Tunaangamia..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaangamia..!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by eRRy, Feb 25, 2010.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,083
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]


  Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa kitabibu, baadhi ya kuku wa kufugwa wanaoingia sokoni wamekuzwa kwa kutumia ‘utundu’ wenye hatari wa baadhi ya wafugaji wasio waaminifu kwa kulisha mifugo hiyo dawa za ARV ambazo huwafanya kuku hao kuonekana wakubwa na wanene kwa muda mfupi.

  Uchunguzi huo unakwenda mbele zaidi na kubainisha kwamba, tabia za dawa hizo ambazo ni kujenga mwili na kuimarisha kinga ya magonjwa kwa mwathirika wa Virusi vya Ukimwi, ndiyo inayompata mlaji wa kuku hao.

  Inadaiwa kuwa, kuku hao wanapokula chakula kilichochanganywa na dawa hizo, huweza kutumia siku kumi na mbili hadi kumi na nne kutoka kuwa vifaranga hadi utayari wa kuingizwa kwenye soko la walaji.

  Ili kukamilisha uchunguzi huo, Amani lilituma machero wake maeneo ya Kibamba, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo ndipo kwenye viwanda vya kuzalisha kuku wa ‘sampuli’ hiyo.

  Kwa mujibu wa kijana mmoja ‘profesheno’ wa kutunza kuku katika moja ya nyumba maarufu kwa uzalishaji maeneo hayo, ambaye hakutaka jina lake lichorwe kwenye ‘pepa’ hii, alikiri kuwepo kwa ishu hiyo, lakini alibainisha kuwa hajui bosi wake anapochukulia vidonge hivyo vya ARV’S.

  MADHARA:
  Kwa mujibu wa Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbi ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, mtu anayependa kula kuku waliokuzwa kwa kutumia ARV na yeye huanza kunenepa kupita kawaida, lakini uzito unaweza kuwa tofauti na unene ‘boya’.

  Mtabibu huyo aliongeza kuwa, watoto wengi wanaozaliwa siku hizo ambao wazazi wao wamekuwa watumiaji wazuri wa kuku, hukua haraka kiasi kwamba, mtoto wa miaka 18 huonekana kama ana miaka 27.

  Aidha, alidai kuwa, wengi ambao kuku hao wamekuwa chakula chao kikuu, hufika mahali wanakuwa ‘legelege’ katika utendaji wa kazi wa kila siku tofauti na zamani huku sehemu kubwa ya chakula hicho ikiangamiza ‘pati’ ya subira na uvumilivu na mlaji kuwa na hasira.

  Dalili nyingine ni mtu kuhisi muda wake wa kuchoka unakuwa mfupi akilinganisha na zamani na wakati mwingine hali ya kuhisi kusinzia humtawala hata kama anafanya kazi.
   
 2. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,083
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ???????????????????????/
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Acheni vyepe mayai!
   
 4. K

  Konaball JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 2,123
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  naona poa si wanatupa kinga kabisa kwa hizo ARVs
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  ndo hali halisi ya maisha tunayoishi sasa vitu vingi vinatuangamiza
  hewa zenye Silica kama kawa ..mabadiliko ya hali ya hewa ,karibia kila kitu ni hazard
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Tumekwisha!
   
 7. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Usanii kutoka china. kila kitu fasta fasta
   
 8. bona

  bona JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,794
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  lets try as much as possible to stay natural, food stuff zote tununue masokoni uswahilini sio supermarket, kama una ham ya kuku jipinde ukanunue wa kienyeji! you will be safe, at least for now!
   
 9. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Drugs have half lives (t half) and can be denatured by various factors.
  It's not a good practice for sure. But as far as being affected by eating ARV treated chicken, nothing to fear
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,210
  Likes Received: 769
  Trophy Points: 280
  heri yangu nilae kuku wa kienyeji.hawa ni wazuri sana
   
 11. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180

  Yea raha ya kuku wa kienyeji unatafuna mpka mfupa tih tih
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...