I was only tryin to cogitate...this's a one side story
du! babu naona unatoa karipio la nguvu.....
ila hata mimi nadhani ningemshauri hivyo kama hana sababu nzito ya kumfanya asizae kwa sasa.
Unajua kuna mabinti wengi tu huwa nawasikia wakisema wanataka kwanza kufaidi maisha baada ya ndoa wakae angalau miaka 2 bila kuzaa. hii inapendeza tena sana tu ila kwa makubaliano ya wote wawili. nani anataka shuruba za kukesha usiku na mtoto siku chache baada ya kuanza kuishi na mpenzi wake? lakini inapofikia kuwa mwenzio anahangaika kutafuta mtoto lakini wewe kontena hutaki kuhifadhi huyo mtoto kwa nini asitafute kontena jingine ambalo lipo tayari?
najiuliza unawezaje kuolewa na mtu ambaye huwezi kupanga naye maisha yenu?
swala la kupata watoto ni lenu wote wawili, mnaamua kwa pamoja, kila mtu anajua majukumu yake kama mzazi. kama mama anaona muda huo hawezi kutimiza majukumu yake ya uzazi kwa nini ashindwe kuongea na mwenzie? kama sababu zake ni genuine anaogopa nini kumshirikisha mwenzie?
nakumbuka tofauti ya mtoto wangu wa kwanza na wa 2 ni miaka 8, hatukuwa na tatizo lolote kiafya lakini mimi nilikuwa nina mambo mengine ya kufanya, na tukaongea kwa pamoja tukakubaliana tusitishe kuongeza watoto mpaka tutakapokuwa na nafasi ya kufanya hivyo. wote wawili tulijua nini kinaendelea kwa hiyo hakuna aliyekuwa anasumbuka kuhusu upatikanaji wa watoto, na maisha yalikuwa mazuri tu.
huyo dada kweli kamkosea mumewe. hata kama mume ni mbabe basi angeongea naye kwanza ili mume akatae. hiyo ingemfanya mume asihangaike mahospitali kutafuta mtoto.
Huyo rafiki yako kama bado anampenda mkewe na yupo tayari kumsamehe basi akae kwa utulivu kuongea naye. amsikilize sababu za yeye kutokata kuzaa kwa sasa, kama zina uzito basi amsikilize...... watoto watakuja tu hapo baadae.
du! babu naona unatoa karipio la nguvu.....
ila hata mimi nadhani ningemshauri hivyo kama hana sababu nzito ya kumfanya asizae kwa sasa.
Unajua kuna mabinti wengi tu huwa nawasikia wakisema wanataka kwanza kufaidi maisha baada ya ndoa wakae angalau miaka 2 bila kuzaa. hii inapendeza tena sana tu ila kwa makubaliano ya wote wawili. nani anataka shuruba za kukesha usiku na mtoto siku chache baada ya kuanza kuishi na mpenzi wake? lakini inapofikia kuwa mwenzio anahangaika kutafuta mtoto lakini wewe kontena hutaki kuhifadhi huyo mtoto kwa nini asitafute kontena jingine ambalo lipo tayari?
A friend of a friend is a friend.....
Salam wakuu wa mmu. Jana mida ya usiku nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu akiwa amepaniki na mwenye hasira nyingi. Tatizo aliliokua nao kwa kweli nilishindwa kumpa ushauri instantly (najijua na siasa zangu za mrengo wa kushoto) hivyo naomba nishee hapa jukwaani tuone tunamsaidia vipi ndugu yetu. Kwa kifupi jamaa ameoa na anapendana sana na mke wake na ndoa yao ina mwaka mmoja na miezi kadhaa. Wote wana successful careers ila tatizo lao kubwa ni kukosa mtoto. Hii imekua changamoto kubwa sana katika maisha yao na wamejaribu kwa kila jinsi kupata mtoto imeshindikana hali ambayo iliwalazimu kwenda hospitali ambapo wote walionekana hawana matatizo.
Kwa kweli swala la kukosa mtoto lilimsononesha sana rafiki yangu japo mke wake (kwa madai yake mwenyewe) alionekana kulichukulia kawaida na siku zote alikua akitoa jibu la "Mungu bado hajapanga tupate watoto). Sasa juzi jamaa wakati anatafuta charger yake ya simu chumbani baada ya kui misplace katika pekua pekua madroo akapigwa na butwaa baada ya kukuta 'contraceptive pills' kwenye droo mkewe akiwa amezificha. Anasema alishtuka sana ila alikausha adi mkewe aliporudi home ndo akaanza kumbana. Kumbana sana mwishowe mkewe akakiri kwa muda mrefu amekua akitumia contraceptive pills kuzuia aishike mimba kwa madai bado ni mapema sana naye ana mipango yake anataka kuaccomplish kwanza hivyo akizaa itaharibu mipango yake. Ndgu yangu amejisikia vibaya sana kwa jibu la mkewe huyo na amehitaji ushauri wa nini cha kufanya. Mimi kama nilivyosema siasa zangu za mrengo wa kushoto nimeshindwa kumpa ushauri kwani ungekua severe sana hivyo naomba basi wana mmu tuweze kutoa ushauri ambao tunahisoi utakua best solution kwa wanandoa hawa wawili. Asanteni sana.
Regards,
Don Lucchese.
mh!babu Mkali wewe!!! Utaua mtu!
hebu mkuu watu8 toka nje ya pandora box and think deeply what will be your reaction kama itatokea kwako
Dont go there.....Ni kweli unenayo mkuu, na hili linachangia ku raise suspicion kwamba kama hili la mtoto kanificha hivi je kuna mengine gani ambayo pia anayafanya kimya kimya? Sometimes I tend to agree kwamba women are complicated creatures.
lol!Mi ndo maana bibi yenu huyu kitu kiliweka kambi tumboni ndo nikatangaza ndoa.
kwani wewe ulikuwa unatafuta kontena la kubeba watoto au mke?Mi ndo maana bibi yenu huyu kitu kiliweka kambi tumboni ndo nikatangaza ndoa.
Unajua nimekuuliza lile swali ili nipime sababu ya huyo mwanamke...
Upande wa pili wa shilingi si ajabu rafiki yako ni mbabe na anataka kila aamualo liwe hilo /ndio maana shemejiyo akatumia hiyo njia...
Pia tungelijua katika mipango ya baada ya kuoana ni lini walitarajia kuanza kupata watoto, tungekuwa na namna nzuri zaidi ya kutoa shauri zetu.
Mwanamke kama huyo ni kumtafutia nyumba ndogo unazaa nayo. By the time anakuja kuwa tayari kupata mtoto we unawahi kufanya vasectomy. Anageuka mama mlezi wa wanao. Pambaf zake, hayuko tayari kuzaa kiherehere cha kuolewa alikitoa wapi?