Tunaendelea kumuonea aibu, kumlinda na kumsitiri

Tunaendelea kumuonea aibu, kumlinda na kumsitiri

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,797
Reaction score
165,542
Watu bado hatutaki kuamini huyu mtu ni tatizo,anatutia umasikini na hana nia njema na nchi hii.

Watu hawataki kujiuliza ana agenda gani hasa na nini anakitafuta au anafanya maandalizi ya jambo gani huko mbele.

Watu wamebaki kumtukuza kwasababu ya nafasi yake, na wale wote wanaojaribu kuhoji au kufichua yanayoendelea, wanaishia kushambuliwa na wale wa upande wa pili ambao kwa ujinga tu wanafurahia bila kutafakari au kujua kesho itakuwa ni zamu yao.

Mtakuja kushituka kapata majority anayoitaka na atabadilisha vifungu ili kujiimarisha then wote mtakuwa kama vijakazi wake.

Kama leo hii anatoa maagizo nyinyi wa chama chake mjieleze kwa kutokuwepo mjengoni na taarifa za gazeti moja la jana kuwa ni kweli mmeanza kujieleza, ni lazima mjiulize hali itakuwaje huko mbeleni iwapo atafanikiwa katika azima yake hii.

Haya yote mnayoyaona anayafanya na ambayo yanaokenekana ni mazuri yana lengo moja tu la kuwapumbaza na kuwafanya msiwaze nje ya box na ndio maana anatumia nguvu kubwa sana ya media hata kwa mambo ambayo ni ya kawaida kabisa.

Mpaka sasa ameshaonyesha dalilili zote na ndio maana watu makini hata kwenye chama chake kwa sasa wanajizuia kumuonyesha kumuunga mkono tofauti na siku za mwanzo.

He is there not only to stay, but also to do anything whether you like it or no.

Uzuri JF ina-keep records, iko siku mtaurejea huu uzi na kusema watu mnaona mbali.

Time will tell.
 
Nkurunzinza Mbowe ni mwenyekiti wako wa kudumu umeshindwa kumtoa unaanzia kurukia kwa mambo ya kufikirika ya JPM. Pambana na Nkurunzinza Mbowe kwanza ndio uanze kufikiria ya kufikirika yako.
Hata TL alipowashauri mliishia kumbeza na kumshambulia mkiamini boss wenu ndio yuko sahihi ila leo ni aibu tupu kwani hata kishika uchumba kimegeuka ndoto.

Uwezo wenu wa kuomba mbali ni mdogo sana.
 
CCM inaburuzwa kuliko hata buzi linavyoburuzwa na nyumba ndogo ! mtu mmoja anajiamulia kila jambo as if wengine ni mifugo yake ! unajua pamoja na Utukufu aliokuwa nao Bwana Yesu bado alikuwa anapokea busara za wanafunzi wake .
 
Hata TL alipowashauri mliishia kumbeza na kumshambulia mkiamini boss wenu ndio yuko sahihi ila leo ni aibu tupu kwani hata kishika uchumba kimegeuka ndoto.

Uwezo wenu wa kuomba mbali ni mdogo sana.

Wewe Salary Slip ndio mwenye uwezo wa kuona mbali? Ila umeshindwa kuona anguko la CDM ? Unafiki mtupu huna hoja.
 
ni vema ukijikita kwenye mada husika mkuu .

Vipi hutaki tuongelee Unkurunzinza wa Mbowe, kwa kuwa Mbowe alibadili katiba ya CDM 2016 na kuondoa term limits unafikiria na Magu atafanya ujinga huo huo? Hivi uchaguzi wa mwenyekiti CDM umefutwa tena, tangu 2013 hadi leo ni miaka 6 sasa, katiba ya CDM inakanyagwa ila upo hapa kuanzisha mada za kufikirika.
 
CCM inaburuzwa kuliko hata buzi linavyoburuzwa na nyumba ndogo ! mtu mmoja anajiamulia kila jambo as if wengine ni mifugo yake ! unajua pamoja na Utukufu aliokuwa nao Bwana Yesu bado alikuwa anapokea busara za wanafunzi wake .
Mkuu nitolee utata huu..
Hivi were no jinsia gani? I'd yako haieleweki
 
Maneno ya Salary Slip msiyabeze. Kuna overreach za ajabu. Mbunge kutokwenda bungeni si suala la rais kumuuliza au hata chama chake kumuuliza in public. Yeye kama Mwenyekiti wake akaumuulizie huko kwenye chama. Utoro wa mbunge unashughulikiwa na Spika kwa kutumima kanuni za kibunge. Masuala ya bunge ni nje ya shughuli za rais wala za mtu awaye yote nje ya bunge. Siku hizi rais ni zaidi ya mbunge.

Juzi juzi hapa viunga vya Dodoma, wabunge wa CCM wakatoka kwenda lunch wanalia lia kuwa mwenzao mmoja alipangwa kamati fulani. Alipohudhuria kamati siku ya kwanza akauliza maswali mazito, kesho yake ikaja simu kutoka juu kwenda kwa Spika kumwamuru amuondoe mara moja kwenye kamati. Spika kwa unyonge akamwita mbungena kuanza kunawa mikono, "unajua Mheshimiwa, Bwana Mkubwa kaja juu wewe kuingia kamati hiyo, kwa hiyo nakuhamishia kamati nyingine. Tuvumiliane ndugu yangu unajua ah..".
 
Back
Top Bottom