Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 121,947
- 95,237
Wacha kujidhalilisha wewe, sisi hatuwezi kuomba msaada maana sisi ni matajiiiriiii sana
In God we Trust
Napenda nizungumzie kipengele kimoja muhimu sana katika Hotuba ya Rais Magufuli jana alipokua akiongea na vyombo vya ulinzi na usalama ,halikadhalika akiongea na taifa kuhusiana na ugonjwa wa corona unaosababishwa na virus COVID-19.
Siwezi rudia yote aliyozungumza kwani yako wazi kabisa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kwa ujumla.
Rais Magufuli aliombwa na baadhi ya wadau mitandaoni aongee na Taifa wengi wakisema kajificha katelekeza nafasi yake anatakiwa atoke hadharani aseme neno, na jana kasema kama baadhi yetu walivyotaka iwe.
Bahati nzuri au mbaya kumbe wanaotaka aseme neno huwa wanataka aseme kile kinachowapendeza wao, na kwa kujua hilo Rais kashambuliwa na walewale waliotaka aseme neno kwa Taifa.
Napenda kwa upande wangu niongelee kipengele kimoja ambacho ni muhimu sana baadhi yetu tunakipotezea na kuangalia upande ambao utafaa kumshambulia.
Nakumbuka alizungumzia jinsi ya kujikomboa kiuchumi kutokana na gonjwa la Corona.
Rais Magufuli kaziomba taasisi za fedha za kimataifa (WB na IMF) kuangalia namna ya kuzisaidia nchi za Afrika, kwa aidha kuzifutia madeni au kuangalia namna ya kupitia upya riba za madeni hayo, kwa maana ya kuzipunguza badala ya kuruhusu nchi hizo kukopeshwa tena,(japo ni jambo jema) ikiwa na maana ya kurundikiwa madeni tena wakati hakuna shughuli za uzalishaji mali (kiuchumi)kama ilivyokua kabla ugonjwa huu.
Nafikiri ni kiongozi wa kwanza barani Afrika kutamka maneno haya yenye mantiki sana ispokuwa hayapewi kipaumbele.
Kauli hii ilinipendeza sana kwani Rais alilenga fedha hizo tulipazo madeni zitumike kama sehemu ya tafiti vifaa kinga na tiba kwa mataifa haya maskini. Ni jambo la kupongezwa sana kwa rais.
Imani yangu ujumbe huu usambae Afrika nzima na upigiwe chapuo na viongozi mbalimbali wa bara hili la Afrika kwani umoja ni nguvu.
Na kwa bahati nzuri leo ni kama nimesikia counselor wa ujerumani bibi Angel Markel kaungana na kauli hii ya muheshimiwa rais,kasema iko haja ya kufanya hivyo.
Nitoe wito kwa watanzania, Rais Magufuli ana nia njema kabisa na Taifa hili kadhalika Afrika kwa ujumla tumtunze tumuenzi, ni viongozi wachache sana Afrika wenye maono kama yake ya kutaka nchi au Afrika kwa ujumla iache utegemezi kama sio kuacha basi ipunguze kwa kiwango kikubwa utegemezi na hapo ndio uhuru kamili unapopatikana .
Ni mimi kapera mlima matikiti Lyangoko Makande,
Kwa maoni tuwasiliane kwa namba hii
0737 169 611
In God we Trust