donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,258
- 22,140
Hiyo mipango ya shemeji yako ni mipango gani??
Mpe pole sana huyo rafiki yako! Kimsingi jambo alilomfanyia huyo jamaa yako ni la kusikitisha siyo siri tena akimpumbaza kwamba MUNGU bado hajaamua wao kuwa na watoto, jambo la kuwa na watoto naamini ndiyo moja ya ajenda kuu ya wanandoa kuungana na kuanzisha familia, kama huyo mwanamke hakuwa tiyari au labda aliona ni mapema sana kuzaa angemshirikisha mume wake lakini siyo kutumia njia mbadala ambazo siyo halali kuzuia jambo hilo ambapo tiyari ameshamuathiri mume wake kisaikolojia!! Kwa kifupi huyo mwanamke hayuko tiyari kuzaa na huyo rafiki yako kwa hiyo haina haja ya kuendelea kuishi na mwanamke wa aina hiyo!!
Inawezakana mke ana nia njema sana ila kwa kutomshirikisha mumewe imekua mbaya sasa, We fikiria mmehangaika hadi mahosipitali mmekwenda na mke huyo huyo, kumbe nyuma anakucheka tu na kuweka unafiki eti Mungu hajapanga.
Ni kosa tayari mkewe amefanya kwa kutomshirikisha na kukubaliana juu ya hilo, Ikiwezekana achukue kalikizo ata ka siku mbili tatu na mkewe watoke wakakae sehemu kwa muda, wagombezane vya kutosha, mwishowe wataelewana cha kufanya. Na Mungu awasaidie.
Kiukweli hata mimi sifahamu ila sijui dunia hii ni mipango gani ambayo eti kwa kuzaa itaharibika. I find it more like an excuse
Kweli mkuu, ndomana sometimes naona sijui kuoa mwanamke literate ni majanga??
Unajua nimekuuliza lile swali ili nipime sababu ya huyo mwanamke...
Upande wa pili wa shilingi si ajabu rafiki yako ni mbabe na anataka kila aamualo liwe hilo ndio maana shemejiyo akatumia hiyo njia...
Pia tungelijua katika mipango ya baada ya kuoana ni lini walitarajia kuanza kupata watoto, tungekuwa na namna nzuri zaidi ya kutoa shauri zetu.
Kweli mkuu, ndomana sometimes naona sijui kuoa mwanamke literate ni majanga??
Mwanamke kama huyo ni kumtafutia nyumba ndogo unazaa nayo. By the time anakuja kuwa tayari kupata mtoto we unawahi kufanya vasectomy. Anageuka mama mlezi wa wanao. Pambaf zake, hayuko tayari kuzaa kiherehere cha kuolewa alikitoa wapi?
du! babu naona unatoa karipio la nguvu.....Mwanamke kama huyo ni kumtafutia nyumba ndogo unazaa nayo. By the time anakuja kuwa tayari kupata mtoto we unawahi kufanya vasectomy. Anageuka mama mlezi wa wanao. Pambaf zake, hayuko tayari kuzaa kiherehere cha kuolewa alikitoa wapi?
Mkuu watu8 hata kama jamaa ni mbabe anataka kile anachoamua kifanyike kitendo cha mama kutumia contraceptive tena kwa kificho bila kumwambia mume na huku mume anahangaika anajua wana matatizo na hospital wameenda na anamuona mume anavyohangaika na kumuacha haileti maana yoyote mkuu
Whether hiyo mipango ina manufaa kwa familia au haina au whether itawasaidia wnafamilia wote ila ilipaswa washirikishane na wasifichane kitendo cha mwanamke kukaa na mipango yake kimya bila mume kujua na huku mume anatarajia mama siku yoyote atapata mimba ni kitendo kibaya na wala hakileti maana kwa kweli