Tumuombee Mhe. Lissu au Rais Magufuli

Tumuombee Mhe. Lissu au Rais Magufuli

MIMH NAMWOMBEA LISSU NA ANASTAHLI KWA SABABU AMEWASAIDIA WANANCH WENG WANYONGE..

KUPAZA SAUTI KWA NIABA YA WANYONGE

KUWATETEA WANYONGE MAHAKAMAN BILA MALIPO

KUISHAURI SERIKALI KUHUSU MIKATABA YA RASILIMALI ZA NCHI.

LISU SYO MNAFIK HATA MUNGU ANAJUA NA NDIYO MANA MUNGU AMEMLINDA NA RISAS 38 ZA KIVITA.
 
Mkuu mbona mwisho hapo hujasema kuwa hii ' taarifa / habari ' yote umeitoa ( yaani umeikopi na kupesti ) kutoka katika toleo la hivi majuzi tu la Gazeti lililokula ' mvua / kifungo ' leo la MWANAHALISI? Na safari hii wameweza kweli kwani mmpigwa ' pini ' kote kote katika Kuchapisha na hadi Online.

Tutaheshimiana tu Kudadadeki!
Unafurahia gazeti kufungiwa?
 
Mimi nilishasema, Lilisu bora linge....tu. Hahahaaaa, nimeogopa
Malizia tu mkuu bora lingekufa!!! , unafikiri Mungu ni kama wewe, ndg unajua mwisho wako kweli, unajua maisha aliyokupangia Mungu kweli, aisee una kiburi cha maisha hata zaidi ya Firauni na Nebukardineza. Kaka unaweza kusema kwa ujasiri bora binadamu mwenzako angefariki??? Dah Mungu akusamehe ila jua hufaja hujaumbika na duniani tunapita.
 
CC: MODS: Hili ni chapisho lenye maneno ya kebehi kwa mkuu ws nchi, ni chapisho lililoandikwa kwenye gazeti la mwanahalisi lililopelekea gazeti hilo kufungiwa. Sidhani kams ni busara lihamishiwe kwenye Jukwaa hili ambalo limejijengea heshima yake.
Kama wamelifungia kwaajili ya chapisho hili, basi serikali imekosa kazi. Katika article hii kuna jambo lililonenwa ambalo ni baya. Kwa hiyo watu wanazuiwa kusikia maoni ya watu wengine ili waendelee kulishwa ujinga?
 
Mie kama Mtanzania hata kwa fimbo hatopata hata sala yangu moja.JPM aombewe na akina Bashite na Mkewe
Kama mtu umekosa wa kumwombea, ni afadhali kumwombea hata shetani ili ikiwezekana siku moja abadilike na kurudia nafasi yake ya kale.
 
Kwanza mwenyewe tukajistukia. Unamsikia siku izi akiomba kuombewa? Ukishajiingiza kwenye njia ovu kama zake huna ujasili tena wa kutegemea Mungu. Mtu anachukia CCM wengine kutembelea wasio chama chake. Huyu ni mkristo fake walahi tena. Moyoni mwake uovu umetamalaki. By the way mtu aniambie ame achieve nini mpaka sasa zaidi kuleta taharuki inchini
 
Nipoteze muda wangu kuombea Pogba?

Hata kwa lazima siwezi
 
Tundu Lissu alipoanza kusisitiza mara kwa mara kwamba mambo mengi yanayofanywa na Rais John Magufuli ni ya kukurupuka, na yataleta hasara kubwa kwa taifa, rais na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa yeyote anayempinga rais ni msaliti.

Hata majuzi, katika moja ya hotuba zake mubashara za hivi majuzi, Rais Magufuli alisema:

*“Nilipokuwa nikizungumza, ndugu zangu, kwamba hii ni vita ya uchumi, na vita ya uchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida.*

*“Vita ya kawaida, adui unamuona. Na saa nyingine msaliti anapowasiliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari wanajua kazi yao huwa wanafanya nini.*

*“Huwezi kuwa msaliti halafu ukawa… uka-survive (ukanusurika, yaani ukaachwa uishi).”*

Kwa Rais Magufuli na baadhi ya wapambe wake, Lissu ni msaliti, si mzalendo.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, wiki kadhaa zilizopita, kuna mtu alithubutu kumshambulia Lissu kwa maneno hayo makali, akisema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki si mzalendo.

Lissu hakusubiri mtu huyo ajibiwe na watu wengine. Alijibu mwenyewe akisema:

Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii. Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya (ya madini) tangu mwaka 1999.

Wakati huo, tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu – Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa CCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi bila kudai malipo Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, na kadhalika.

Sijui wewe ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani – alikuwa upande wa CCM na wanyonyaji hawa.

Soma gazeti la Rai la tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini (Rais Benjamin) Mkapa siku alipokwenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa anatetea “tumbo lake” na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya (kutetea wananchi wa) Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi, ila najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo, na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana naye. Ni muongo.

Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata kwa siku chache tu. Zingatia maneno yangu. Ataumbuka, na (nyie mnaomtetea) mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Mimi si mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga (makinikia) atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo, hana pa kwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati atakapokuwa anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa hohe hahe kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa fedha nyingi ya fidia na mahakama za usuluhishi za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya, basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. (Abdulkarim) Mruma haitamaliza hata nusu saa, iwapo itachunguzwa kwa kina.

Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina msingi wowote wa kuaminika. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka 1999, utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy, na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu.

Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni ujinga, hata kama ni wa kiprofesa. Hatuibiwi kwenye mchanga.

Huo ni ujinga unaoweza kukubaliwa tu na watu mbumbumbu. Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, basi, Mungu na atusamehe!

Kama serikali inasaini mikataba mibovu, na Lissu anapiga kelele kwamba mikataba hii ni mibovu na itaingiza taifa katika hasara, msaliti ni yeye anayesema au maofisa wa serikali waliosaini mikataba hiyo?

Msaliti ni yeye au rais anayetaka kumnyamazisha ili nchi isisikie sauti yake ya kinabii?

Kama viongozi wetu wamevunja mikataba; uamuzi wa viongozi wetu ukasababisha tushitakiwe, tukashindwa katika mahakama za usuluhishi; msaliti ni Lissu anayesema tumeshitakiwa na tumeshindwa?

Kama tunadaiwa na makampuni ya nje, yakakamata ndege yetu, Lissu akasema ndege yetu imekamatwa kwa sababu ya uamuzi mbovu wa viongozi wetu, na akasema watakaolipa fedha hizo si viongozi bali ni wananchi maskini; msaliti ni yeye au hao waliosababisha madhira hayo?

Kama rais anatoa amri zinazopoka uhuru wa wananchi kufikiri, kujieleza na kukusanyika – kinyume cha katiba – na Lissu anajitokeza kusema huu ni udikteta uchwara; inatosha kumuita msaliti?

Na katika mazingira ya “ugomvi” tunaoshuhudia mfululizo kati ya serikali na Lissu, na kwa kuzingatia matamko mabaya ya viongozi wakuu wa serikali dhidi yake; na sasa amepigwa risasi mchana kweupe, tutarajie nani awe mtuhumiwa wa kwanza dhidi ya Lissu?

Nimesikia kauli tata za viongozi wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Wanazungumza kisiasa na kwa jeuri isiyotarajiwa, kubeza wananchi wanaohoji unyama aliofanyiwa Lissu.

Kwa hili la Lissu, serikali na wapambe wake watatunga propaganda za kutoa watu mstarini, lakini tayari naona Mungu amewakatalia.

Rais Magufuli, katika hotuba zake kadhaa, amekuwa anataka tumuombee. Sasa, kwa matukio haya, taifa limetambua kuwa anayestahili kuombea ni Tundu Lissu.
Ansbert Ngurumo - Jina lake la NGURUMO linashabihiana na KELELE KALI anazopiga. Hakika amelitendea haki jina lake. Heko Ngurumo kwa kuendelea kuunguruma hata kutoka huko uliko, katika gazeti la Raia Mwema. Wewe ni SHAHIDI wa kiwango cha juu sana sawa tu na SHAHIDI mwingine TUNDU ANTIPAS MUGHWAI LISSU. Mungu akubariki sana wewe mwenyewe, na ailinde Familia yako. Wewe na Lissu ndio mnastahili KUOMBEWA, pamoja na TAIFA LETU TANZANIA
 
Mkuu unaweza kumuombea tu ili abadilike awe aina ya raisi umtakae. Sio lazima umuombee aendelee na huko anakotaka atupeleke kwa njia azitakazo yeye.
Sasa kama keshajiita kuwa yeye ni jiwe, unatarajia atabadilika vipi?
 
Sasa hapo weledi wa uandishi uko wapi?
Mbona story imejaa jazba na kuongea kwa kutoneshwa kidonda.

Hatuwezi kuendelea kusoma makovu ya watu.
Akajaribu huko aliko.
 
Yaani bandiko hili ndilo limemlazimisha Ansbert Ngurumo atafute ukimbizi wa kisiasa Finland?

Kama ninaambiwa nichague wa kumwombea kati ya Tundu Lissu vs Magu, hakika kwangu Mimi ni LAZIMA nimwombee Lissu

Kwa kuwa najua kwa matendo yake Magu hata nikimwombea, maombi yangu hayatamfikia Mungu, kwa kuwa atayapiga STOP njiani kabla hayajamfikia!
 
Back
Top Bottom