Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wameutwaa urithi wetu wakagawana;
Urithi huo waliogawana wamemegeana vipande vipande na kurithishana wao na watoto wao! Urithi wa taifa letu umekuwa wa kwao peke yao na sisi wengine tumeachiwa tugombanie nyumba iliyotupu ambacho hati miliki yake wao wanayo!
Mgongano unaondelea sasa kwa watu wenye maono madogo ni mgongano wa watu! Watu hao wanaona kinachoendelea sasa ni kati ya Mengi na Manji, Mengi na Rostam, Dr. Slaa na mafisadi, Mwakyembe na Rostam, n.k Wanayaona yanayoendelea kama mgongano kati ya mtu na mtu. Wenye maono haya wanaangalia nani atashinda; na wapo wanaoombea nani ashinde kwani kwa kushinda kwa mtu huyo kwao ni furaha.
Ukiwa unaangalia kutoka mbali utaona kuwa kinachogombaniwa ni urithi wetu. Mara ya kwanza tuliwanyang'anya watu urithi wa taifa letu tulipotangaza Azimio la Arusha. Tulitaka kuhakikisha kuwa wana na watoto wetu huko mbeleni watakuwa na nafasi sawa ya kumiliki na kufurahia utajiri wa nchi yao. Tulipotangaza Azimio lile tulisema kimsingi kuwa nchi hii ni yetu sote na wale watu ambao hawataki wengine wairithi hawa tunawanyang'anya.
Tukaimba wakati ule "mabepari walia, mabepari walia kukatiwa mirija". Tukajaribu kutoa nafasi sawa kwa kila Mtanzania kupata nafasi ya kunufaika badala ya kuacha utajiri wa nchi hii uwe mikononi mwa kikundi cha watu wachache huku mamilioni ya Watanzania wakiishi kama wahamiaji na wapangaji kwenye nchi yao.
Miaka 40 baadaye, waliokatiwa mirija wamerudi kwa nguvu zaidi; wameichomeka mirija yao siyo kwa Watanzania watu wazima tu bali hadi kwenye vichanga vinyonyavyo! Wanatufyonza kama nzi wa "kizungu" ambao wanamereta kwa rangi ya kijani lakini furaha yao iko katika kufyonza uchafu! Mirija yao ya sasa imeunganishwa na kutengeneza pingiri za unyonyaji!
Wanatunyonya kwenye madini, wanatunyonya kwenye fedha, wanatunyonya kwenye elimu na wanatunyonya bila huruma. Ili kuhakikisha hatusikii maumivu ya mijira yao wanatupiga ganzi ya misaada ya kigeni. Bila misaada ya kigeni tungesikia maumivu ya unyonyaji wao. Hili wanalijua.
Hivyo kila kukicha hukika bakuli zao toka kwa mabwana zao ili wamwagiwe ganzi ya misaada ya kigeni. Tukilala wao wanakuja na kutufyonza mpaka karribu tone la mwisho, tukiamka tunajikuta tumenenepa tena na hatusikii maumivu; kumbe walipotunyonya na kuondoka wakarudi na kutujaza misaada ya kigeni! Wenyewe tunawaona wananenepa na kufura kwa utajiri wetu!
Sasa asitokee mtu kuwahoji au kuwapigia kelele; Asitokee mtu awanyonyesheee kidole; Asitokee mtu kuwaambia mbona mnatunyonya? Mtu huyo atakuwa adui na atashukiwa kama na mwewe wa Tanga na kama kuvamiwa na kundi la nyuki atafukuzwa. Kwa sababu amewahoji.
Sisi wengine tuna uamuzi wa kufanya; aidha tukubali yaishe kuwa nchi hii ni ya kwao na tukae pembeni kuangalia nani kati ya "watu" hawa atashinda au kusimama na kusema yule mwenye kutetea urithi wetu yuko upande wetu. Na huyo naye hatuna mkataba naye wa milele kwani yuko upande wetu kwa kadiri ya kwamba anatetea urithi wetu.
Ndugu zangu tunachogombania siyo Benki Kuu, tunachogombania siyo madini, tunachogombania siyo umiliki wa makampuni au kupata kura. Tunachogombania ni Tanzania gani tunataka kuwarithisha watoto wetu na watoto wa watoto wetu. Tunachogombania ni nchi gani tunataka waikute.
Je, tuwarithishe watoto wetu nchi inayotawaliwa kifisadi?
Je, tuwarithishe watoto wetu Benki Kuu ambayo wizi mkubwa umefanyika na unafanyika?
Je, tuwarithishe watoto wetu nchi inayoongozwa na chama kilicholewa ugimbi wa madaraka na kinakwenda kwa kuyumbayumba kama Pombe Sikali?
Je, tuwarithishe watoto wetu Bunge la wabunge waliogawanyika kwa mujibu wa maslahi ya matumbo yao wakitunga sheria za kuuchilia urithi huo kwa bei ya chee?
Je, tuwarithishe watoto wetu mchakato mbovu wa uchaguzi unaochangia kuwachagua wale wale waliotunyonya?
Je, tuwarithishe watoto wetu mfumo mbovu wa elimu ambapo kwa kadiri unavyokwenda juu ndivyo kupasi kunavyoshuka? Angalia wanaopasi kwenye Mtihani wa Bodi ya Wahasibu na mitihani mingine!
Je, tuwaritishe watoto wetu nchi ambayo madini yake yamewekwa chini ya makampuni ya kigeni kama Barrick na kutaka kubadilisha mikataba hiyo inatubidi tuwabembeleze wao?
Je, tuwarithishe nchi yenye viongozi wasiothubutu kutenda lakini wakiwa mahiri wa maneno na mikwara?
Mimi nasema hapana! Ninasema inatosha. Tutawarithisha watoto wetu taifa tulitakalo, taifa lenye nafasi sawa kwa wote na lenye kutawala kwa misingi ya sheria (siyo maneno ya sheria). Tutawarithisha watoto wetu taifa ambalo ndani yake hakuna bwana na mtwana; taifa ambalo Mtanzania mmoja hamnyonyi mwingine kwa sababu tu ya umaskini wake!
Wanaofurahia mgongano wa watu hawa, waendelee kufurahia; lakini tukumbuke kuwa tunachogombania ni kikubwa kuliko Mengi, ni kikubwa kuliko Manji, ni kikubwa kuliko Rostam ni kikubwa kuliko Jeetu Patel na kwa hakika ni kikubwa kuliko Kikwete na wapambe wake! Tunachogombania ni urithi wetu.
Na huo hatuwaachii watu wachache watugawie. Hivyo basi: Tumedhamiria yafuatayo: