Hii nchi inamatatizo makubwa sana. Tukianza na bodi ya mikopo tu, kutotoa pesa kwa wanafunzi kwa wakati ni tatizo kubwa sana. Haya sasa hadi wanafunzi wa Uzamivu hali ni hiyohiyo. Poleni sana ndugu zetu, kwani hapo ni ngumu kuweka juhudi kwenye masomo wakati unadaiwa pango, mavazi na chakula.
Tusidanganyane watanzania, hii nchi inabidi kuikomboa kutoka kwenye fikra zilizopo ambazo hazitaki kubadilika. Elimu hakuna mtu anayeijali kabisa, aiwezekani mnapelekwa nchi za nje tena ulaya bila pesa za kutosha wakati inajulikana huko hakuna magumashi kama bongo.