Alipitisha yeye alikuwa rais kipindi hicho?au hujui process ya utungwaji wa sheria?
We jamaa tumia akili zako japo kidogo, unadhihirisha unyumbu wako mbele ya jamii...!
Sheria hutungwa na bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania baada ya serikali kuipeleka muswada wa sheria kusudiwa bungeni.
Bunge linajadili na kupitisha muswada husika na baadae kurudishwa kwa rais kusain na kuwa sheria halali iliyotungwa na bunge, hivo inaanza kutumika rasmi nchini.
Kipindi mikataba mibovu na ya kinyonyaji ambazo sasa zinaonekana kulitia taifa hasara, huyo ndugu yenu anayejiita mzalendo na kutaka aombewe alikua bungeni akiungana na manyumbu wengine wa ukoo wa panya wakipiga meza na kusema ndioooo na hatimae kura za ndioooo zinashinda na kupitishwa sheria za kibaradhuli na kinyonyaji.
Pili hao wanao jiita wazalendo walikuepo kwenye baraza la mawaziri ambapo mambo mengi hupangwa na mikataba kujadiliwa, wote kwa pamoja ukoo wa panya waligonga gilasi na matokeo yake leo hii hiyo mikataba inalitia taifa hasara, ni mwenda wazimu tu ndie anaye weza kuwaelewa.
Hoja zinapoibuliwa na wazalendo wa kweli na watetezi wa rasilimali za taifa letu, ni vema mkajitokeza na kujibu hoja kwa hoja zenye mashiko, siyo hoja kwa silaha. Acha akili za kimakinikia zinduka mtanzania acha ubinafsi tuungane kama taifa kutetea rasilimali zetu.