Tumuogope mungu-kidela"

Tumuogope mungu-kidela"

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,991
Reaction score
30,188
Nipo mahali, wenyewe au members wanapaita Club. Nimekuja hapa nikiwa napita tu kushibisha tumbo kisha niende zangu home. Hapa mahali kuna wateja wa kila aina, wazee kwa vijana na wakike kwa waume. Muziki wa Bongo Flava unapigwa hapa na watu wanafurahi sana, maana ngoma ni zile kali kali.

Wimbo uliopo hewani sasa ni wa Abdul Kiba na Ally Kiba uitwao "KIDELA". Wimbo kiitikio chake kinaimbwa "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA, DUNIA MAPITO-KIDELA, MBELE KUCHUNGU-KIDELA, e.t.c".

Vinywaji pia ni vya kila aina, vile vyetu vilaini kama Juisi, Soda au Maji, pia vile vikali kidogo na vikali sana. "Penye Miti hapakosi Wajenzi", hivyo vinywaji hivi haviko burebure tu, bali wanywaji pia wapo. Hawa wanywaji/walevi hapa nao wanafuatisha wimbo huu kwa Juhudi kwelikweli.
-Nawaona walevi hawa wanavyojitahidi kuimba "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA",

-Pia naona wale dada zangu wanaopatikana pale nje ya Club kwa malipo maalumu nao wanaimba eti "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA"

-Nikicheki kule mbele nawaona wanaume fulani ambao ukiwaangalia kwa ghafla unaweza kudhani ni wanawake kwa mikao na mapozi yao ukiongezea ongea yao na tembea yao (Nimeeleweka), nao wanaimba eti "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA"

-Upande wa Pili huku gizani gizani nako naona Kuna Wateja wanaonekana kabisa ni Mume wa Mtu anaiba na Mke wa mtu. Yaani Mwizi wa Wake za watu yuko na mwizi wa waume za watu, maana wamejificha halafu wanakunywa kwa mashaka mashaka kwelikweli. Nao kwenye hiki kiitikio wanaimba kwa sauti ya juu kweli "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA"

- Kuna vijana nilipishana nao mahali wakiwa wanavuta Bangi muda fulani hivi wakati naenda msalani, nao nawaona hapa wakiimba kwa nguvu zote "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA"

-Wapo wengine ambao ukiwacheki tu sura zao zinaonyesha kama sio wakabaji basi watakua ni watu wa mishemishe fulani za kibabe maana wanatisha mno. Lakini nao wanaimba hapa "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA"

-Kuna wengine wamepiga "bingo" ofisini, zile bingo za magumashi a.k.a RUSHWA. Ingawa kuwatambua watu kama hawa sio rahisi lakini nina uhakika wapo hapa kwenye hii CLUB, nao pia wanaimba kwa sauti kubwa "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA"

-Hapa CLUB bana kuna hadi watu maarufu hapa bongo, Yupo Msanii wa BONGO MOVIE ambae kila siku haishi skendo za ajabu ajabu na mbaya kwenye magazeti ya udaku, lakini na namuona hapa anaimba moyo wote "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA"

-Hata yule mchezaji wa timu fulani ambae kipindi fulani mlisemaga kua ana tabia ya kupewa Rushwa ili auze Mechi kwa kucheza chini ya kiwango nae namuona hapa anaimba kwa sauti kweli "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA"

-Kuna yule Mwandishi wa Magazeti ya Udaku anaefuatiliaga skendo mbalimbali za wasanii ili apewe Rushwa asiziandike gazetini hapa nae anaserebuka kwa nguvu mno huu wimbo wa "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA".

List ni ndefu aisee, lakini "TUMUOGOPE MUNGU-KIDELA" inaimbwa na kila mtu hapa, wema na wabaya wote wanaimba. Najiuliza hawa watu wako serious kweli? Mungu ndio anaogopwa kwa style hii?? Haya bana, mie simo aisee.
 
tumuogope Mungu KIDELA dunia mapito
 
Mungu ni wa watu wote wenye mwili...pengine nafsini mwao watu hao wanajuta kwa hayo wayafanyayo.
 
Mungu gani?

Kuna watu wanaamini kila kitu kina mungu wake,kwa hiyo kilevi kina mungu wake, na kumuogopa munguwake maana yake ni lazima uabudu kilevi, et cetera et cetera.

Sasa ukiimba tu "tumuogope mungu" bila kufafanua mungu gani, wanaoamini katika kumuabudu mungu wa kilevi wataanza kugida zaidi.

The whole mungu idea is hokum. Cant stand examination.

Tumuogope mungu, dunia mapito, tusipomuogopa ndiyo itakuwa si mapito?

Some of these shorthand for morality populist tunes are taken way too serious. Muimbaji mwenyewe Ali Kiba anakwambia tumuogope mungu, halafu akitoka hapo anaenda kumgegeda madam kinyume na maadili ya dini yake.

Unafiki mtupu.
 
Mungu ni wa watu wote wenye mwili...pengine nafsini mwao watu hao wanajuta kwa hayo wayafanyayo.

Mkuu,

Yaani ungewaona jinsi walivyoufurahia huu wimbo, wala hata haionyeshi kuna kujuta nafsini
 
Mungu gani?

Kuna watu wanaamini kila kitu kina mungu wake,kwa hiyo kilevi kina mungu wake, na kumuogopa munguwake maana yake ni lazima uabudu kilevi, et cetera et cetera.

Sasa ukiimba tu "tumuogope mungu" bila kufafanua mungu gani, wanaoamini katika kumuabudu mungu wa kilevi wataanza kugida zaidi.

The whole mungu idea is hokum. Cant stand examination.

Tumuogope mungu, dunia mapito, tusipomuogopa ndiyo itakuwa si mapito?

Some of these shorthand for morality populist tunes are taken way too serious. Muimbaji mwenyewe Ali Kiba anakwambia tumuogope mungu, halafu akitoka hapo anaenda kumgegeda madam kinyume na maadili ya dini yake.

Unafiki mtupu.

Ha ha ha,

Dah, imebidi nikusome mara mbili mbili maana umeongea Point tupu. Ndio nakumbuka hapa kuna watu wanaabudu mapenzi, wengine wanaabudu pombe, wengine wanaabudu pesa!!
 
^^
Waache waimbe, kuimba kunapunguza mengi. Kila nafsi ina majuto yake.
Haijalishi ni unafiki au vinginevyo la muhimu wanaandika historia zao
^^
 
Back
Top Bottom