VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Hata kama ni wapinzani wetu,mazuri yao tutayachukua.Ima kwa kuwaomba au kuyafanya tu na wao wagutuke baadaye. Kwenye chaguzi za CHADEMA zinazoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City, CHADEMA inatufunza mambo mbalimbali ya kidemokrasia. Wametulia;wamejipanga na wanapendeza. Kuanzia maandalizi ya nje ya ukumbi;ukumbini na luningani. Na hata fulana na kofia zao. Tutajifunza kwa maboresho yetu.
Kuanzia Baraza la Wazee; BAVICHA na leo hii BAWACHA,CHADEMA wamejipanga na wakapangika. Intelijensia huru imeshindwa kuona mikutano mbalimbali ya kificho nje ya Ukumbi rasmi inayolenga kupanga takrima au mshikemshike wa hapa na pale. Mbabe wa sera na sura huonekana Ukumbini (Ukumbi rasmi wa mikutano). Kambi za wagombea mbalimbali huishia mlangoni ili kuwapa wasio na kambi muda wa kutafakari sera na sura za wagombea wao.
Hadi kufikia leo, hakuna hata mgombea aliyekimbilia kwa waandishi wa habari kulalamikia ukiukwaji wa sheria na kanuni za kichama. Kila mmoja anamuamini aliyeshinda na kuapa kupambana naye kwa hoja uchaguzi ujao. Mipango ya CHADEMA isitutishe wapinzani wao ila itufunze. Tukubali kuchukua angalau utulivu na umeremetaji wa ukumbi na wanaukumbi katika vyama vyetu. CCM yangu isibaki tena nyuma. Ichote mema ya CHADEMA.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam