Tumpongeze Rais Magufuli kwa ushauri wake kwa Benki ya Dunia na IMF. Viongozi wengine Afrika wamuunge mkono

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Napenda nizungumzie kipengele kimoja muhimu sana katika Hotuba ya Rais Magufuli jana alipokua akiongea na vyombo vya ulinzi na usalama ,halikadhalika akiongea na taifa kuhusiana na ugonjwa wa corona unaosababishwa na virus COVID-19.

Siwezi rudia yote aliyozungumza kwani yako wazi kabisa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kwa ujumla.

Rais Magufuli aliombwa na baadhi ya wadau mitandaoni aongee na Taifa wengi wakisema kajificha katelekeza nafasi yake anatakiwa atoke hadharani aseme neno, na jana kasema kama baadhi yetu walivyotaka iwe.

Bahati nzuri au mbaya kumbe wanaotaka aseme neno huwa wanataka aseme kile kinachowapendeza wao, na kwa kujua hilo Rais kashambuliwa na walewale waliotaka aseme neno kwa Taifa.

Napenda kwa upande wangu niongelee kipengele kimoja ambacho ni muhimu sana baadhi yetu tunakipotezea na kuangalia upande ambao utafaa kumshambulia.

Nakumbuka alizungumzia jinsi ya kujikomboa kiuchumi kutokana na gonjwa la Corona.

Rais Magufuli kaziomba taasisi za fedha za kimataifa (WB na IMF) kuangalia namna ya kuzisaidia nchi za Afrika, kwa aidha kuzifutia madeni au kuangalia namna ya kupitia upya riba za madeni hayo, kwa maana ya kuzipunguza badala ya kuruhusu nchi hizo kukopeshwa tena,(japo ni jambo jema) ikiwa na maana ya kurundikiwa madeni tena wakati hakuna shughuli za uzalishaji mali (kiuchumi)kama ilivyokua kabla ugonjwa huu.

Nafikiri ni kiongozi wa kwanza barani Afrika kutamka maneno haya yenye mantiki sana ispokuwa hayapewi kipaumbele.

Kauli hii ilinipendeza sana kwani Rais alilenga fedha hizo tulipazo madeni zitumike kama sehemu ya tafiti vifaa kinga na tiba kwa mataifa haya maskini. Ni jambo la kupongezwa sana kwa rais.

Imani yangu ujumbe huu usambae Afrika nzima na upigiwe chapuo na viongozi mbalimbali wa bara hili la Afrika kwani umoja ni nguvu.

Na kwa bahati nzuri leo ni kama nimesikia counselor wa ujerumani bibi Angel Markel kaungana na kauli hii ya muheshimiwa rais,kasema iko haja ya kufanya hivyo.

Nitoe wito kwa watanzania, Rais Magufuli ana nia njema kabisa na Taifa hili kadhalika Afrika kwa ujumla tumtunze tumuenzi, ni viongozi wachache sana Afrika wenye maono kama yake ya kutaka nchi au Afrika kwa ujumla iache utegemezi kama sio kuacha basi ipunguze kwa kiwango kikubwa utegemezi na hapo ndio uhuru kamili unapopatikana .

Ni mimi kapera mlima matikiti Lyangoko Makande,
Kwa maoni tuwasiliane kwa namba hii

0737 169 611
 
Anaongea na taasisi za kimataifa kama anaongea na Waziri Kamwelwe pale darajani Moro! Asubiri kama watamsikia kwa style ile.
Siku zote unayekopa huwez mpangia anayekukopesha ndo ikogi hivyo, yeye ndo anayempangia mkopeshagi
 
Ukiachana na mengine ambayo yametrend kama ya kujifukiza ambayo wapinzani wamechukua kama theme nzima ya hotuba ya Rais.

Ombi la msamaha wa madeni toka kwa taasisi za kifedha ni muhimu sana na jambo jema ambalo Rais kaliona.

Msamaha wa hayo madeni katika kipindi hiki utatufanya tuweze kujimudu vyema kifedha kwa kutegemea vyanzo vyetu kuliko kwa wao kutupa fursa tena ya kukopa ili tuzidi kujididimiza.

Hapo ndipo utaona malengo halisi za taasisi za aina hiyo.
 
Mkuu corona imeyakumba mataifa yote lakini pia nchi masikini wako kwenye safe side zaidi kuliko nchi tajiri.mfano Tz tuna kesi 284, rais anasema anazo habari zaidi ya watu Mia wamepona just in one or two months.

Sasa, Kati ya mdai ambaye hana dawa ya kutibu corona kiasi kwamba watu wake wanapukutika na mdaiwa wenye dawa kiasi kwamba watu wake wanaugua na kupona haraka na kuendelea kuchapa kazi, huoni pia Kama tungeweza kufikiria kulipa madeni yetu tungekuwa tumewasaidia na wao kutafuta dawa ya watu wao?
 
Attachments

  • IMG-20200423-WA0008.jpg
    IMG-20200423-WA0008.jpg
    50.2 KB · Views: 1
Hawa ni Mabeberu wazuri au Wabaya ?, ni vigumu kutambua siku hizi.....
 
Kama anakiri uzalishaji umepungua maana yake watu wake hawana uwezo wa kumudu maisha.

Je, yeye amechukua hatua gani kwa watu wake ambao wanahitaji yale mahitaji muhimu kama nishati ya umeme?

Je, ameshaongea na mashirika hayo kuangalia ni namna gani kwa kipindi hiki wananchi wanaweza wakapunguziwa gharama za nishati hiyo muhimu?
 
Ukiachana na mengine ambayo yametrend kama ya kujifukiza ambayo wapinzani wamechukua kama theme nzima ya hotuba ya Rais.

Ombi la msamaha wa madeni toka kwa taasisi za kifedha ni muhimu sana na jambo jema ambalo Rais kaliona.

Msamaha wa hayo madeni katika kipindi hiki utatufanya tuweze kujimudu vyema kifedha kwa kutegemea vyanzo vyetu kuliko kwa wao kutupa fursa tena ya kukopa ili tuzidi kujididimiza.

Hapo ndipo utaona malengo halisi za taasisi za aina hiyo.

Hizo taasisi moja ya kigezo muhimu ni utawala bora, sifa ambayo Magufuli na serikali yake hawana.
 
Ukiachana na mengine ambayo yametrend kama ya kujifukiza ambayo wapinzani wamechukua kama theme nzima ya hotuba ya Rais.

Ombi la msamaha wa madeni toka kwa taasisi za kifedha ni muhimu sana na jambo jema ambalo Rais kaliona.

Msamaha wa hayo madeni katika kipindi hiki utatufanya tuweze kujimudu vyema kifedha kwa kutegemea vyanzo vyetu kuliko kwa wao kutupa fursa tena ya kukopa ili tuzidi kujididimiza.

Hapo ndipo utaona malengo halisi za taasisi za aina hiyo.

Mkuu, wamesikiaje wakati anawaombea nchi masikini (alishawahi kusema sisi sio nchi masikini!) hawakupeleka ombi hilo kama umoja wa masikini?? Tulisikia SADC ikioomba nchi za magharibi ziondoe vikwazo kwa Zimbabwe - unaweza kutoa mrejesho ombi hilo lilifanywaje? Au ni kuongea na waandishi wa habari halafu inakuwa basi?

Unawaombaje wakusamehe deni wakati wa ghafla ya kuapisha na kutoa taarifa za korona?? Sisi hatuwezi kuchukuliwa kama tumeathiriwa na korona kwa sababu hatujasimamisha uzalishaji waka kuweka mazuio yanayoathiri uchumi. Inakuwaje tunaitumia korona kama sababu ya kusamehewa madeni? Nikukumbushe hapa Kenya, Rwanda wamefaidika na kuahirisha ulipaji wa madeni yao, kwanini sio sisi pia? Huoni alipaswa kuongea na wawakilishi wa wadai nchini? Hivi wakisema hawakupata structure ya msamaha unaoombwa watakosea??

Ninajiuliza tu kwa sauti!!
 
Mkuu hivi yeye ameshindwaje kuwasamehe watanzania angalau Kodi ya mwezi mmoja?Najua pesa hawezi kutupa,jamani hata kupunguza asilimia kidogo ya Kodi watu tujimudu ameshindwa why yeye aliyelie? Au nchi ni masikini bali watanzania ni matajiri?
 
Waanze wakubwa kusamehe ,msamaha huo ushuke chini,ndio kanuni hiyo mkuu
Mkuu hivi yeye ameshindwaje kuwasamehe watanzania angalau Kodi ya mwezi mmoja?Najua pesa hawezi kutupa,jamani hata kupunguza asilimia kidogo ya Kodi watu tujimudu ameshindwa why yeye aliyelie? Au nchi ni masikini bali watanzania ni matajiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajuaje ?,pengine kaongea nao kisha katoka hadharani kwa watanzania na dunia nzima,kauli ya rais ndio msimamo wa nchi moja kwa moja

Back
Top Bottom