Tunachofikiri ndio tunachozalisha

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Tunachofikiri ndio tunachozalisha. Sisi ni zao la akili na mawazo yetu wenyewe. Aina ya taifa letu ni zao la mawazo yetu wenyewe liwe zuri au baya. Taifa hili tutalijenga kwa akili zetu wenyewe. Inategemea tuna busara na hekima kiasi gani. Tutalijenga taifa hili kulingana na akili zetu na tutalibomoa hivyo hivyo kulingana na akili zetu ni za kipuuzi kwa kiwango gani. Hakuna kinachokuja kwa bahati mbaya. Majaliwa ya binadamu yanatokana na matendo yake mwenyewe.

Umaskini wetu kama taifa hakuna mtu wa kumlaumu. Uwezo wa kuondoa umaskini huu uko chini ya nguvu zetu.

Kama tu wadhaifu sana kuuondoa au tumekosa maarifa ya kufanya hivyo au utashi wa kuuondoa hilo ni juu yetu pia.

Lakini nguvu ya kuuondoa tunayo lakini imelala au inatumika katika mambo yasiyo na manufaa.

Au pengine sababu ya migawanyiko yetu. Au kwa kutenda au kutokutenda kwetu na kwa tabia na aina ya fikra tulizonazo. Na pengine kukosa nidhamu na dira ya pamoja na muelekeo ili tupeleke nguvu zetu huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well mkuu,.kuna msemo pia usemao "You Are What You Think"...ni dhahiri kuwa vile tulivyo kama Taifa ni matokeo ya fikara zetu ambazo hizo huja kujidhihirisha kwenye matendo/utendaji(matokeo) wetu,.sasa ni either tunafikiri vyema lakini tujue kuna mamlaka husika za kiutedaji katika Taifa ambazo zinaweza kubadili jema kuwa baya and vice versa na pengine hazitaki iwe hivyo kwa maslahi binafsi au ni uwezo wetu tuu wa kupambanua mambo kwa viwango vya juu kama wanataifa ni mdogo kiasi kupelekea mazuri kuwa machache kuliko mabaya"
 
Ni sisi kwa umoja wetu kwakuwa hao viongozi wanatoka kwetu. Tuna wakuza katika jamii zetu, mitaa yetu na vijiji vyetu, mifumo yetu ya elimu na kisha huwachagua kwa kutumia akili zetu.

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Basi tusubiri kizazi hiki kipite,.maana kama ni kubadii mfumo itakuwa ni mfumo ujao na si huu wa sasa,.tuanze kuimarisha misingi ikomae kwelikweli Ili nyumba itakayojengwa juu yake ikawe imara..
 
Basi tusubiri kizazi hiki kipite,.maana kama ni kubadii mfumo itakuwa ni mfumo ujao na si huu wa sasa,.tuanze kuimarisha misingi ikomae kwelikweli Ili nyumba itakayojengwa juu yake ikawe imara..

Tunaweza kufanya kitu sasa hivi ili kuunda jamii iliyopo kama tukishindwa sisi sasa hivi nani ataweza lazima kuwepo na starting point. Kama tunataka kufanya kitu lazima tuanze sasa. Hiko kizazi kijacho hakiwezi kujitengeneza chenyewe .....
 
Back
Top Bottom