Tumuombee Mhe. Lissu au Rais Magufuli

Tumuombee Mhe. Lissu au Rais Magufuli

Mimi nilishasema, Lilisu bora linge....tu. Hahahaaaa, nimeogopa

Ungemalizia tu Mkuu maana ndivyo mlivyotumwa kufanya ila Mungu amewaaibisha.

Nategemea 'PUA' yako imeangalia juu.hope umenielewa
 
Kama ushahidi wa JF uliweza kuiangusha baraza la mawaziri wakati wa JK (Richmond) naamini hata ICC siku moja wanaweza kupitia huku na kupata ushahidi huu!
 
Hakika Lissu alikuwa ni mwiba mkali kwa hawa waliouza nchi,kumbe sisonje haujui ni vita gani anapigana na Lissu anaelewa kila kitu......kazi kweli kweli!
 
Tundu Lissu alipoanza kusisitiza mara kwa mara kwamba mambo mengi yanayofanywa na Rais John Magufuli ni ya kukurupuka, na yataleta hasara kubwa kwa taifa, rais na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa yeyote anayempinga rais ni msaliti.

Hata majuzi, katika moja ya hotuba zake mubashara za hivi majuzi, Rais Magufuli alisema:

*“Nilipokuwa nikizungumza, ndugu zangu, kwamba hii ni vita ya uchumi, na vita ya uchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida.*

*“Vita ya kawaida, adui unamuona. Na saa nyingine msaliti anapowasiliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari wanajua kazi yao huwa wanafanya nini.*

*“Huwezi kuwa msaliti halafu ukawa… uka-survive (ukanusurika, yaani ukaachwa uishi).”*

Kwa Rais Magufuli na baadhi ya wapambe wake, Lissu ni msaliti, si mzalendo.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, wiki kadhaa zilizopita, kuna mtu alithubutu kumshambulia Lissu kwa maneno hayo makali, akisema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki si mzalendo.

Lissu hakusubiri mtu huyo ajibiwe na watu wengine. Alijibu mwenyewe akisema:

Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii. Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya (ya madini) tangu mwaka 1999.

Wakati huo, tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu – Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa CCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi bila kudai malipo Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, na kadhalika.

Sijui wewe ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani – alikuwa upande wa CCM na wanyonyaji hawa.

Soma gazeti la Rai la tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini (Rais Benjamin) Mkapa siku alipokwenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa anatetea “tumbo lake” na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya (kutetea wananchi wa) Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi, ila najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo, na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana naye. Ni muongo.

Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata kwa siku chache tu. Zingatia maneno yangu. Ataumbuka, na (nyie mnaomtetea) mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Mimi si mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga (makinikia) atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo, hana pa kwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati atakapokuwa anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa hohe hahe kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa fedha nyingi ya fidia na mahakama za usuluhishi za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya, basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. (Abdulkarim) Mruma haitamaliza hata nusu saa, iwapo itachunguzwa kwa kina.

Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina msingi wowote wa kuaminika. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka 1999, utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy, na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu.

Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni ujinga, hata kama ni wa kiprofesa. Hatuibiwi kwenye mchanga.

Huo ni ujinga unaoweza kukubaliwa tu na watu mbumbumbu. Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, basi, Mungu na atusamehe!

Kama serikali inasaini mikataba mibovu, na Lissu anapiga kelele kwamba mikataba hii ni mibovu na itaingiza taifa katika hasara, msaliti ni yeye anayesema au maofisa wa serikali waliosaini mikataba hiyo?

Msaliti ni yeye au rais anayetaka kumnyamazisha ili nchi isisikie sauti yake ya kinabii?

Kama viongozi wetu wamevunja mikataba; uamuzi wa viongozi wetu ukasababisha tushitakiwe, tukashindwa katika mahakama za usuluhishi; msaliti ni Lissu anayesema tumeshitakiwa na tumeshindwa?

Kama tunadaiwa na makampuni ya nje, yakakamata ndege yetu, Lissu akasema ndege yetu imekamatwa kwa sababu ya uamuzi mbovu wa viongozi wetu, na akasema watakaolipa fedha hizo si viongozi bali ni wananchi maskini; msaliti ni yeye au hao waliosababisha madhira hayo?

Kama rais anatoa amri zinazopoka uhuru wa wananchi kufikiri, kujieleza na kukusanyika – kinyume cha katiba – na Lissu anajitokeza kusema huu ni udikteta uchwara; inatosha kumuita msaliti?

Na katika mazingira ya “ugomvi” tunaoshuhudia mfululizo kati ya serikali na Lissu, na kwa kuzingatia matamko mabaya ya viongozi wakuu wa serikali dhidi yake; na sasa amepigwa risasi mchana kweupe, tutarajie nani awe mtuhumiwa wa kwanza dhidi ya Lissu?

Nimesikia kauli tata za viongozi wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Wanazungumza kisiasa na kwa jeuri isiyotarajiwa, kubeza wananchi wanaohoji unyama aliofanyiwa Lissu.

Kwa hili la Lissu, serikali na wapambe wake watatunga propaganda za kutoa watu mstarini, lakini tayari naona Mungu amewakatalia.

Rais Magufuli, katika hotuba zake kadhaa, amekuwa anataka tumuombee. Sasa, kwa matukio haya, taifa limetambua kuwa anayestahili kuombea ni Tundu Lissu.
Watu aina ya Tundu Lissu sio wengi duniani, ni wachache sana, Tanzania tuna bahati ilioje kuwa na Lissu....!

Lissu ni mzalendo wa kweli na mtetezi wa rasilimali za taifa, hata miccm wanajua na kuelewa anacho kisema Lissu siku zote ila ni unafiki, chuki ubinafsi uliowajaa mioyoni mwao.

Wanao imba kila siku kwenye majukwaa kuwa waombewe ni wanafiki na wapuuzi sana, nao ni miongoni mwa ukoo wa panya walioisababishia hasara na matatizo makubwa taifa letu.

Wakati Lissu akipinga juu ya mikataba mibovu na ya kinyonyaji kwa taifa letu bungeni, wao walikua wakigonga meza na zile kura za ndioooo ili kupitisha mikataba ya kinyonyaji ndani ya bunge, leo hii eti ndio wanajiita wazalendo na wenye uchungu na rasilimali zetu, huu ni unafiki wa hali ya juu sana.

Mtawadanganya na kuwarubuni manyumbu wenu wasio elewa ndio watakao endelea kuwapigia ndioooo na kuyashabikia mambo yenu ya kipuuzi, watu wote wenye uelewa wa mambo watawapinga kwa hoja hai na si mitutu ya silaha. Tanzania ni ya watanzania wote, hakuna mwenye hati miliki ya nchi hii, wapinzani si maadui.
 
Lissu ataombewa na familia yake. Rais Magufuli anastahili kuombewa na kila mtanzania.
Naona hata Mungu mmeanza kummiliki! Lakini haishangazi maana huenda tunazungumzia Mungu wa tofauti. Huenda kule magogoni kuna Mungu kawekwa humo si ajabu. Kama ni huyo, basi huyo si wetu bali ni wa DAB na JPM. Mungu wetu ni Mungu wa wote...Pen Down
 
CC: MODS: Hili ni chapisho lenye maneno ya kebehi kwa mkuu ws nchi, ni chapisho lililoandikwa kwenye gazeti la mwanahalisi lililopelekea gazeti hilo kufungiwa. Sidhani kams ni busara lihamishiwe kwenye Jukwaa hili ambalo limejijengea heshima yake.
Toka na li smg lako hapa.
 
Hii akili inaweza kweli kutengeneza mikakati imara ili sera yetu ya nchi ya viwanda ikamilike na tushuhudie viwanda halisi?
Hapo hamna kitu, hata boga lina akili kumzidi bichwa komwe!
 
Ni mwenye akili potofu tu ndiye anayeweza kumuombea mtu dhalimu kama huyu ambaye hana sifa ya kuongoza nchi yetu. Mkewe aliona mbali sana wangemsikiliza wangetuepusha na hili jinamizi nchini kwetu.

Kumuombea bwana yule ni Usumbufu kwa Mungu.
 
Wa kuombewa ni yule mkweli kwa ajili ya Mali za Tanzania sio mwongo mbele za watanzia
 
Magufuli alipitisha sheria zizizoleta mikataba hii mibovu, hansadi zipo!
Haya sema Lissu amesaliti nini?
Alipitisha yeye alikuwa rais kipindi hicho?au hujui process ya utungwaji wa sheria?
 
Alipitisha yeye alikuwa rais kipindi hicho?au hujui process ya utungwaji wa sheria?
Usiulize, jibu swali langu.

Uzalendo wa Lissu ni kuwa amesimama kidete kutetea sii tu rasilimali za nchi bali pia utawala bora.
Mpaka mnampiga risasi ili kumnyamazisha baada ya kukosa majibu ya hoja anazoziweka hadharani.

Magufyuuul alikuwemo kwenye baraza la mawaziri waliopitisha sheria hizo (rejea hansad)

Taja usaliti wa Tundu Lissu!
 
Back
Top Bottom