Tumuunge mkono Lukuvi kwa hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumuunge mkono Lukuvi kwa hili

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280


  Na Mhariri

  [​IMG]
  Maoni ya katuni  Juzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitangaza kukamatwa kwa Mkuu wa kitengo cha Ardhi katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, pamoja na kusimamishwa kwa maofisa wengine saba wa idara hiyo, pia kufungwa wa ofisi hiyo kutokana na tuhuma za kughushi nyaraka na kuuza maeneo mawili ya wazi yaliyopo katika rasi ya Msasani.
  Agizo la kuchukuliwa kwa hatua hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kupata taarifa za kuwepo udanganyifu wa kuuza viwanja vya wazi, huku akiagiza uchunguzi zaidi wa kina ufanywe kubaini wahusika wengine wa vitendo hivyo ambavyo vimevuruga sana taratibu za mipango miji na kuleta migongano ndani ya jamii.
  Hii ni mara ya kwanza kwa hatua kali na za haraka kuchukuliwa na kiongozi wa serikali hasa katika Jiji la Dar es Salaam juu ya kero kubwa ya uvamizi wa viwanja vya wazi, kughushi nyaraka na pia kusababisha wenye haki ya kutumia maeneo ya wazi kubaki wakitafuta maeneo ya kupumzika na kucheza kwa sababu maeneo yao yameuzwa kinyemela.
  Tunajua kwamba Mkuu wa Mkoa aliamua kwenda mwenyewe kwenye ofisini hizo na kushuhudia mikakati ikipangwa kukamilisha kazi ya kugawa viwanja hivyo kwa raia wanaoshirikiana na watumishi wa umma kupindisha sheria kwa sababu ya vishawishi mbalimbali.
  Katika uvamizi huo, imeelezwa kwamba nyaraka mbalimbali zilikamatwa zikiwemo barua zilizosainiwa na viongozi waandamizi waliowahi kuongoza Manispaa hiyo.
  Tungependa kuchukua fursa hii kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam; kwanza, kwa ujasiri wa kuthubutu kufanya alichofanya, lakini la pili ambalo ni muhimu kuamua kupambana na kero ambayo kwa hakika imekuwa sugu kwa miaka na miaka.
  Itakumbukwa kwamba mara baada ya kuchaguliwa kwa Waziri John Magufuli, kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mwanzoni mwa utawala wa Awamu ya Nne, alitangaza Manispaa ya Kinondoni kuwa moja ya maeneo ambayo yamekithiri nchini katika kuvuruga taratibu na kanuni za ugawaji ardhi.
  Waziri huyo alitangaza kupambana na tatizo hilo, lakini kwa habati mbaya sana, hakudumu muda mrefu katika wizara hiyo, hivyo tangu aendolewe baadhi ya maofisa waliokuwa wametopea katika uvunjaji wa kanuni za kugawa ardhi, wakarejea kwenye utamaduni wao.
  Ni bahati ya mtende kwamba sasa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amaeona mambo ya ovyo yanayofanywa na watendaji hawa wa serikali ambao wanawajibika kuhakikisha kwamba kanuni na sheria za matumizi bora ya ardhi zinafuatwa, lakini zaidi sana wakiwa ndio vinara wa kuhakikisha kwamba taratibu za mipango miji zinafuatwa vilivyo.
  Tatizo la uvamizi wa maeneo ya wazi katika miji mingi nchini ni kubwa; kwa mkoa wa Dar es Salaam ni tatizo kubwa mno; kwa wastani maeneo mengi ya wazi yameuzwa na yanaendelea kuuzwa kiasi cha kuufanya mji huo kuwa kama unaendeshwa bila kuwepo kwa mpango kabambe wa uendelezaji.
  Ni Manispaa hii hii ambayo hivi karibuni ilikuwa imeamua kugawa eneo la ufukwe wa Coco kwa watu binafsi kuendesha, kama si kuingilia kati kwa viongozi wa juu serikalini, leo hii Coco Beach ingekuwa ni ufukwe wa mtu binafsi. Aibu tupu!
  Kumekuwa na kesi nyingi mno za kugawa kiwanja kimoja kwa zaidi ya mtu mmoja; wapo walioshitakiana mahakamani, lakini wapo walioingia katika ugomvi mkubwa; huku wengine wakiingizwa kwenye hasara kubwa. Hawa ni wale wanaojikuta wamekwisha kutumia rasilimali zao nyingi kuendeleza viwanja vyao lakini baadaye kuja kugundua kwamba vilikuwa na mgogoro kwa kuwa viligawanywa kwa zaidi ya mtu mmoja.
  Ni bahati njema kwamba baada ya maofisa hawa kuendelea na tabia ya kutokujali maadili ya kazi yao, kujitengenezea mazingira ya kujinufaisha binafsi na ofisi za umma, sasa ameibuka kiongozi mwingine anawamulika na kuwachukulia hatua stahili ili kurejesha misingi ya uwajibikaji katika Idara ya Ardhi ya Manispaa ya Kinondoni.
  Ni katika misingi hii tunamuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ujasiri wa kuthubutu kuutafuna mfupa ambao umewashinda wengi, na kwa kweli kufanikiwa kuusaga kwa nguvu inayostahili. Sote tumuunge mkono kiongozi huyu.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mimi Pia namuunga Mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kazi yake anayoifanya ila azidi kufanya kweli tuone mafanikio yake.
   
 3. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hongera Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa. Na yale maeneo ambayo hayajawahi kupitishwa greda wala kufanyiwa usafi, jee hawa Manispaa wafanywe nini?
   
 4. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ni sawa, lakini tukumbuke kuwa radi ikipiga na kutwama katika dimbwi la maji, basi yeyote atakayepita
  humo halali yake, huu ni wakati wa kampeni za chini kwa chini basi mnyonge hugeuzwa ngazi
  ya kujitangaza

  ina bidi hao wahusika waulizwe wameiga kwa nani hiyo tabia ya kughushi nyalaka usije kuwa
  ndiyo ule msemo wa ''jinsi baba alivyo ndivyo watoto walivyo'' waingereza wanasema '' like father like son'' heheeeee mahoka!!
   
 5. T

  Tall JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.hongera sana lukuvi,

  2.kumbuka kabla afisa ardhi hajatoa hati ni lazima town planer nae aruhusu....au nae sign yake ilighushiwa?

  3.yapo maeneo mengi ya wazi yaliyokwishavamiwa akitaka awaombe wananchi wanajua kila kitu.

  4.kuna wakati jamaa ilibaki kidogo tu wajenge pale kwenye viwanja vya mnazi mmoja.

  5. Mfano mimi leo nikiwa na pesa zangu nikapenda kujenga katikati ya makaburi ya kinondoni,afisa ardhi baada ya kumuweka sawa ananipa hati. Hapo mimi na afisa wote si wakosaji?

  6.ni mawazo yangu kuwa hawa nao waliojenga sehemu za wazi ni wakosefu,tena ndio mzizi wa kosa,mheshimiwa ukikamata maafisa peke yake patachipua tena mimea mingine.umeacha mizizi....kama mfano afisa alikuwa anafoji kwa jina la tall,kwa nini tall nae asihusike?....mtoa na mpokea rushwa wote ni wakosaji.

  7.ni mawazo yangu pia kuwa yeyote aliejenga pasipostahili abomoe mwenyewe,kama ni fidia akamwombe aliempa hati.

  8.leo hii kuna petrol station ambazo hata kuwasha mkaa nyumbani kwako unaogopa.zipo katikati ya makazi ya watu.nadhani hadi mtaa mzima uje uungue ndipo tutashituka.mbona master plan ya jiji ipo inaonyesha kila kitu???????
   
 6. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  hongera sana lukuvi.

  ardhi kinondoni pameoza kwa rushwa.
  jamaa ni wachafu kupindukia.

  pale mahali haki ya wanyonge inapindwa
  na kunyang'anywa utafikiri hakuna serikali!
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  SAKATA LA UUZAJI WA VIWANJA VYA WAZI KINONDONI-KAZI BADO
  Kwa mara nyingine tunashuhudia tukio lililoamsha hasira za umma wa Watanzania kuhusu utendaji usioridhisha wa watendaji wa serikali. Mheshimiwa Lukuvi mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kagundua kuwa maafisa wa ardhi wilaya ya Kinondoni wameuza kiwanja cha wazi kwa mwekezaji kinyemela na hivyo kuwanyima wananchi hususani watoto huduma muhimu. Mheshimiwa kahamaki kweli kweli-hili jambo limemuudhi mno, na safari hii anaonyesha makali ya makucha yake kwa kuagiza hatua za kinidhamu papo kwa papo. Anasema watumishi wote wa idara ya ardhi wilaya ya Kinondoni wahamishiwe sehemu nyingine kuanzia kesho ili wapishe uchunguzi wa polisi. Hapa natoa pongezi kwa mkuu huyu kujiunga katika “kilio” cha wananchi cha muda mrefu kuhusu hujuma zinazofanywa na watendaji wake katika kutoa huduma kwa umma.
  Hata hivyo wakati tunasubiri kuona matokeo ya hatua za mkuu huyu, ni vyema wananchi tukawa na subira ya kushangilia mafanikio ya muda mrefu. Hii si mara ya kwanza kusikia matamko haya makali hususani kwa watendaji wa manispaa ya Kinondoni. Sina nia ya kubeza agizo la mkuu huyu, lakini lakini histioria husaidia watu kutafakari-kumbukumbu za sakata la matukio ya watendaji wa hospitali za Mwananyamala na Amana bado mbichi. Tumeambiwa watendaji waliobainika kuharibu kazi wamehamishiwa sehemu nyingine, lakini sina uhakika kama hii imesaidia kuboresha huduma kwa wananchi. Nasikia wataalam waliohamishiwa Mwananyamala hawajaripoti wote! Hofu yangu na watanzania wengi ni kuhusu dhamira ya viongozi wa serikali kushughulikia udhaifu wa utendaji ndani ya taasisi zake. Tunaamini kuwa njia zinazotumika kushughulikai matatizo haya zimekumbwa na usugu kama choroquine ilivyoshindwa kutibu malaria-yaani KUUNDA TUME NA KUHAMISHA WATUHUMIWA.
  Hebu nirejee kwenye masuala ya ardhi Kinondoni na kwingineko katika miji yetu. Hivi ni kiongozi gani asiyejua kuwepo kwa matatizo ya ardhi hususani kuvamiwa au kuuzwa kwa viwanja vya wazi na kufungwa kwa barabara zinaunganisha mitaa? Mimi huwa napata faraja kuwa kuna vipindi serikali inakuwa sikivu na kuchukua hatua……zimeundwa tume na kamati lukuki kushughulikia matatizo ya ardhi na sehemu kubwa ya migogoro imetatuliwa na hata baadhi ya watendaji kuchukuliwa hatua! Lakini moja ya hatua zilizowatia wananchi moyo ni lile agizo la Raisi wa awamu ya nne, Mheshimiwa Jakaya Kikwete la kuunda kamati za kuchunguza matatizo ya ardhi kila wilaya kama sehemu ya kutekeleza ahadi yake ya kumaliza migogoro ya ardhi. Bila shaka kamati ya Kinondoni pia ilifanya kazi yake vizuri na kubaini matatizo ya viwanja vya wazi na barabara zilizofungwa makusudi. Kinachotushangaza ni kuwa takribani miaka minne ya uundaji wa kamati hizi, ule moto wa kushughulikia matatizo yaliyobainika umepotea-hadi mkuu wa mkoa atembelee sehemu! Kulikoni? Hivi kuna dhamira ya kumsaidia Raisi kutekeleza ahadi zake kweli?
  Mwisho naomba kutoa rai kwa Mheshimiwa Lukuvi. Tumekusikia na tunakutakia kila heri ufanikishe utekelezaji wa agizo hili. Hata hivyo kuna haja ya kuwa makini katika kuchagua dawa ya kumaliza ugonjwa huu, tusije kuwa tunahangaika na kupunguza maumivu ya dalili za ugonjwa wakati chanzo hakijaguswa.
  [FONT=&quot]Kwanza, sote tunajua kuwa ugawaji wa matumizi ya ardhi si kazi ya mtu mmoja, na hasa ikigusa matumzi ya umma! Ndiyo maana nadhani kuwahamisha watumishi wote wa ardhi siyo suluhu, na pengine hatua [/FONT]

  Chanzo Japhet Makongo
  Mtaa wa Bwawani-Makumbusho (0754 571256)
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  hii haitawatendea haki wale watumishi wachache wazuri-tunajua wapo. Katika hatua hii ya kwanza ungewasimamisha watendaji wakuu wasimamizi wa manispaa…Mkurugenzi, maafisa wasimamizi wa vitengo vya ardhi na kamati za ardhi za manispaa. Hatua ya pili ungewashauri viongozi wa kuchaguliwa-meya na madiwani husika wajiwajibishe kwani hii ni kashfa katika sifa za uongozi bora. Tuige tamaduni nzuri za wenzetu nchi za nje kazi zao zinapokumbwa na kashfa, hata kama haziwagusi moja kwa moja. Hii itatuongezea imani kuwa tunaviongozi wanaojali maslahi ya watu an siyo ya viongozi-muda wa kulindana umekwisha na hasa katika kipindi hiki.
  Pili, kama mzee Lukuvi umeamua kutumia ziara kama sehemu ya kutatua matizo ya wananchi, hebu jikumbushe yaliyomo katika taarifa ya kamati zilizoundwa kushughulikia matatizo ya ardhi (2006/7) ikusaidie kutambua sehemu za kutembelea…endelea na manispaa ya kinondoni tu…njoo mwananyamala, makumbusho, kijitonyama kwa kuanzia….utayaona ya firauni. Na katika ziara zako, chukua jambo moja tu…..kuhakiki matumizi ya viwanja vya wazi na barabara/mitaa iliyofungwa. Maana yangu ni kuwa usiunde tena kamati nyingine na kutumia askari kuchunghuza mambo yaliyo wazi.
  Tatu, hebu serikali ifikie mahali ifanye kazi yake kikatiba. Tunasikia kuwa serikali inasita kurudisha baadhi ya sehemu zilizovamiwa au kuuzwa kwa kuhofia kulipa fidia au kufikishwa mahakami! Tunamwomba Mheshimiwa Raisi atumie mamlaka yake kisheria….. anaweza ku-revoke maamuzi ya nyuma ya matumzi ya ardhi kwa faida ya umma." Ni aibu kwa nchi kukosa sehemu za mapumziko zilizoko kwenye mpango miji eti kwa saabau zimemilikishwa kihalali (kiharamu) kwa watu wanaouza pombe, maegesho ya magari, gereji bubu, makanisa/misikiti, vituo vya mafuta na ujenzi binafsi…… jamani tuwe makini hii si sawa.
  Mzee Lukuvi, ukiyazingatia haya utakuwa umeshirikia kivitendo katika kumkumbuka "Mtoto wa Afrika" kwenye sherehe tuliyomaliza juzi badala ya hotuba zinazorudsia yale yale. Ni matumaini yangu kuwa utayasoma haya na kutafakari.

  Chanzo Japhet Makongo http://groups.google.com/group/wanabidii/browse_thread/thread/b5406e7b7c5df833?hl=sw
  Mtaa wa Bwawani-Makumbusho (0754 571256)
   
 9. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Its about time!!
   
 10. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ameen hukuyajua hayo kwa sababu ya akili zako, bali kwa kuwa yule roho wa ufahamu toka kwa Mungu alikutumia ili uyajue
  saaaaaaaaaafi MziziMkavu maana imeandikiwa kila ulimi utakili habari zake na ya kuwa yeye ni Bwana
   
Loading...