MKWAMO: Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ijitafakarini haraka

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,281
2,423
Niende moja kwa moja kwenye mada husika ndugu wanajamvi.

Taifa lolote lazma liheshimu elimu inayotolewa nchini maana elimu ni msingi wa maendeleo ya Taifa au jamii husika. Tangu nchi hii tupate uhuru tumekua tukicheza sana hudhuma hii muhimu kwenye Taifa letu. Kila waziri anaepewa nafasi ya kuongoza wizara hii lazma aje na jambo au mambo yake yeye kama yeye nasio kama Taifa, utaratibu huu si sawa kabisa na inabidi tubadirike sana.

Siku za hivi juzi, wizara kupitia katibu wake DR.Mtahabwa amepigilia msumali kuhusu waraka wa huduma ya elimu kwa shule za msingi zenye utaratibu wa kulaza(boarding schools) watoto kua utaratibu huo umefutwa kwahiyo hakuna shule itakayo ruhusiwa kutoa huduma hiyo kwa madarasa ya la kwanza mpaka darasa la tano.

Nilimsikiliza vizuri na mpaka sababu alizo zitoa kuhusu kufungiwa hizo huduma. Moja ya sababu alizotaja ni kua watoto awapati malezi ya wazazi, watoto wanaonewa huko mabwenini, watoto wananyimwa haki zao na mwisho kua watoto hao wanafundishwa maadili mabaya.

Ni kweli mambo hayo yapo nkwenye baadhi ya taasisi au shule lakini sio kwa kiwango hicho na suluhu iliyototewa sio sawa ,sio tiiba ya tatizo nk. Wizara imejisahau kabisa kujua kua watanzania wengi wamewekeza pesa zao katika kutoa hiyo huduma ambayo niya msingi na faida kwenye Taifa letu.

Yaani wameipumguzia mzigo ata serikali. Je, wamiliki wa hizo shule watafanyia nini hayo majengo waliyo jenga ili kutoa huduma ya kulala wanafunzi? Je, wazazi ambao wamelipa pesa ya mwaka mzima kwenye hizo shule watarudishiwa pesa zao? Hapa serikali aioni imetengeneza mgogoro kati ya wazazi na wamiliki wa shule?

Lakini pia sijui kama serikali imefanya utafiti wa kina kuhusu ni watu wa namna au aina gani uwapeleka watoto wao kwenye shule za kulala. Kuna wazazi wanaishi mikoa tofauti ila makazi yao yapo mikoa tofauti. Kuna wazazi awakai na watoto wao kwa sababu ya kazi zao zilivyo. Je,wawe wanaambatana na watoto wao mkila wanapo kwenda kazini?

Kuna hoja kua kuna basi watoto wabaki na wasaidizi wa nyumbani. Hivi tukumbuke kua kuna watoto wengi walipata au wameisha pata matatizo waliyofanyiwa na hao wasaidizi, sasa leo mnataka wazazi turudi kule?

Shuleni ni sehemu salama sana kuliko ata huko nyumbani kuwaachia houseboy aned housegirl mtoto. Nimeshanga ata serikali aijui kua kuna familia yaaani baba na mama wote ni wafanyakazi na kila siku lazma waende kazini asubui na kurudi usiku. Hao watoto wakirudi kutoka shule wakae na nani kabla ya wazazi wao awajarudi? Je, serikali aioni kua pia ni kutengeneza tatizo kubwa tena.

USHAURI
1. Serikali iwatumie vizuri maafisa maendeleo ya jamii katika kutimiza wajibu wao asa kwa kutembelea mashule na kupata taarifa.

2. Waratibu wa elimu /shule ambao wapo katika kila ngazi mbali mbali kuanzia kijiji,mtaa, kata ,tarafa nk watimize wajibu wa wao maana wengi wao wamekua wakila tu kodi zetu nbi;la kutimiza wajibu wao.

3. Wathibiti ubora wa elimu pamoja na wakaguzi wa elimu na mashule pia watimize wajibu wao nasio kukaa tu maafosini na kupiga soga huku wakisuburi tu mishahara na posho.

4. Mwisho kabisa, iwe ni lazma kwasasa serikali iweke utaratibu wa wenye shule kuajiri watu wenye uzoefu na elimu ya malezi asa matrons na patrons maana shule nyingi aziwapi ajira watu hao. Kuna vijana wamesoma masomo ya malezi na makuzi, elimu ya awali ,maendeleo ya jamii lakini wapo mitaani.

Sasa iwe lazma kila shule kua na watu maalum wa kushughurikia malezi na makuzi y a watoto katika shule. Jambo ili tusilione dogo kisa sisi serikali hatuna shule za hivyo au tunao uwezo wa kua na familia popote pale tulipo.

Muije akibazi-Itahwa.
 
Familia zinazojitambua huwa hazipelekagi kabisa watoto bweni ni vile wabongo mnajifanya mna mambo mengi ya kufanya.


ASANTE.
 
Familia zinazojitambua huwa hazipelekagi kabisa watoto bweni ni vile wabongo mnajifanya mna mambo mengi ya kufanya.


ASANTE.
Karibu katika huu mjadala ndugu. Ukisema familia zinazo jitambua azipeleki watoto shule za bweni unakua unaleta taharuki maana shule za bweni sio kua ni shule za wajinga,
Hivi mimi ni dereva wa mabasi ya mikoani na mke ni mfanyakazi wa kiwandani ambako wa shift za mchana na usiku. Je, mmoja wetu aache kazi ili kukaa na watoto wakati kuna shule zenye huduma za bweni ili tuendelee kutafuta karo ?
Jambo ili linahitaji busara ya kuelewa uhalisia wa maisha ya watanzania.
 
Hili suala basically limefanyika kimihemko wizara haina budi kulipitia upya
Na mara zote watawala wetu wamekua wakifanya maamuzi kwa mihemko sana jambo ambalo ni hatari kwa afya ya Taifa letu.
 
Back
Top Bottom