Tunadhalilika PHD students tunaosoma Ujerumani kwa ufadhili wa Wizara ya Elimu

educator2025

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
386
438
sisi wanafunzi wa kitanzania tunaosoma vyuo vikuu mbali mbali hapa ujerumani masomo ya Shahada ya Uzamivu kwa ufadhili wa wizara ya elimu, tunadhalilika kutokana na mfadhili (wizara ya elimu, TZ) kutokutulipa pesa ya kujikimu kwa muda wa miezi 4 sasa.

Huku tunadaiwa kodi za nyumba pamoja na pesa za chakula. kila tukifuatilia wizarani tunapigwa kalenda. Tunaishi kwa taabu na kukopa kopa maana hapa ngumu kupata vibarua ukiwa mwanafunzi. kwa kweli hata wenye nyumba wametishia kutufukuza kwenye nyumba kwa kulimbikiza kodi muda mrefu inafikia hatua mtu unakosa nauli ya kutoka nyumbani kwenda chuoni. wizara ya elimu liangalien hili suala kwa jicho la 3
 
Dah!!!! kwanini hii serikali dhalimu inawatesa watanzania kiasi hiki? kama serikali haina pesa kwanini iwadanganye watanzania kwamba itagharamia masomo yao nchi za nje huku ikiwaacha miezi yote hiyo bila hata kuwapa pesa za kukidhi gharama zenu za maisha!? poleni sana.
 
Poleni sana wakuu, sa mnaishije? Akina dada zetu huko wanapona kweli kwa situation ka hiyo?

Ndio ccm hii bana
 
Wanawapa stress mpate phd pass bure, ila na nyie mkishakuja onesheni changes basi sio kutaka vyeo na heshima mtu huna peer viewed or published paper mwaka mzima. Mkija mje na impact, nawaomba tu
 
Nawashaurini mkirudi uzalendo wekeni pembeni,ikitokea chukua chako mapema....!!
 
Hii nchi inamatatizo makubwa sana. Tukianza na bodi ya mikopo tu, kutotoa pesa kwa wanafunzi kwa wakati ni tatizo kubwa sana. Haya sasa hadi wanafunzi wa Uzamivu hali ni hiyohiyo. Poleni sana ndugu zetu, kwani hapo ni ngumu kuweka juhudi kwenye masomo wakati unadaiwa pango, mavazi na chakula.

Tusidanganyane watanzania, hii nchi inabidi kuikomboa kutoka kwenye fikra zilizopo ambazo hazitaki kubadilika. Elimu hakuna mtu anayeijali kabisa, aiwezekani mnapelekwa nchi za nje tena ulaya bila pesa za kutosha wakati inajulikana huko hakuna magumashi kama bongo.
 
Poleni sana vijana.Najua ni namna gani inavyokera na inavyouma kwa kusoma bila ya pesa ktk nchi yenye high living cost km hiyo.
Huku viongozi wana lumbana kinafki ktk bajeti zao za kinafki zenye utekelezaji wa kinafki na wa kisiasa
 
Mkuu poleni sana!Na huku nyumbani hali ni mbaya zaidi wadogo zako walioko kwenye vyuo vikuu mbali mbali mpaka leo hawajapewa boom leo,wadada wanajiuza,wakaka wengi wako taabani hawajui wafanye nini huku baadhi ya wakiwa vibaka.Hii ni dalili kuwa huko hazina amna kitu.Poleni sana.
 
Hela zakuwalipa wabunge hata 600,000 kwa siku zipo !

Ila wanafunzi hazipo
serikali hii mamaee sana !
 
Ni aibu kwa serikali kuwaacha wanafunzi wa ndani na nje ya nchi wadhalilike. Kinana na timu yake ndo mambo ya msingi ya kuangalia hayo.
 
Kwa nini serikali inawatelekeza na kuzalilisha wasomi? Siyo vizuri japokuwa nyie na phd zenu hamleti tija yoyote hapa tz si ajabu mkabaki huko huko na phd zenu wakati mnasoma kwa kodi zetu
 
Mkuu poleni sana!Na huku nyumbani hali ni mbaya zaidi wadogo zako walioko kwenye vyuo vikuu mbali mbali mpaka leo hawajapewa boom leo,wadada wanajiuza,wakaka wengi wako taabani hawajui wafanye nini huku baadhi ya wakiwa vibaka.Hii ni dalili kuwa huko hazina amna kitu.Poleni sana.

Wanasema na wafanyakazi hawajalipwa mishahara hadi tarehe 3
 
sishangai wanafunzi wa hapa nyumbani hadi muda huu wengine hatujapewa pesa itakuwa nyi wa huko mbali! chezea ccm wewe
 
Hii ndo serikali ya CCM bwana. Hata huku ni hivyo hivyo, wamejenga shule lakini hazina waalimu na vifaa vya kufundishia na kufundishiwa.

Hospitali zipo tena nyingi tu hata kama ni za makanisa zilizo nyingi lakini madawa na vifaa hakuna, Madaktari wana hali ngumu na wameamua kukimbilia nchi za nje.

Barabara zinajengwa sana tu ila ubora ndo hivyo..... Kabla ya kukabidhiwa zinabomoka na hata zile zilizoanza kujengwa tayari zimesimama kwasababu ya ukosefu wa pesa ingawa fedha ya ujenzi ilikwishatengwa imepotea!!!

Vumilia tu Phd Student, yana mwisho!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom