Tumuombee Rais au tumhurumie?

Tumuombee Rais au tumhurumie?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
677
TUMUOMBEE RAIS AU TUMHURUMIE?

Na Elius Ndabila
0768239284

Juzi Mh Rais akiwa mkoani Kagera alitoa maagizo kwa mkoa wa Dar es salaam juu ya video iliyokuwa mitandaoni ikionyesha moja ya shule iliyopo Ubungo wanafunzi wake wakisomea nje na kukaa chini. Akizungumza kwa uchungu mkubwa Mh Rais aliwaagiza viongozi wa Manispaa ya Ubungo na RC wa Mkoa kushughulikia tatizo hilo haraka.

Baada ya kauli ya Mh Rais, yametolewa maelekezo ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kwenye moja ya Chombo cha habari ambacho kinajulikana kwa jina la NJOMBE PRESS TV. Mkurugenzi huyo amesema "Awali ya yote niyapokea maelekezo ya Mh r Rais, Sisi tangu tulipoona hiyo clip hatukukaa kimya kila mtu alishangaa kwa sababu ni taarifa ambazo hazikuwahi kufika ofisini kwangu":- Beatrice Dominic Mkurugenzi wa Manisipaa ya Ubungo.

Anasema kila mtu alishangaa kwa kuwa hizo taarifa hazikuwa kufika ofisini. Wakati Mkurugenzi anazungumza hayo mimi nimeifikiria kuwa yaani Mkurugenzi anashangaa! Yaani taarifa hazijafika ofisini? Hivi gari za Wakurugenzi zina kazi gani? Mkurugenzi anataka taarifa zifike ofisini? Nani amfikishie ofisini? Wilaya ya Ubungo kwa ukubwa wake ni ndogo kuliko kata yetu ya Ibaba Wilayani Ileje. Ni Wilaya ambayo Mkurugenzi anaweza kutembelea shule zake zote za msingi na sekondari kwa masaa matatu akamaliza Wilaya nzima. Lakini nimejiuliza Kama Mkurugenzi wa Ubungo, wilaya yenye kila aina ya rasilimali, wilaya ndogo kiasi hiki hawezi kujua changamoto za wilaya yake hadi yeye na wenzake wote WANASHANGAA! Vipi Wilaya ambazo ni kubwa kuliko mkoa wa Dar es salaam wote, Wilaya ambazo hazina rasilimali kama za Ubungo, ambazo tu hata barabara kwa msimu huu wa mvua hali ikoje? Ninazungumza Wilaya kama Namtumbo, Kalambo, Newala, Kiteto, Matela, Makete, Ileje, Chunya n.k huko hali ikoje? Hali ni mbaya. Dar es salaam ndo sura ya nchi kuko hivi, vipi huko kwenu?

Hali hii umenifanya nifikirie kazi ya kumuombea Rais iendelee, lakini wasio weza kuomba waendelee kumhurumia kwani baadhi ya Wasaidizi wake hawamsaidii bali wanamuongeza stress. Badala ya Mh Rais kupambana na ujenzi wa Taifa kwa kushughulikia mambo makubwa, lakini wakati mwingi amekuwa anapambana na mambo ambayo yangesimamiwa na hata mtendaji wa mtaa. Kutokana na uzembe mkubwa wa baadhi ya watu ambao Mh Rais aliwaamini kushindwa kuendana na kasi yake ndiyo maana mara kadhaa tumemuona Mh Rais anafanya kazi za VEO, WEO, DEO, DMO, DED, DC n.k

Watanzania wangejua ni channel ipi Mh Rais anafuatilia na wangeamua kutuma kila mtu clip ya matatizo hasa kwa upande wa Elimu tu kwa kila mtu sehemu alipo Mh Rais angeshaa kuwa hii ni Tanzania au ni Malawi? Mh Rais ukitaka kujua haya undaa kikosi independent cha watu hata 50 kwa nchi nzima ili wazunguke huko mitaani kama mazingira ya baadhi ya shule yanafanana na Tanzania mpya. Yapo maeneo ambayo hali ni mbaya kuliko hata Ubungo, lakini sidhani kama unajua. Zipo Wilaya zenye miti lakini utakuta watoto wanakaa chini.

Kuna tetesi nimesikia baada ya kauli yako ya juzi kuna baadhi ya maeneo toka jana viongozi hawajalala. Hawa unajiuliza wakisubiri Rais atoe tamko? Wao kazi zao ni zipi?

Kila mtu achague upande wake, Kumuombea au kumhurumia kwa kuwa na watu ambao si msaada kwake?
 
Kama kuna JANGA kubwa nchi hi basi ni wafanyakazi na watendaji wengi wa serikalini; hawana ubunifu, ni business as usual always; wanacho jali wao ni kwenda na kurudi kazini, hawajali sana matokeo ya kwenda kwao kazini mara kwa mara; nitafafanua.

1. Mwezi December mara baada ya kutoka matokeo ya darasa la saba, tulimsikia waziri mkuu pamoja na waziri wa TAMISEMI kaka Suleman Jafo wakiwaelekeza wakurugenzi kuhakikisha yanajengwa madarasa ya sekondari haraka kabla ya mwezi March; nina hakika hilo litafanyika, cause waziri mkuu na waziri wa TAMISEMI wanajua rasilimali za kutekeleza hilo zipo, but swali ni hili, huko wilayani na tarafani kuna waratibu na maafisa elimu, wapo pia ma DED, kazi mojawapo kwa watu wa elimu ni kujua maendeleo ya elimu katika eneo lao la utawala, wanatembea shule, wanakagua maendeleo ya kielimu shuleni na of course wanakagua hata ufundishaji wa walimu kwa watoto wetu, wao ndio wana ratibu hata mitihani ya MOCK na wanaratibu hadi matokeo na usahihishaji wa mitihani hiyo, na report zinaandikwa, kama kweli hayo yote yanafanyika then inakuaje wanashindwa ku predict ufaulu wa watoto kwenda sekondari and hence maandalizi ya vyumba vya darasa la 9 kufanyika mapema? Kweli hao ma DED ambao wengine ni pHD holders, wanasubiri hadi PM aseme? Wao wenyewe hawana intiatives hata kidogo? Kwanini tuwalipe mshahara???? SOmetimes mhe akiwa anatumbua watu, tunweza kumuona kama ni katiri sana but watendaji wengi wanaboa sana.

2. Jana nimeiona clip fulani ya mama Gwajima, waziri wa afya akiwa Mwanza nadhani, yaani baada ya kufunga mfumo sijui wa kukusanya fedha, mapato yamepanda kwa zaidi ya 400% How, nilishangaa sana, so zile pesa tulizokua tunalipishwa hospitals before mfumo hazikua zinafika sehemu husika? Halafu tunashangaa MSD kuzidai halmshauri nyingi pesa nyingi na sisi tunapeleka lawama serikalini, kumbe pesa zinakusanywa na zinapelekwa KIBRA, kweli?

Wakati fulani niliwahi kuuliza sehemu nani hasa shareholders wa Azania bank; nilikuja kugundua ni mashirika giant ya hifadhi ya jamii. NSSF na PPF kabla haijaunganishwa ni hizo zingine, kufanya vizuri kwa bank ya Azania ndio mafanikio ya NSSF na PPF, but gues what? Hayo mashirika hayana account kwenye bank wanayoimiliki wao wenyewe; hivi bado tunaweza kusema sasa hivi mashirika yetu hayafanyi vuziri kwasababu ya utaalamu kweli? Bongo hatuna tatizo hata moja la elimu, tunashida ya watu kukariri. Nakumbuka kabla ya ujio wa mhe No 1, kile kiwanda kinacho tengeneza Transformer za umeme sijui ni Tanareck; TBS inazitambua transofrmer za kiwanda kile kwa ubora, Tanesco ni shareholder wa hicho kiwanda, again gues what, Taneseco hawakua wateja wa transformer wa kiwanda kile. Swali la kijinga ni hili, hivi umeme Tanzania umekua monopolized na Tanesco, unategemea nani anunua bodhaa unazo zitengeneza kama wewe mwenyewe huziamini? HAlafu MD wa Tanesco ni PHD holder, mwenyekiti wa body nae ni msomi tu mwenye vyeti vyake. Tuna tatizo kubwa sana, elimu haijatusaidia kiviile sana.
 
Mimi siwezi kumuombea rais kwa sababu,
(1) hayo mambo ameyataka mwenyewe kwa ubaguzi wa kiitikadi na uswahiba
(2) Mazuzu ya uvccm ndio anayapa hizo kazi kwa kuangalia nani anamshangilia na kumsifia,
(3)alitamka waziwazi kwamba hawezi kumteua mtoto wa jirani wakati wa kwake wapo,(UVCCM hata kama hawana uwezo wa kufanya kazi)
Ndio hao sasa wanamuonyesha uwezo wao duni wa kiutendaji,hawawezi kwenda field kazi yao ni kukaa ofisini na kusikilizia posho tu

Maendeleo yana vyama
 
Mimi namuombea tu kwa Mwenyezi Mungu amrehemu dhambi zake zote alizowafanyia/anazoendelea kuwafanyia Wafanyakazi wa Nchi hii ya Kusadikika.

Haiwezekani Mfanyakazi aliyeajiriwa mwaka 2014 alingane mshahara/ daraja na yule aliyeajiriwa 2020! Huu ni uonevu usio vumilika. Hali hii inapunguza sana morali ya kufanya kazi.
 
Huyo mkurugenzi ni muongo.
PM aliwaambia wasiende likizo mpaka wakamilishe ujenzi wa madarasa.Sasa yeye alikuwa wapi kama si kwenye huo ujenzi?She must be knowing.
 
Haya ni matokeo ya kufyatua watoto . Alisema watu wazaliane yye atasomesha.
Asomeshe sasa
 
TUMUOMBEE RAIS AU TUMHURUMIE?

Na Elius Ndabila
0768239284

Juzi Mh Rais akiwa mkoani Kagera alitoa maagizo kwa mkoa wa Dar es salaam juu ya video iliyokuwa mitandaoni ikionyesha moja ya shule iliyopo Ubungo wanafunzi wake wakisomea nje na kukaa chini. Akizungumza kwa uchungu mkubwa Mh Rais aliwaagiza viongozi wa Manispaa ya Ubungo na RC wa Mkoa kushughulikia tatizo hilo haraka.

Baada ya kauli ya Mh Rais, yametolewa maelekezo ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kwenye moja ya Chombo cha habari ambacho kinajulikana kwa jina la NJOMBE PRESS TV. Mkurugenzi huyo amesema "Awali ya yote niyapokea maelekezo ya Mh r Rais, Sisi tangu tulipoona hiyo clip hatukukaa kimya kila mtu alishangaa kwa sababu ni taarifa ambazo hazikuwahi kufika ofisini kwangu":- Beatrice Dominic Mkurugenzi wa Manisipaa ya Ubungo.

Anasema kila mtu alishangaa kwa kuwa hizo taarifa hazikuwa kufika ofisini. Wakati Mkurugenzi anazungumza hayo mimi nimeifikiria kuwa yaani Mkurugenzi anashangaa! Yaani taarifa hazijafika ofisini? Hivi gari za Wakurugenzi zina kazi gani? Mkurugenzi anataka taarifa zifike ofisini? Nani amfikishie ofisini? Wilaya ya Ubungo kwa ukubwa wake ni ndogo kuliko kata yetu ya Ibaba Wilayani Ileje. Ni Wilaya ambayo Mkurugenzi anaweza kutembelea shule zake zote za msingi na sekondari kwa masaa matatu akamaliza Wilaya nzima. Lakini nimejiuliza Kama Mkurugenzi wa Ubungo, wilaya yenye kila aina ya rasilimali, wilaya ndogo kiasi hiki hawezi kujua changamoto za wilaya yake hadi yeye na wenzake wote WANASHANGAA! Vipi Wilaya ambazo ni kubwa kuliko mkoa wa Dar es salaam wote, Wilaya ambazo hazina rasilimali kama za Ubungo, ambazo tu hata barabara kwa msimu huu wa mvua hali ikoje? Ninazungumza Wilaya kama Namtumbo, Kalambo, Newala, Kiteto, Matela, Makete, Ileje, Chunya n.k huko hali ikoje? Hali ni mbaya. Dar es salaam ndo sura ya nchi kuko hivi, vipi huko kwenu?

Hali hii umenifanya nifikirie kazi ya kumuombea Rais iendelee, lakini wasio weza kuomba waendelee kumhurumia kwani baadhi ya Wasaidizi wake hawamsaidii bali wanamuongeza stress. Badala ya Mh Rais kupambana na ujenzi wa Taifa kwa kushughulikia mambo makubwa, lakini wakati mwingi amekuwa anapambana na mambo ambayo yangesimamiwa na hata mtendaji wa mtaa. Kutokana na uzembe mkubwa wa baadhi ya watu ambao Mh Rais aliwaamini kushindwa kuendana na kasi yake ndiyo maana mara kadhaa tumemuona Mh Rais anafanya kazi za VEO, WEO, DEO, DMO, DED, DC n.k

Watanzania wangejua ni channel ipi Mh Rais anafuatilia na wangeamua kutuma kila mtu clip ya matatizo hasa kwa upande wa Elimu tu kwa kila mtu sehemu alipo Mh Rais angeshaa kuwa hii ni Tanzania au ni Malawi? Mh Rais ukitaka kujua haya undaa kikosi independent cha watu hata 50 kwa nchi nzima ili wazunguke huko mitaani kama mazingira ya baadhi ya shule yanafanana na Tanzania mpya. Yapo maeneo ambayo hali ni mbaya kuliko hata Ubungo, lakini sidhani kama unajua. Zipo Wilaya zenye miti lakini utakuta watoto wanakaa chini.

Kuna tetesi nimesikia baada ya kauli yako ya juzi kuna baadhi ya maeneo toka jana viongozi hawajalala. Hawa unajiuliza wakisubiri Rais atoe tamko? Wao kazi zao ni zipi?

Kila mtu achague upande wake, Kumuombea au kumhurumia kwa kuwa na watu ambao si msaada kwake?
acha unafiki ww kabla ya kumuombea jiulize hospitali ya chato kwa ukubwa wake af Waziri analalamika wagonjwa wachache swali je kwann isingeboreshwa zaidi bugando kuokoa kanda ya ziwa jibu ni sanaa zinaendelea
 
Anapaswa kuondolewa madarakani haraka sana.
 
Kama kuna JANGA kubwa nchi hi basi ni wafanyakazi na watendaji wengi wa serikalini; hawana ubunifu, ni business as usual always; wanacho jali wao ni kwenda na kurudi kazini, hawajali sana matokeo ya kwenda kwao kazini mara kwa mara; nitafafanua.
1. Mwezi December mara baada ya kutoka matokeo ya darasa la saba, tulimsikia waziri mkuu pamoja na waziri wa TAMISEMI kaka Suleman Jafo wakiwaelekeza wakurugenzi kuhakikisha yanajengwa madarasa ya sekondari haraka kabla ya mwezi March; nina hakika hilo litafanyika, cause waziri mkuu na waziri wa TAMISEMI wanajua rasilimali za kutekeleza hilo zipo, but swali ni hili, huko wilayani na tarafani kuna waratibu na maafisa elimu, wapo pia ma DED, kazi mojawapo kwa watu wa elimu ni kujua maendeleo ya elimu katika eneo lao la utawala, wanatembea shule, wanakagua maendeleo ya kielimu shuleni na of course wanakagua hata ufundishaji wa walimu kwa watoto wetu, wao ndio wana ratibu hata mitihani ya MOCK na wanaratibu hadi matokeo na usahihishaji wa mitihani hiyo, na report zinaandikwa, kama kweli hayo yote yanafanyika then inakuaje wanashindwa ku predict ufaulu wa watoto kwenda sekondari and hence maandalizi ya vyumba vya darasa la 9 kufanyika mapema? Kweli hao ma DED ambao wengine ni pHD holders, wanasubiri hadi PM aseme? Wao wenyewe hawana intiatives hata kidogo? Kwanini tuwalipe mshahara???? SOmetimes mhe akiwa anatumbua watu, tunweza kumuona kama ni katiri sana but watendaji wengi wanaboa sana.
2. Jana nimeiona clip fulani ya mama Gwajima, waziri wa afya akiwa Mwanza nadhani, yaani baada ya kufunga mfumo sijui wa kukusanya fedha, mapato yamepanda kwa zaidi ya 400% How, nilishangaa sana, so zile pesa tulizokua tunalipishwa hospitals before mfumo hazikua zinafika sehemu husika? Halafu tunashangaa MSD kuzidai halmshauri nyingi pesa nyingi na sisi tunapeleka lawama serikalini, kumbe pesa zinakusanywa na zinapelekwa KIBRA, kweli?

Wakati fulani niliwahi kuuliza sehemu nani hasa shareholders wa Azania bank; nilikuja kugundua ni mashirika giant ya hifadhi ya jamii. NSSF na PPF kabla haijaunganishwa ni hizo zingine, kufanya vizuri kwa bank ya Azania ndio mafanikio ya NSSF na PPF, but gues what? Hayo mashirika hayana account kwenye bank wanayoimiliki wao wenyewe; hivi bado tunaweza kusema sasa hivi mashirika yetu hayafanyi vuziri kwasababu ya utaalamu kweli? Bongo hatuna tatizo hata moja la elimu, tunashida ya watu kukariri. Nakumbuka kabla ya ujio wa mhe No 1, kile kiwanda kinacho tengeneza Transformer za umeme sijui ni Tanareck; TBS inazitambua transofrmer za kiwanda kile kwa ubora, Tanesco ni shareholder wa hicho kiwanda, again gues what, Taneseco hawakua wateja wa transformer wa kiwanda kile. Swali la kijinga ni hili, hivi umeme Tanzania umekua monopolized na Tanesco, unategemea nani anunua bodhaa unazo zitengeneza kama wewe mwenyewe huziamini? HAlafu MD wa Tanesco ni PHD holder, mwenyekiti wa body nae ni msomi tu mwenye vyeti vyake. Tuna tatizo kubwa sana, elimu haijatusaidia kiviile sana.
agiza unachokunywa mkuu nipo njiani nakuja tudiscuss soln la hili tatizo ingawa shida akili za wasomi wengi zpo kwny uteuzi
 
Watendaji wengi hapa Tanzania ni bure kabisa!

Wao wanawaza kuchapana bakora tu.
Huwa ninacheka sana zile sifa Za kijinga zisizoendana na uhalisia, eti kuwa rais karejesha nidhamu na utendaji serikalini. Pita kwenye taasisi za serikali utakuta mambo ni yaleyale. Tuna mifumo dhaifu, na sababu hasa ya mifumo kutokubadilishwa ni ili kulinda watawala dhaifu. Huu mchezo wa kumfanya rais ndio muamuzi wa kila kitu utatugharimu miaka yote.
 
Mkumbuke kuwaombea madaktari na walimu pia
 
Tuwahurumie kina Tundu Lissu, kina Mdude, familia ya Mawazo nk ambao wamekua wahanga wa majanga
 
Huwa ninacheka sana zile sifa Za kijinga zisizoendana na uhalisia, eti kuwa rais karejesha nidhamu na utendaji serikalini. Pita kwenye taasisi za serikali utakuta mambo ni yaleyale. Tuna mifumo dhaifu, na sababu hasa ya mifumo kutokubadilishwa ni ili kulinda watawala dhaifu. Huu mchezo wa kumfanya rais ndio muamuzi wa kila kitu utatugharimu miaka yote.
Tena wale wenye ukaribu na rais kwa namna yeyote ile wanajiona wako juu ya sheria, wao ni kila kitu. Yeye anafanya kosa na wananchi wakilalamika anaanza “mnanijua mimi ni nani”.
 
Kama kuna JANGA kubwa nchi hi basi ni wafanyakazi na watendaji wengi wa serikalini; hawana ubunifu, ni business as usual always; wanacho jali wao ni kwenda na kurudi kazini, hawajali sana matokeo ya kwenda kwao kazini mara kwa mara; nitafafanua.
1. Mwezi December mara baada ya kutoka matokeo ya darasa la saba, tulimsikia waziri mkuu pamoja na waziri wa TAMISEMI kaka Suleman Jafo wakiwaelekeza wakurugenzi kuhakikisha yanajengwa madarasa ya sekondari haraka kabla ya mwezi March; nina hakika hilo litafanyika, cause waziri mkuu na waziri wa TAMISEMI wanajua rasilimali za kutekeleza hilo zipo, but swali ni hili, huko wilayani na tarafani kuna waratibu na maafisa elimu, wapo pia ma DED, kazi mojawapo kwa watu wa elimu ni kujua maendeleo ya elimu katika eneo lao la utawala, wanatembea shule, wanakagua maendeleo ya kielimu shuleni na of course wanakagua hata ufundishaji wa walimu kwa watoto wetu, wao ndio wana ratibu hata mitihani ya MOCK na wanaratibu hadi matokeo na usahihishaji wa mitihani hiyo, na report zinaandikwa, kama kweli hayo yote yanafanyika then inakuaje wanashindwa ku predict ufaulu wa watoto kwenda sekondari and hence maandalizi ya vyumba vya darasa la 9 kufanyika mapema? Kweli hao ma DED ambao wengine ni pHD holders, wanasubiri hadi PM aseme? Wao wenyewe hawana intiatives hata kidogo? Kwanini tuwalipe mshahara???? SOmetimes mhe akiwa anatumbua watu, tunweza kumuona kama ni katiri sana but watendaji wengi wanaboa sana.
2. Jana nimeiona clip fulani ya mama Gwajima, waziri wa afya akiwa Mwanza nadhani, yaani baada ya kufunga mfumo sijui wa kukusanya fedha, mapato yamepanda kwa zaidi ya 400% How, nilishangaa sana, so zile pesa tulizokua tunalipishwa hospitals before mfumo hazikua zinafika sehemu husika? Halafu tunashangaa MSD kuzidai halmshauri nyingi pesa nyingi na sisi tunapeleka lawama serikalini, kumbe pesa zinakusanywa na zinapelekwa KIBRA, kweli?

Wakati fulani niliwahi kuuliza sehemu nani hasa shareholders wa Azania bank; nilikuja kugundua ni mashirika giant ya hifadhi ya jamii. NSSF na PPF kabla haijaunganishwa ni hizo zingine, kufanya vizuri kwa bank ya Azania ndio mafanikio ya NSSF na PPF, but gues what? Hayo mashirika hayana account kwenye bank wanayoimiliki wao wenyewe; hivi bado tunaweza kusema sasa hivi mashirika yetu hayafanyi vuziri kwasababu ya utaalamu kweli? Bongo hatuna tatizo hata moja la elimu, tunashida ya watu kukariri. Nakumbuka kabla ya ujio wa mhe No 1, kile kiwanda kinacho tengeneza Transformer za umeme sijui ni Tanareck; TBS inazitambua transofrmer za kiwanda kile kwa ubora, Tanesco ni shareholder wa hicho kiwanda, again gues what, Taneseco hawakua wateja wa transformer wa kiwanda kile. Swali la kijinga ni hili, hivi umeme Tanzania umekua monopolized na Tanesco, unategemea nani anunua bodhaa unazo zitengeneza kama wewe mwenyewe huziamini? HAlafu MD wa Tanesco ni PHD holder, mwenyekiti wa body nae ni msomi tu mwenye vyeti vyake. Tuna tatizo kubwa sana, elimu haijatusaidia kiviile sana.
Na ukijaribu kuwashauri kosa, utasingiziwa makosa mpaka utajuta na ukoo wako. Viongozi wengi wa taasisi, mashirika na kurugenzi wanapenda siasa kuliko performance...
 
Hivi swala la watoto kuingia darasa la kwanza Januari ni emergence kweli?

Hii inahitajika iwe planned for na itashangaza sana kwenye nchi ambayo tunadai hakuna ajira eti madawati hayako, madarasa hayajajengwa na bado hatuoni kwamba hizo ndizo ajira zenyewe...
 
Back
Top Bottom