Tunadhalilika PHD students tunaosoma Ujerumani kwa ufadhili wa Wizara ya Elimu

sisi wanafunzi wa kitanzania tunaosoma vyuo vikuu mbali mbali hapa ujerumani masomo ya Shahada ya Uzamivu kwa ufadhili wa wizara ya elimu, tunadhalilika kutokana na mfadhili (wizara ya elimu, TZ) kutokutulipa pesa ya kujikimu kwa muda wa miezi 4 sasa.

Huku tunadaiwa kodi za nyumba pamoja na pesa za chakula. kila tukifuatilia wizarani tunapigwa kalenda. Tunaishi kwa taabu na kukopa kopa maana hapa ngumu kupata vibarua ukiwa mwanafunzi. kwa kweli hata wenye nyumba wametishia kutufukuza kwenye nyumba kwa kulimbikiza kodi muda mrefu inafikia hatua mtu unakosa nauli ya kutoka nyumbani kwenda chuoni. wizara ya elimu liangalien hili suala kwa jicho la 3

tz tatizo kila konaaaaaa.. Na bado kuna we...hu wanaamini ktk low hasa na wapu...uz wa type hiyo.
 
daah yaani hela ya Scholarship ikipitia wizarani andika maumivu. Wakuu waziangalie tu zipite kuja huko kwenu kwani wao hawazitaki? Poleni sana wandugu jaribuni kubeba box na kusafisha vyoo vya umma mpate senti kadhaa mjikimu.
 
inahuzunisha sana kusikia wasomi wakilia lia kwa kukosa pesa za kujikimu natumaini hakuna dada zetu huko.
 
Sisi wenyewe Bodi ya mikopo ilipeleka mikopo yetu kwingine tofauti na chuo nilipo (loan allocation udsm admission Sua) mpaka Leo hiii nalala njaaa wamesababisha mpaka Jana nimegombana na mchumba wangu yuko shinyanga alinitumia laki moja nimnunulie cm na pia nimuongezeee kidogo baada ya kupata hiyo hela nimeila yote mpaka sasa tumekosana .
 
Back
Top Bottom