Tumwamini Nani? Hayati Magufuli au Polepole?

Tumwamini Nani? Hayati Magufuli au Polepole?

Sahihi kabisa
Tumuamini polepole, pale magufuli alikua akiongea kisiasa, ni wazi na ukweli usio kuwa na shaka magufuli hakuwa chaguo la kikwete.

Hata mimi ningeongea kama magufuli mbele ya kikwete ila hata kikwete alijua ndio maana akawa anacheka kiasi kile.
 
Wote wa kupuuza. Utawala Fulani ukiwa mtamu kwako unakaa kimya hata mabaya Gani yafanyike lakini utawala mwingine ukiwa mchungu kwako unatoka shimoni kupinga.
1. Waliikumbatia hihiii katiba na Wala hawakutaka kabisa kusikia katiba mpya na wakasema hadharani kabisa hawana mpango wa mchakato wa katiba mpya. Watanzania hawali katiba Bali wanahitaji maendeleo. Kama huyo polepole na Magufuli walikuwa na dhamira ya kweli kwanini hawakuendeleza ule mchakato wa katiba ya warioba?
2. Kama ni watu kupotea haya yote haya kuanzia Kwa mama Bali ni kipindi yeye akiwa mwenezi, miaka yote mitano mbona hakusema lolote?
3. Walimuondoa CAG Asadi unconstitutional Kwa sababu yapo aliyoyaweka wazi kuhusu utawala wao, mbona alikaa kimya?
4. Bunge lilijadiliwa gizani mbona hakuyaongea?
5. Upinzani ulipigwa marufuku hata kukaa meza moja kula chakula mbona hakujiuzulu?
6.Hata hizo wanazosema Magufuli alichukua fomu na kuomba nafasi hawamu ya pili tofauti na wanavyomsema mama ni kutuona sisi mazumbukuku tu. Hv mnafikiri mama naye angeamua kupitia huo mchakato na power aliyonayo kikatiba na akaamua kweli kubaki kuna ambaye angemzuia.
7. Njoo kwenye uchaguzi wa wabunge, wapo waliokuwa nafasi ya nne kwenye kura za maoni ndani ya CCM na wakachukuliwa kuwawakilisha wananchi, hiyo ndio ilikuwa demokrasia?

NB: Atueleze ya Tundu lisu, Beni saa nane na wengineo maana yeye anasema haiwezekani kwamba polisi hawajui watekaji Kwa hawamu hii. Mbona enzi zao na power waliyopewa hawakuwajua watekaji? anaishia kuongelea kibiti tu. Kibiti walishughulika nayo Kwa sababu walioguswa zaidi walikuwa polisi na sio raia wa kawaida zaidi.
Polepole apunguze unafiki wake watu wanaakili na uzuri siku hizi ipo mitandao ya kijamii zipo kumbukumbu
 
Back
Top Bottom