Pretty
JF-Expert Member
- Mar 19, 2009
- 2,579
- 574
Katika misingi ya mila na desturi zetu tulizojijengea toka enzi za mababu na mabibi zetu, linapotokea suala la msiba sehemu yoyote, watu hujikusanya sehemu husika wakiwa na huzuni kubwa kwa kuomboleza na kumfariji mfiwa.
Msiba utaombolezwa nyumbani kwa mhusika na hapo mipango yote ya mazishi itafanywa na mambo mengine ya vyakula na vinywaji kwa ajili ya wafiwa na waombolezaji waliofika kujumuika nao.
Michango itapitishwa kwa kuweka daftari kwenye sinia kwa ajili ya kumbukumbu za mahesabu au sahani na kila anayeingia kwenye nyumba ya msiba, huwajibika kuchukua daftari na kuandika jina lake kisha kuchangia kiasi anachoona kuwa kinafaa au alichojaliwa kuwa nacho kwa wakati huo ili kusaidia shughuli za msiba.
Kwa upande wa akina mama ambao mara nyingi huwa na vyama vyao vya kuzikana, huwekeana viwango vya kuchangia hasa linapotokea suala muhimu la dharura kama hilo.
Katika namna yoyote mara nyingi kwa wanawake, mavazi maalum yanayovaliwa katika mazingira kama hayo ni khanga. Wengi huvaa khanga mbili, moja akiwa amejifunga kiunoni na nyingine amejitanda kuanzia mabega huku baadhi yao wakijifunga kilemba kichwani.
Kama pengine hakufanikiwa kuvaa khanga, basi atakuwa amefunga kitenge kiunoni na khanga atakuwa amejitupia kwa juu. Au kuna wengine wasiopenda kuvaa khanga wala vitenge, utakuta wamevaa nguo ndefu ambazo huja na mitandio yake (maarufu kama madira).
Akina baba wao, hawana makuu katika mavazi mara nyingi ni suruali na shati, au kanzu na kofia juu na kwa wale wanaopenda kuvaa suti ni sawa tu.
Siku za hivi karibuni hali hiyo imeanza kubadilika, sijui ni kutokana na mambo ya utandawazi,dunia kuonekana kama kijiji kimoja kikubwa, kutokana na kuaangalia kwenye luninga na kuona wenzetu wanavyovaa na baadhi yetu kujikuta wakitumbukia kuiga kila kitu bila ya kuchuja.
Kwa baadhi ya misiba utaona jinsi akina dada wanavyovaa unashindwa kuamini kama kweli wameenda pale kwa ajili ya misiba au wamekosea njia walikuwa wanakwenda kwenye 'miradi' yao .Kwa mtu makini na mwenye akili timamu, ukiwatazama unabaki midomo wazi na kujiuliza huyu amekuja kwenye msiba au mawindoni ? Nafikiri anapopata habari ya msiba tu, kwanza huanzia salun kutengeneza nywele na kuukarabati uso katika namna ya kuvutia soko kinguvu.
. Akitoka hapo anavyomeremeta utafikiri anaenda kwenye sherehe ya harusi. Ukija kwenye mavazi hapo ndo utachoka kabisa. Sawa kuna wengine huvaa suti Kuna baadhi unawashuhudia wakienda misibani kwa magari yao hadi makaburini, lakini kabla ya kushuka ili kujumuika na waombolezaji ili kukamilisha safari hiyo ya mwisho ya marehemu hapa duniani , anachukua poda, wanja na kuanza kujisiliba kiuhakika au magauni meusi, kofia na miwani mweusi ya jua lakini nguo hizo zinakuwa za heshima.
Kuna baadhi utawakuta wamevaa suruali za kubana mwili halafu anachukua kimtandio chepesi na kukifunga kifundo kiunoni katika namna ya uchokozi, hapo unajiuliza huyu anaenda kumfariji mfiwa au anaenda kumsanifu? Au anakwenda kwenye msiba kujionyesha? Tena akipita sehemu ambayo akina baba wameketi, hata mwendo unabadilika na kuwa kama wa twiga katika hifadhi ya taifa anayatia majani ya nchani. Watu wanaofanya mambo hayo, huvizia misiba ya watu wenye maarufu au wenye majina makubwa , kwa sababu wanajua huko ndiko watu wengi wenye majina na hadhi zao hufika. Kwa kweli haipendezi.
Hata staili ya kulia hubadilika, utamuona mtu ameshika leso yake na kujikanda kanda kwenye macho kama anayerekebisha kitu fulani kikae vyema. Tulizoea kuona unapokwenda kwenye nyumba ya msiba, unaanza kusikia mtu akianza kupiga yowe la kilio hasa kuanzia nyumba ya tatu kabla ya kufika kwenye nyumba husika (sio wote, baadhi ya makabila).
Wengine wamegeuza misiba kama sehemu za kujipatia kipato kwa kuanzisha kamati kama za harusi. Tena kamati hizo hufanyikia kwenye baa. Wanakamati wakitoka hapo wamelewa chakari. Jamani waungwana tunaelekea wapi?
Pia sehemu za misiba zimegeuzwa kuwa za kuwachunguza na kuwateta watu. Utakuta mtu bila aibu anauliza, "hii ndo nyumba ya marehemu, Mh! Mbona mbaya hivi hata haifanani na jinsi alivyokuwa."
Au akiwa na nyumba nzuri "He! hii ndo nyumba ya marehemu? Lazima alikuwa anafanya ufisadi, haiwezekani awe na nyumba nzuri namna hii."
Ni mengi utasikia watu wakimteta marehemu, wengine utaona wanaonyeshana "unamuona yule! alikuwa demu wake, si una muona anavyolia." Jamani, wewe ina kuhusu nini? Hatukatazi kuiga wenzetu wanavyofanya, lakini visizidi mipaka. Unapokwenda kumfariji mfiwa huku ukiwa umejiremba kama unaenda harusini, huko ni kusanifu si kufariji.
CHANZO: NIPASHE
Nimesoma hii link na kubaki na mshangao jinsi misiba ya kisasa ilivyo. Je hivi ni sawa kweli? Au ndio mambo ya globalization hadi misibani.