Tunaenda Misibani kuomboleza au kutega watu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaenda Misibani kuomboleza au kutega watu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pretty, Jul 1, 2009.

 1. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Katika misingi ya mila na desturi zetu tulizojijengea toka enzi za mababu na mabibi zetu, linapotokea suala la msiba sehemu yoyote, watu hujikusanya sehemu husika wakiwa na huzuni kubwa kwa kuomboleza na kumfariji mfiwa.
  Msiba utaombolezwa nyumbani kwa mhusika na hapo mipango yote ya mazishi itafanywa na mambo mengine ya vyakula na vinywaji kwa ajili ya wafiwa na waombolezaji waliofika kujumuika nao.
  Michango itapitishwa kwa kuweka daftari kwenye sinia kwa ajili ya kumbukumbu za mahesabu au sahani na kila anayeingia kwenye nyumba ya msiba, huwajibika kuchukua daftari na kuandika jina lake kisha kuchangia kiasi anachoona kuwa kinafaa au alichojaliwa kuwa nacho kwa wakati huo ili kusaidia shughuli za msiba.
  Kwa upande wa akina mama ambao mara nyingi huwa na vyama vyao vya kuzikana, huwekeana viwango vya kuchangia hasa linapotokea suala muhimu la dharura kama hilo.
  Katika namna yoyote mara nyingi kwa wanawake, mavazi maalum yanayovaliwa katika mazingira kama hayo ni khanga. Wengi huvaa khanga mbili, moja akiwa amejifunga kiunoni na nyingine amejitanda kuanzia mabega huku baadhi yao wakijifunga kilemba kichwani.
  Kama pengine hakufanikiwa kuvaa khanga, basi atakuwa amefunga kitenge kiunoni na khanga atakuwa amejitupia kwa juu. Au kuna wengine wasiopenda kuvaa khanga wala vitenge, utakuta wamevaa nguo ndefu ambazo huja na mitandio yake (maarufu kama madira).
  Akina baba wao, hawana makuu katika mavazi mara nyingi ni suruali na shati, au kanzu na kofia juu na kwa wale wanaopenda kuvaa suti ni sawa tu.
  Siku za hivi karibuni hali hiyo imeanza kubadilika, sijui ni kutokana na mambo ya utandawazi,dunia kuonekana kama kijiji kimoja kikubwa, kutokana na kuaangalia kwenye luninga na kuona wenzetu wanavyovaa na baadhi yetu kujikuta wakitumbukia kuiga kila kitu bila ya kuchuja.
  Kwa baadhi ya misiba utaona jinsi akina dada wanavyovaa unashindwa kuamini kama kweli wameenda pale kwa ajili ya misiba au wamekosea njia walikuwa wanakwenda kwenye 'miradi' yao .Kwa mtu makini na mwenye akili timamu, ukiwatazama unabaki midomo wazi na kujiuliza huyu amekuja kwenye msiba au mawindoni ? Nafikiri anapopata habari ya msiba tu, kwanza huanzia salun kutengeneza nywele na kuukarabati uso katika namna ya kuvutia soko kinguvu.
  . Akitoka hapo anavyomeremeta utafikiri anaenda kwenye sherehe ya harusi. Ukija kwenye mavazi hapo ndo utachoka kabisa. Sawa kuna wengine huvaa suti Kuna baadhi unawashuhudia wakienda misibani kwa magari yao hadi makaburini, lakini kabla ya kushuka ili kujumuika na waombolezaji ili kukamilisha safari hiyo ya mwisho ya marehemu hapa duniani , anachukua poda, wanja na kuanza kujisiliba kiuhakika au magauni meusi, kofia na miwani mweusi ya jua lakini nguo hizo zinakuwa za heshima.
  Kuna baadhi utawakuta wamevaa suruali za kubana mwili halafu anachukua kimtandio chepesi na kukifunga kifundo kiunoni katika namna ya uchokozi, hapo unajiuliza huyu anaenda kumfariji mfiwa au anaenda kumsanifu? Au anakwenda kwenye msiba kujionyesha? Tena akipita sehemu ambayo akina baba wameketi, hata mwendo unabadilika na kuwa kama wa twiga katika hifadhi ya taifa anayatia majani ya nchani. Watu wanaofanya mambo hayo, huvizia misiba ya watu wenye maarufu au wenye majina makubwa , kwa sababu wanajua huko ndiko watu wengi wenye majina na hadhi zao hufika. Kwa kweli haipendezi.
  Hata staili ya kulia hubadilika, utamuona mtu ameshika leso yake na kujikanda kanda kwenye macho kama anayerekebisha kitu fulani kikae vyema. Tulizoea kuona unapokwenda kwenye nyumba ya msiba, unaanza kusikia mtu akianza kupiga yowe la kilio hasa kuanzia nyumba ya tatu kabla ya kufika kwenye nyumba husika (sio wote, baadhi ya makabila).
  Wengine wamegeuza misiba kama sehemu za kujipatia kipato kwa kuanzisha kamati kama za harusi. Tena kamati hizo hufanyikia kwenye baa. Wanakamati wakitoka hapo wamelewa chakari. Jamani waungwana tunaelekea wapi?
  Pia sehemu za misiba zimegeuzwa kuwa za kuwachunguza na kuwateta watu. Utakuta mtu bila aibu anauliza, "hii ndo nyumba ya marehemu, Mh! Mbona mbaya hivi hata haifanani na jinsi alivyokuwa."
  Au akiwa na nyumba nzuri "He! hii ndo nyumba ya marehemu? Lazima alikuwa anafanya ufisadi, haiwezekani awe na nyumba nzuri namna hii."
  Ni mengi utasikia watu wakimteta marehemu, wengine utaona wanaonyeshana "unamuona yule! alikuwa demu wake, si una muona anavyolia." Jamani, wewe ina kuhusu nini? Hatukatazi kuiga wenzetu wanavyofanya, lakini visizidi mipaka. Unapokwenda kumfariji mfiwa huku ukiwa umejiremba kama unaenda harusini, huko ni kusanifu si kufariji.

  CHANZO: NIPASHE  Nimesoma hii link na kubaki na mshangao jinsi misiba ya kisasa ilivyo. Je hivi ni sawa kweli? Au ndio mambo ya globalization hadi misibani.
   
 2. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tena siku hizi watu wanashona hadi sare za harusi,
  lakini nadhani ni watu kuiga utamaduni wa nchi za magharibi ambao siyo kila kitu kinatakiwa kuigwa, unapoenda kwenye msiba unatakiwa ujisitiri siyo unaenda kama kwenye maonyesho ya mavazi au mtu akuone, yani kuna misiba mingine ukienda hadi unasikia aibu, tena akifa mtu maarufu ndo balaa.
   
 3. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimeshashuhdia wengine huenda kuchunguza nani leo hajaja msibani au nani hajatoa mchango. Wanavyopepesa macho kuona mbona fulani leo hapa hayupo; utasikia hata ule msiba wa fulani na wa fulani hakutokea
   
 4. M

  Msindima JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mhh kwa kweli sijui tunaelekea wapi,nakumbuka siku moja kuna watu walipitia ofisini kwangu wakiwa wanelekea msibani nilichoka,kwanza walipofika nilifikiri wamekuja kunisalimia kumbe walipita hapo wanisalimie huku uelekeo ukiwa msibani,walipofika tu wakaniambia madam tumepita hapa tukusalimie tunaenda msibani,moyoni mwangu niliguna nikawauliza msiba wa nani mmoja akanijibu wa kaka yetu,nikajiuliza huyu aliefariki ni kaka yao kweli au ni danganya toto? na hili tatizo la kwenda kwenye misiba katika hizo hali za kujiremba na kujikwatua ziko sana kwetu wanawake,sijui hizi tabia kweli zimetokea wapi,hebu wanawake tujichunguze tuna matatizo gani,au wengine wanakuwa wako sokoni? TUJIULIZE JAMANI.
   
 5. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
   
 6. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Nimesoma hii link na kubaki na mshangao jinsi misiba ya kisasa ilivyo. Je hivi ni sawa kweli? Au ndio mambo ya globalization hadi misibani.[/QUOTE]

  Mhh! Pretty yaani sisi wanawake tunakoenda kubaya, ndo kusema competition zimekuwa kubwa mno kiasi hawataki kupoteza chance hata ya masaa mawili waendane na mazingira husika au? maana hata nyumba za ibada ni hivyo hivyo tena mbaya zaidi wengine ni Mrs sasa nini lakini kinaendelea: KUTOJIAMINI? KUTOJIHESHIMU? DHARUA ILIYOPITILIZA KIASI HANA CHA MJOMBA, WAKWE AU WATU WAZIMA WENGINE KUTOKANA NA MALEZI? KWAKWELI KAMA KUNA KITU TUNATAKIWA KUWAFUNZA BINTI ZETU NI HIZI TABIA - WAJARIBU KUJIHESHIMU WALAU KWENDA NA MAZINGIRA HUSIKA.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Watu wataiga style ya msiba wa MJ nyie subilini bongo hapa we acha tu mtaona ukoo mzima wanapiga suti nyeusi na miwani black maana akili zetu wabongo hazitutoshi.
   
 8. n

  niale25yahoocom New Member

  #8
  Jul 8, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni vizuri pia watu wakaweza kusoma alama za nyakati. Namaanisha kwamba kila sehemu inakuwa na mavazi ambayo yanaendana nayo. Otherwise utaonekana kituko sehemu ambayo hukutegemewa kuvalia hivyo...
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Wakifanya hivyo basi nitakubali kwamba kweli sisi manunda.
   
 10. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Mkuu Mungu akuwezeshe ubahatike ujionee viroja vya kina dada kuna baadhi ya hawa tunao waita maselebati wa kike hapa bongo wamekuwa na mtindo wa kuwafata kina Britini spear kutokuvaa chupi wakiwa katika vilabu vya starehe ,unamuangalia msichana na kuona nyama ile pale ,ni hatari kwa jamii na kizazi katika maisha yetu ya Kiafrica
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Lord of Mercy, wakibakwa.....?
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  kuwa uyaone!!!!!
   
 13. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  pole sana babylon, kwsa hiyo hayo mambo ya kutoka bila chupi mwishowe tutayaona misibani, si mambo ya kuiga kila kitu
   
Loading...