Tumsaidie huyu kimawazo

huyo binti anaanzaje kupanga mahari apewe nani wakati masuala ya mahari yanahusisha wazazi.
Wewe umeifunga mada.

Na kama kutakuwa na ukweli wa malumbano katika suala hilo, basi huyo binti ndiyo chanzo cha mgogoro.

Baba wa kambo kafuga na kulea joka linalokuja kumletea madhara makubwa sasa!

Huyo binti aelewe kuwa katika maisha kuna wazazi ama walezi wanaokuwa na hadhi sawa katika mustakabali wa malezi na makuzi ya mtu(mtoto).

Laana sometimes ndipo zinapoanziaga
 
Kama mtoto sio wako usihangaike kumlea kama unaweza saidia afu temana nae
Utamu wa Mama ndiyo utakaokufanya kumlea mtoto wake,usidhani watu wanapenda kulea tu,kuna mengi sana nyuma ya pazia!!
 
Huyo binti analeta complications tu. Unless otherwise pawe na story behind juu ya huyo baba mzazi ambayo haijawekwa wazi.

Maana haiwezekani mtu ambae amepotea tangia ukiwa na miaka mitatu, then uje kumuhusisha kwenye mahari.
Labda mwenye makosa ya baba mzazi kupotea ni Mama mzazi, na binti kweli ameona kua baba mzazi hana kosa!!
 
Kama mimi ndio huyo baba mlezi naachana na hilo suala na hata hiyo ndoa sijihusishi nayo kabisa
 
Shukrani kwa huu ushauri
 
Baba mzazi na mlezi wote watumie hekima.
Baba mzazi apokee pesa na kiasi kikubwa akamkabidhi mlezi.
 
Huyo binti na mama ake hawana Utu, shukrani kabisa. Baba mlezi awaache mama na mwanae wafanye wanachoona kwao kinafaa.
Ila malipo n hapa hapa Duniani.
 
Yule wa kambo amegoma kata kata mzigo uje kwake yeye ndie aliemtunza kuanzia mdogo mpaka alipo sasa nadhan atakuwa humu na kusoma mawazo yenu;
Mama yake yeye anasemaje?

Wale wajinga wa Kitanda hakizai haramu😂😂
 
Huyu mzee mwenangu atakuwa anafail mahali fulani. Makubaliano ya yeye kumwoa mama wa binti yalikuwa makubaliano yao wawili hayakuhusisha binti.
Kuhusu kumlea na kumsomesha pia nimakubaliano yake na mama yake binti, hayakuhusisha binti mwenyewe.
Mahari ni ujira unaotolewa kwa wazazi kama shukurani kwa upane wa pili baada ya kuchukuwa binti yao.
Kuachana kwa mama binti na baba binti hakumaanishi binti naye amchukie babake. Alafu mahari yenyewe kiasi gani hata imtoe roho huyu mlezi, uko kwetu Kanda maalumu tumekuwa tukioa kwa kutoa mahari ya ng'ombe mbuzi, kondoo na majembe, lakini kwa Harusi mjini ni hela hivo sioni sababu ya mlezi kulilia mahari ambayo kimsingi haiwezi kulingana na gharama alizotumia kumtunza huyo binti tangu akiwa na miaka 3 mpaka kumaliza chuo tena kwa kumsomesha utabibu, nani hajui gharama za kozi za afya?

Wenzetu huko Sudani mahari ni ng'ombe 100 -500 tena baada ya kutoa hiyo mahari mwanamke anakaa ndani tu kwa miaka 4 akifanyiwa kila kitu na mawifi huku akitumia muda huo kumsoma mme, baada ya hiyo miaka minne ndo inafanyika tena sherehe ya kupika ambapo ndo siku wanachinjwa kuanzia ng'ombe watatu na kuendelea ili mwanamke awapikie wakwe na familia ya mme.
Na endapo kwa kipindi hiki mwanamke hakukubaliana na tabia za mme basi anaweza kuchagua kuondoka na ng'ombe hawatarudishwa.

Hitimisho mzee mwenzangu achana na hizi stress zisizo za lazima na amabazo zitazalisha stress nyingine. Mzee mwenzangu usijidanganye kuwa mkeo anakupenda kuliko anavyo mpenda mwanae kitakachofuata hautokimdu kabisa.
Acha mahari apewe huyo baba mzazi wa huyo binti
 
Umeongea point nzuri sana. Kama mzee mwenzako angesoma hii ingemfaa sana
 
k
Shukran ila binti anataka baba yake mzazi achukue mahari
ana umri gan hako kabint hakajitambui hapo mahar apokee baba mlez ndie mwenye mchango mkubwa katika maisha yake na asipochunga litamkuta jambo atakosa msaada kwa baba mlezi kwa kumdharau na baba mzazi kula mahar na kusepa zake hatomuona huyu baba mzazi kilichomsogeza karibu na binti yake ni hiyo maharri hakuna kingine
 
Shukrani kabisa uwe na pasaka njema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…