Tumpongeze Rais Magufuli kwa ushauri wake kwa Benki ya Dunia na IMF. Viongozi wengine Afrika wamuunge mkono

Mm nadhani kufutiwa au kupunguziwa madeni ni muhimu hasa ktk kipindi hichi ch gonjwa hili la corona yy ameomba hajalazimisha hata ww unaweza kuomba ufutiwe madeni yako uliokopa hapa nchini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada kumbuka kilichoombwa na Magufuli kuhusu unafuu wa mikopo kwa nchi masikini zilizokumbwa na covid tayari kilishaombwa na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad. Magufuli amekopi tu. Kwanini hukumpongeza Seif?
Huyu nae! Sisi tunaongelea wakuu wa nchi wewe unatuletea mifano ya maguruguja wa mitaani. Leta mfano wa mkuu yeyote wa nchi barani Africa ambaye ameshatoa hoja hiyo.
 
Huyu nae! Sisi tunaongelea wakuu wa nchi wewe unatuletea mifano ya maguruguja wa mitaani. Leta mfano wa mkuu yeyote wa nchi barani Africa ambaye ameshatoa hoja hiyo.
Nilitaka tu kuweka sawa kwamba hilo sio wazo la Magufuli bali ni la Seif.
 
Napenda nizungumzie kipengele kimoja muhimu sana katika Hotuba ya Rais Magufuli jana alipokua akiongea na vyombo vya ulinzi na usalama ,halikadhalika akiongea na taifa kuhusiana na ugonjwa wa corona unaosababishwa na virus COVID-19.

Siwezi rudia yote aliyozungumza kwani yako wazi kabisa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kwa ujumla.

Rais Magufuli aliombwa na baadhi ya wadau mitandaoni aongee na Taifa wengi wakisema kajificha katelekeza nafasi yake anatakiwa atoke hadharani aseme neno, na jana kasema kama baadhi yetu walivyotaka iwe.

Bahati nzuri au mbaya kumbe wanaotaka aseme neno huwa wanataka aseme kile kinachowapendeza wao, na kwa kujua hilo Rais kashambuliwa na walewale waliotaka aseme neno kwa Taifa.

Napenda kwa upande wangu niongelee kipengele kimoja ambacho ni muhimu sana baadhi yetu tunakipotezea na kuangalia upande ambao utafaa kumshambulia.

Nakumbuka alizungumzia jinsi ya kujikomboa kiuchumi kutokana na gonjwa la Corona.

Rais Magufuli kaziomba taasisi za fedha za kimataifa (WB na IMF) kuangalia namna ya kuzisaidia nchi za Afrika, kwa aidha kuzifutia madeni au kuangalia namna ya kupitia upya riba za madeni hayo, kwa maana ya kuzipunguza badala ya kuruhusu nchi hizo kukopeshwa tena,(japo ni jambo jema) ikiwa na maana ya kurundikiwa madeni tena wakati hakuna shughuli za uzalishaji mali (kiuchumi)kama ilivyokua kabla ugonjwa huu.

Nafikiri ni kiongozi wa kwanza barani Afrika kutamka maneno haya yenye mantiki sana ispokuwa hayapewi kipaumbele.

Kauli hii ilinipendeza sana kwani Rais alilenga fedha hizo tulipazo madeni zitumike kama sehemu ya tafiti vifaa kinga na tiba kwa mataifa haya maskini. Ni jambo la kupongezwa sana kwa rais.

Imani yangu ujumbe huu usambae Afrika nzima na upigiwe chapuo na viongozi mbalimbali wa bara hili la Afrika kwani umoja ni nguvu.

Na kwa bahati nzuri leo ni kama nimesikia counselor wa ujerumani bibi Angel Markel kaungana na kauli hii ya muheshimiwa rais,kasema iko haja ya kufanya hivyo.

Nitoe wito kwa watanzania, Rais Magufuli ana nia njema kabisa na Taifa hili kadhalika Afrika kwa ujumla tumtunze tumuenzi, ni viongozi wachache sana Afrika wenye maono kama yake ya kutaka nchi au Afrika kwa ujumla iache utegemezi kama sio kuacha basi ipunguze kwa kiwango kikubwa utegemezi na hapo ndio uhuru kamili unapopatikana .

Ni mimi kapera mlima matikiti Lyangoko Makande,
Kwa maoni tuwasiliane kwa namba hii

0737 169 611

Du ni kiongozi wa kwanza???? Ebu sifuni penye kustahili Corona wenzie wako vitani toka January, Yeye alitakiwa kutilia mkazo serikali yake inafanya nini kuwanusuru watanzania kama Kulipa haraka madeni ya watu wanaoidai serikali, Kulipa pension sasa hivi, kutoa nafuu kwa mahitaji muhimu, yeye ni kuelekeza wenzie.

Nakubaliana kabisa na wewe Jiwe anayo nia njema sema weledi ndio mdogo katika madude complex na mtambuka, katika madaraja reli and etal yuko bien lakini yanayohusu utu na ubinadamu. Ukimlinganisha na wenzie katika swala la corona hapa EA yeye mpira kamwachia mwenyezi Mungu mapema.
 
Anaongea na taasisi za kimataifa kama anaongea na Waziri Kamwelwe pale darajani Moro! Asubiri kama watamsikia kwa style ile.
Zimesha fika
IMG-20200424-WA0000.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Man, yaani ulipoongea suala la "Na sijui kama Rais anawapenda watu wa namna hiyo!" nikajisikia kaubaridi fulani!
Umenikumbusha wakati nafanya kazi kwenye ofisi moja pale city center... kulikuwa na hawa washikaji wawili! Kuna mmoja, nikiongea mambo 10 basi angalau 7 lazima anipinge tu!

Huyu mwingine sasa... nikiongea mambo 10 yote lazima aniunge mkono na mengine mawili anayaongezea!

Trust me... ingawaje na mwenyewe nilikuwa namaani nachoongea ni sahihi bila kujali kwa wengine pia ni sahihi, lakini huyu aliyekuwa ananiunga mkono kila kitu alikuwa ananiboa kupita maelezo!!

Yule mpinzani wangu akiwa likizo au asipokuja kazini nilikuwa naona na-miss kitu kikubwa sana... CHALLENGE!!

What about Magufuli?!

Kuna siku hapa niliwahi kusema ningekuwa Magufuli ningekerwa sana na aina ya wafuasi wake ambao wapo tayari kuunga mkono kila kitu!! Na kariba ya Magufuli, sina shaka hata chembe hawa ndio aina ya wafuasi anaowapenda!!!

Kumbuka siku anakabidhiwa Uenyekiti alipomuambia JK wazi wazi kwamba "wale waliokuwa wanaimba wanamtaka bwana fulani ningekuwa ndo mimi, wangepotea" na kweli wangepotea... kivipi, anajua mwenyewe!

Hiyo inaonesha wazi hataki wafuasi wanaoweza kum-challenge bali anawataka wale wanaounga mkono kila kitu!
Katika utendaji kazi, kama hupendi watu wanaoku-challenge, you will never grow. Mtu unakua kimawazo, kiuwezo, kiutendaji, na kiweledi, unapopata wata au mambo yanayokupa challenge. Mambo hayo au hao watu watakufikirisha. Na kama ulikosea, utakapojisahihisha utakuwa u.epiga hatua moja mbele katika uelewa na kiutaalam.

Ukizungukwa na wanaokusifia tu maana yake kila siku utabakia na ulicho nacho. Na hali hiyo itakufumaza na kukufanya usiwe makini katika matendo, maamuzi na maneno yako maana utajua wapo wa kukushangilia kwa chochote utakachofanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unadai shilingi ngapi?
Du ni kiongozi wa kwanza???? Ebu sifuni penye kustahili Corona wenzie wako vitani toka January, Yeye alitakiwa kutilia mkazo serikali yake inafanya nini kuwanusuru watanzania kama Kulipa haraka madeni ya watu wanaoidai serikali, Kulipa pension sasa hivi, kutoa nafuu kwa mahitaji muhimu, yeye ni kuelekeza wenzie.

Nakubaliana kabisa na wewe Jiwe anayo nia njema sema weledi ndio mdogo katika madude complex na mtambuka, katika madaraja reli and etal yuko bien lakini yanayohusu utu na ubinadamu. Ukimlinganisha na wenzie katika swala la corona hapa EA yeye mpira kamwachia mwenyezi Mungu mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa akimwambia nani kuwa wasamehewe deni? Kama kukaa na viongozi wa usalama halafu unabwabwaja tu ujinga wa kusamehewa kunasaidia basi tuone hao Benki ya Dunia kama watafanya lolote? Alipe hilo deni....kwani hizo pesa zilienda kwenye kukabili CORONA? Magufuli anachezea fedha za mikopo. Lazima mfahamu zile fedha ni fedha za watu na nchi tajiri na zimewekezwa ili wapate faida ni kama ilivyo kwa Benki za CRDB na NMB.
Tanzania ilishasamehewa madeni mengi tangu ilipopata uhuru hadi leo lakini bado viongozi wana matumizi ya ovyo sana, sasa mnataka msamehewe? Viongozi wenyewe na baadhi ya wananchi KAMA WEWE mpo arrogant mnawatukana wafadhili wenu kuwa ni MABEBERU, Mnatukana mamba kabla hamjavuka mto?...HAMNA SHUKRANI. Lipeni madeni yenu!!!
Sema lingine
tapatalk_1587829406584.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom