Tunahangaika kutafuta fedha watoto wetu nani atawalea?

Watanzania hasa vijana wa sasa wanaishi fake life, kila kitu ni fake ,fake, fake.......na nitarudia mpaka kesho you guys your living fake life........mnaishi maisha ya Ulaya, Tanzania....mnajifanya mko busy na kazi kumbe siku nzima mmeshinda JF na kwenye mitandao mingine.......mnajifanya mnabeba malaptop na ma ipad kumbe hamna kitu ni facebook na mainstagram na pornvideos tu yamejaa huko ndani....mnasahu cultural na hata familia zetu........mnapotoshwa na marafiki zenu wanaoishi huko Ulaya na America......eti mnataka kushindana kwenye kwenda outing na mavazi...ni aibu leo hii hata chupi unayovaa unaipiga picture dunia nzima inaona....ni aibu sana. Mnawatesa watoto wenu kwa kufanya mambo ya kuiga.......acheni hizo bwana. Hamna ubuzzy Tanzania....linchi liko tu kila kitu hakiendi kuanzia private sector mpaka government sectors....sasa niambie huo ubizy uko wapi....si mambo yangeenda. Leo unakutana na mdada wa heshima kakaa kwenye computer ofisini unafikiri anafanya kazi kumbe anaangalia aina za mishono ya mavazi kwenye internet....wanaume tulo buzy kutafuta madem online.....upuuzi mtupu huu. Hamna ubuzy wowote ni unafiki tu. Unafikiri ukimpeleka mtoto kuogelea jumapili ndio umemaliza.? unampeleka ili tu upige picture uweke kwenye mitandao watu wakuone na wewe una mtoto lakini ukweli utabaki wewe sio mlezi. Nashikwa na hasira sana watu mnaishi maisha ya vitabu na TV. Ujinga mwingine ni huu wa mtu kuzaa watoto wawili alafu anasema hawezi gharama ya watoto zaidi ya wawili.......upuuzi huu.......li nchi likubwa lina watu Milion 40 wakati vi nchi vidogo ulaya vina watu kuanzia milioni 80 kwenda juuu.....leo hii mnadanganywa fateni nyota ya uzazi na nyie mnadanganyika.....nchi ina mapori kila kona.......nawaambie kizazi hichi cha ngozi nyeusi kitafutika mda si mwingi....inakuaje wao wana ardhi ndogo na maradhi watuambie sisi wenye ardhi kubwa na mali nyingi tupunguze kuzaliana?......upuuzi mtupu huuu.
Aiseee basi...basi mkuu umeongea kwa uchungu mkubwa,wazazi tuko bize tukiitwa kwenye vikao vya wazazi kuzungumzia maendeleo ya watoto hatuendi,na tatizo kubwa ni wazazi ule uhusiano uliokuwepo kati ya mzazi na waalimu haupo hii ni kutokana na kwamba wazazi wanajifanya wana uchungu na wanao hata ikitokea mtoto amekosea akaadhibiwa mzazi anakuja juu,kwa hiyo ule wito wa waalimu kuwa kama mzazi wa mwanafunzi umepungua sana,waalimu wamebaki kufanya majukumu ya kufundish tu ili wapate mshahara wao suala la ulezi wamelipiga chini kwani hawapati ushirikiano kwa wazazi matokeo yake ndiyo kama hayo.

Basi wazazi katika ubize wetu na watoto wawe sehemu ya huo ubize,watu hapa kila mtu anasema Mungu atusaidie je huyo Mungu anatusaidia bila kumuomba? na unapomuomba unatimiza majukumu yako? huwezi kumuacha mtoto peke yake eti kisa mama fulani yupo bila kumuomba huyo mama fulani akuangalizie mtoto kwa muda utakaokua umetoka. Tumuombe Mungu huku tukitimiza sehemu ya majukumu yetu ya ulezi kwa watoto
 
Usichoke pambana nayo tu mpaka uyashinde, mie niko poa namshukuru Mungu. Jitahidi basi usipotee muda mrefu hivyo.

Niko bana maisha yananitenda ila niko....niaje lakini???
 
Usichoke pambana nayo tu mpaka uyashinde, mie niko poa namshukuru Mungu. Jitahidi basi usipotee muda mrefu hivyo.

Usijali BAK wangu am back now....in full force ila kucatch up kidogo itakuwa shughuli
 
Bila hata ya ufumbuzi wewe mwenyewe unaona hali inavyobadilika kila siku zinavyoenda watoto wanawahi sana ufuska, magonjwa ya milipuko yamekuwa mengi, ajali nyingi, watu wanapukutika kama kumbikumbi. Kifupi majanga yamezidi sana.

Wewe mwenyewe sema ukweli kipindi ulipokuwa mdogo na sasa hivi huoni kuna tofauti kubwa nina uhakika hata msiba udogoni ulikuwa unaogopa sasa hivi imekuwa kitu cha kawaida kwa watoto kukiwa na msiba wala hawastuki kwa sana.

Kwa jinsi hali tu ilivyo inaonyesha kwa kiasi kikubwa maisha yamebadilika kupita kiasi

Kukiwa na tatizo lazima solution ipatikane, kama hamna ufumbuzi na badala yake kila mtu "Mungu atusaidie" hains mashiko kabisa.

Wazazi wameacha kulea wanatafuta mali, sijui hizi Mali wanamtafutia nani, watu hawaridhiki...wanawategemea "dada wa kazi" ambaye hata hivyo wanamtesa kwa kutompa mshahara, ama kumpa mshahara mbuzi, kila kitu afanye yeye. Hata mda mfupi ambaye mko nyumbani hamtaki kufuatilia mienendo ya watoto....kila kitu ni dada...

Vifo vinaongezeka, maradhi yanaongezeka...uasi umezidi, ni tafrani tu sasa hivi.
 
Pongezi nyingi kwako Mtoa mada!,Hakika umeudhihirishia umma ni jinsi gani ulivyo HAZINA NJEMA KWA USTAWI WA JAMII YETU!,binafsi huwa najisemeaga "Kazi yoyote itayoonesha dalili za kunikeep busy kiasi cha kutokuwa na muda wa kuingalia familia yangu kwa ukaribu basi sitasita kuiachilia mbali!,KWANGU MIMI THAMANI YA USTAWI WA FAMILIA NI ZAIDI YA THAMANI YA FEDHA"
 
Maisha kwa sasa yamekuwa na changamoto nyingi sana hasa kwa wale wanaoisha Dar watanielewa zaidi..
Tunahangaika sana kutafuta hela na kuhakikisha watoto wetu wanapata mlo wa kila iitwapo leo..
Tunatoka nyumbani saa 10 Usiku watoto wamelala tunarudi nyumbani saa 4 usiku watoto wamelala..
Hatujuai tabia na mienendo ya watoto wetu..

Tumeshindwa kuelewa tofauti ya kulea watoto na kulisha watoto kitu ambacho wengi wetu ndio tunachokifanya kila siku,,Dada mtoto amekula? ameenda shule? weka net vizuri si unajua kuna ugonjwa wa dengu?.haya ndio maongezi yetu ya kila siku..

Rafiki yangu wiki iliyopita akapata wito kutoka shuleni anakosoma mwanae wa kike wa miaka 12 ambaye yuko darasa la tano..ni mtoto mdogo sana kiumbo ila kwa muonekano amesha vunja glass zote kabatini..
Waalimu wakazungumza na mzazi na kumpa counseling kabla ya kumpatia mkanda wakiogopa siku hizi presha ni nyingi ya presha juu,presha ya chini, presha ya katikati..

Huwezi kuamini mambo ya ulimwengu huu. mtoto tayariiii!!!! siku nyingi tu mbona!!! kaisha haribikiwa, waalimu wakampatia list ya majina 6 ya wanaume ambayo mtoto amewataja kwamba wanamshiriki karibia kila iitwapo leo, wengine ni class mate zake...

Baba wa mtoto hajui cha kufanya zaidi ni presha, mara kichwa kinauma, mara tumbo la kuhara...
Ndugu zanguni tunahangaika kutafuta fedha watoto wetu ni nanai atawalea??

True kabisa,sijui solution ninn?
 
True kabisa,sijui solution ninn?

Katika maisha haya muhimu ni kujaribu ku-balance at any cost mtu usielemee upande mmoja ukasahau majukumu mengine. Tatizo ni kuelemea upande mmoja kuwaridhisha maboss wetu mpaka watoto tunawasahau. Wazazi wetu wangekuwa hivyo wallahi kizazi cha miaka ya sabini na themanini kingekuwa balaa.
 
Ni sawa ,,ila foleni ndio tatizo sio kazi
 
haya maisha, kihwa kinauma ukifikiria, kijijini hapo ninapokaa kuna jamaa na mkewe wananichukia kwa utata niliowafanyia, mkewe jamaa anamdogo wake wa kiume akaanza kuzoe home kimtindo binti yangu mkubwa akiwa likizo, mimi nikiwa safarini na mamake akiwa nje kimasomo, sasa niliporudi nikahisi kitu kumuuliza mama nikaambiwa tabia ya huyo dogo, sikukawia asubuhi nikatoa mtutu nikaanza kuusafisha....
ikatokea jamaa akapita nikamueleza kuwa sitanii nitaua amwambie shemegi yake asikatize hapa hapa home.
najua ni ngumu sana haya malezi lakine some measures we need to take.....

Haa haa....naona wewe unaenda the hard way...unahama kutoka kwenye kulea unaenda kwenye mikwara ya bunduki...anzia na ku-guide jamii yako kwanza ndio umalizie na gobore...Utawatisha wa nje kumbe wa ndani anafungua mlango na kutoka...

Ila bado mkwara unalipa...
 
mkiambiwa mfanye maombi na mbadilishe tabia mnaona mnazinguliwa...mtajiju
 
ubusy unaangamiza familia kwa sasa ukichanganya binadamu wamekuwa zaidi ya wanyama kila wakionacho wanararua.........wazazi/ walezi tunatakiwa kuweka mikakati thabiti kusaidia familia yako haitakuwa na maana hata unaowatafutia hawapo salama......tuhakikishe tunatenga muda wa kuongea na watoto na kupata chochote kutoka kwao inawezekana wakawa na jambo wanataka kushare nawe mzazi/mlezi lakini hawapati nafasi
 
Unapo acha malezi kwa third party tarajia matokeo mabaya.wengine wana ajiri h/girl 2 au 3 zaidi kujipa hope kwamba watoto watahudumiwa na kulelewa vyema.Wengi hawajui kwamba hawa wasichana wanaongea lugha ile unayopenda kuisikia.
hata udhibiti wa hao watoto h/girls wengi hawana.Mfano watoto wetu wana anagalia sana movies.Mambo ya kiss,romance,na sexy body language zote wanazijua.Wenyewe mmejifungia chumban,watoto wanajua nin kinaendelea huko.MZAZI KUHUSIKA MOJA KWA MOJA NA MALEZI NDIO SULUHU.
 
Hata kama nina kazi kiasi gani,kuna muda wa kazi na muda wa familia,my kids are my evry thing!,wazazi mjue thamani ya wtt wenu!dunia inarudi kinyume nyume cku hizi!
 
Watanzania hasa vijana wa sasa wanaishi fake life, kila kitu ni fake ,fake, fake.......na nitarudia mpaka kesho you guys your living fake life........mnaishi maisha ya Ulaya, Tanzania....mnajifanya mko busy na kazi kumbe siku nzima mmeshinda JF na kwenye mitandao mingine.......mnajifanya mnabeba malaptop na ma ipad kumbe hamna kitu ni facebook na mainstagram na pornvideos tu yamejaa huko ndani....mnasahu cultural na hata familia zetu........mnapotoshwa na marafiki zenu wanaoishi huko Ulaya na America......eti mnataka kushindana kwenye kwenda outing na mavazi...ni aibu leo hii hata chupi unayovaa unaipiga picture dunia nzima inaona....ni aibu sana. Mnawatesa watoto wenu kwa kufanya mambo ya kuiga.......acheni hizo bwana. Hamna ubuzzy Tanzania....linchi liko tu kila kitu hakiendi kuanzia private sector mpaka government sectors....sasa niambie huo ubizy uko wapi....si mambo yangeenda. Leo unakutana na mdada wa heshima kakaa kwenye computer ofisini unafikiri anafanya kazi kumbe anaangalia aina za mishono ya mavazi kwenye internet....wanaume tulo buzy kutafuta madem online.....upuuzi mtupu huu. Hamna ubuzy wowote ni unafiki tu. Unafikiri ukimpeleka mtoto kuogelea jumapili ndio umemaliza.? unampeleka ili tu upige picture uweke kwenye mitandao watu wakuone na wewe una mtoto lakini ukweli utabaki wewe sio mlezi. Nashikwa na hasira sana watu mnaishi maisha ya vitabu na TV. Ujinga mwingine ni huu wa mtu kuzaa watoto wawili alafu anasema hawezi gharama ya watoto zaidi ya wawili.......upuuzi huu.......li nchi likubwa lina watu Milion 40 wakati vi nchi vidogo ulaya vina watu kuanzia milioni 80 kwenda juuu.....leo hii mnadanganywa fateni nyota ya uzazi na nyie mnadanganyika.....nchi ina mapori kila kona.......nawaambie kizazi hichi cha ngozi nyeusi kitafutika mda si mwingi....inakuaje wao wana ardhi ndogo na maradhi watuambie sisi wenye ardhi kubwa na mali nyingi tupunguze kuzaliana?......upuuzi mtupu huuu.

Maneno kuntu haya!!
 
Back
Top Bottom