Tumuombe Mhe. Mkapa atuongoze tena japo miaka 5 tu

connections

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
1,736
2,297
Nina wazo wandugu ikibidi tumuombe Mhe. Mkapa arudi madarakani atuongoze japo miaka mitano. Najua katiba haikatazi yeye kurudi maana hajaunganisha zaidi ya miaka 10 maadamu amepumzika miaka 10 sasa atakuja na nguvu mpya na kasi zaidi kuendeleza ya awamu ya 4.
 
Nina wazo wandugu ikibidi tumuombe Mhe. Mkapa arudi madarakani atuongoze japo miaka mitano. Najua katiba haikatazi yeye kurudi maana hajaunganisha zaidi ya miaka 10 maadamu amepumzika miaka 10 sasa atakuja na nguvu mpya na kasi zaidi kuendeleza ya awamu ya 4.

Sipingi mtazamo wako najua ukikuwa utakuwa na mtazamo mzuri zaidi na mawazo ya busara.
 
yafaa akuongoze wewe na mkeo!
Unapoteza mda kufikiria option iliyo kinyume na katiba. Acha kuwa na mawazo mgando huu ni muda wa kufikiria kiongozi mwingine kati ya waTZ waliosalia
 
Unaweza Kumwomba wewe binafsi akuongozee familia yako, lakini sisi kama Taifa lenye watu wenye Maono hatupo Tayari kufanya Re-cycling ya Viongozi. Hii Tabia ya ni utamaduni wa CCM. Ukimwona anafaa uongozi ni uongozi tu Muraaaaaa, mkabidhi familia yako.
 
RADA(tutanunua tupo tayari kula nyasi),NDEGE ya kutua viwanja vitano tu,NYUMBA za SERIKALI,EPPA.BUNGE alikataza live,ripoti ya MKAGUZI WA HESABU YA SERIKATI Inapelekwa IKULU tu,haijadiliwi BUNGENI,AKUONGOZE WEWE NA AWALA YAKO.
 
Duu kweli watanzania wengine tunasahau haraka. Huyu ndiye aliyetuingiza kwenye mikataba mibovu ya madini. Pia alipitisha sheria mbaya ya madini ya royalty Asilimia tatu kwa dhahabu. Huyu ndiye aliyeuza mashirika yetu kwa bei chee ikiwepo NBC kwa makaburu. Huyo ndiye aliyeeingiza nchi kwenye ufisadi wa EPA. Huyu ndiye aliyeingiza nchi kwenye mafisadi wa radar. Huyu ndiye aliyeiingiza nchi kwenye kashfa ya meremeta. Huyu ndiye aliyeeingiza nchi kwenye kashfa ya kiwira coal mine. Huyu ndiye aliyeiingiza nchi kwenye kashfa ya minofu. Na huyu ndiye aliyeitwa Mr clean wakati anaingia madarakani Leo Sijui kama anaweza kuitika jina hilo. Mmesahau ukapa Mara hii. Duu kweli kutawala watanzania ni rahisi sana. Huyo hafai na hajawahi kufaa. Akaongoze familia yako labda. Hatujaishiwa na viongozi wazalendo na waadilifu wa kweli.
 
Naunga mkono hoja, tukifanya hivyo wala hatutakuwa tumevunja katiba maana katika haisemi chochote kuhusu mtu kurudi kuongoza baada ya kutoka madarakani kwa muda Fulani kasha kurudi tena kama mkuu wa nchi. Kama ni kashfa hakuna kiongozi yoyote humu dunani akose kashfa ikiwemo PAPA, Mkuu wa Kanisa katoliki duniani & Rais wa Vatican.
 
Mkapa akirudi Kuna watu itabidi wakimbie tuuu Kwanzaa maana team ya mkapa inataabika Sanaa nadhani mnawajua...sasa hao watu wakiwa free uraiani...team ya mkwere itatoa jasho la damu
 
Ni kitu cha kawaida kwa mtoto kuogopa kutembea gizani, tatizo kubwa ni pale inapotokea mtu mzima kuogopa kutembea kwenye mwanga.

Kipindi ambacho tupo Mkapa hatufai hata kidogo kwa sababu akiwa Rais alilenga kunusuru taifa kwa kuliweka rehani. Ni moja ya watu wanafiki tunapofanya analysis ya sera alizosaini. Nini kinakufanya uamini huyo mzee ni bora? Hivi hili taifa lina Mkapa? Hakuna watu rational?.

Bado nachelea kuamini akili na mtazamo wako kumpigia chapuo mtu asiyejali wapiga kura wake na kuona kifo kwa njaa na vipigo toka kwa polisi ni halali kwa sababu ya maslahi ya kundi dogo lenye nguvu kubwa.

Naendelea kujihoji ni criteria zipi ulizotumia kumuona Mkapa anang'ara kiasi cha kufanya uovu wake usiuone. Au kwa sababu ni rais wa kwanza wa kidemokrasia Tanzania, aliyehubiri utawala bora huku anasaliti watanzania?

Nisiseme mengi zaidi nikupe nafasi ya kutoa hoja za kumpendekeza.
 
Back
Top Bottom