuwafahamisha kuwa wametuudhi. Sio wa CCM peke yao hata wengine ambao wanatumia vyama vya siasa kama mradi wa kujiingizia pesa, na kututumia wananchi kama madaraja.

Ili tuondoe ile Ndivyo tulivyo, we need to teach them a lesson that we are no longer fools. Kama tuykishindwa kufanya hivyo wataendelea kutuchezea tu, hata chama kingine kikija it will be the same old s**t, different party.
 
Vyama ni vizuri tatizo hao watu, hebu tuwabadilishe kwa kutowachagua kwenye chaguzi zijazo jamani
 
Back
Top Bottom