888I
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 462
- 576
Mei 3, ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Habari...
Katika ulimwengu unaozidi kujazwa na taarifa bila kikomo, ambapo mitandao ya kijamii inachochea hofu, chuki na migawanyiko kwa kasi, na akili bandia (AI) inazalisha maudhui kwa sekunde chache, tunahitaji zaidi ya hapo awali waandishi wa habari huru na wanaotegemewa.
Tunahitaji waandishi ambao si wafuasi wa hadithi zinazopendwa na watu au wanasiasa, bali wanaotoa ukweli kutoka kwenye taarifa nyiingi zilizopo. Ukweli unaohusu afya zetu, elimu yetu, maisha yetu ya kila siku, utendaji wa serikali zetu, fursa za ajira, mwelekeo wa siasa, na hali halisi ya uchumi wetu.
Kwa sababu siku moja, taarifa zitatosha. Watu wataacha kutafuta “likes” na “shares”, na badala yake watataka ukweli... ukweli unaoweza kuwaokoa, kuwaelimisha, na kuwawezesha kufanya maamuzi bora kuhusu maisha yao na mustakabali wa taifa lao.
Sekta huru ya uandishi wa habari ni nguzo muhimu ya demokrasia, haki ya binadamu, na maendeleo ya pamoja. Ni kinga dhidi ya upotoshaji, propaganda na udanganyifu wa kisasa.
Katika Tanzania na duniani kwa ujumla, wakati huu ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote.. tuwe walinzi wa ukweli, si wafuasi wa kelele.
Ukweli una nguvu. Na ukweli unahitaji uhuru.
#worldpressfreedomday #uhuruwahabari #journalismmatters #pressfreedom #habarihuru