Serikali irudi nyuma na kuangalia maamzi yake ambayo yameiweka nchi katika hali tete. Kupiga marufuku sukari ya nje, kufungia matangazo ya bunge, kuongeza VAT kwa mizigo ya nchi jirani inayopita bandari ya Dar na kubwa zaidi kufungia vyama vya siasa kufanya mikutano. Haya ni mambo yameifanya nchi kuyumba na kuwa ktk hali amvayo hatujaizoea. Pamoja na kelele zote serikali wameziba masikio kama hawaioni hali hii!
Tukiwa kwenye mtanzuko huo serikali inaleta mswaada ambao utatuingiza kwenye sintofahamu nyingine. Fao la kujitoa limepingwa na kila mtumishi na siyo leo, vyama vya wafanyakazi vyote vimepinga wazi wazi serikali haisikii. Sasa watumishi wametishia kugoma, bado hatusikii! Ndiyo maana nikasema tusipepese macho, tuwaambie wakubwa wanaivuruga nchi yetu!