Nina rafiki yangu mmoja amekuwa na mpenzi tangu chuo.
Yeye alimtangulia mwenzake mwaka mmoja kumaliza na alipomaliza akarejea kwao Shinyanga na dem wake ni wa Njombe.
Licha ya umbali uliojitokeza hawakuweza kutengana maana lengo lao ni kuoana.
Huwa wanashinda wanachat karibia siku nzima lakini bado huyu jamaa anakuwa na wasi wasi na anawaza sana kwamba upo uwezekano wa kuibiwa huyu mpenzi wake.
Wanaweza kupitisha hata mwaka hawajawahi kukutana ila wanawasiliana vizuri kwa simu, wanagombana na kupatana pia.
Wadau naombeni tumshauri huyu jamaa kweli mapenzi ya namna hii yanaweza kupelekea ndoa?
Na je huyu mchumba wake anaeza kuvumilia kipindi chote hiki bila kumegwa?
Pia itakuwa sio mbaya kumshauri afanyeje kuondoa tatizo la wasi wasi na mawazo aliyonayo.
Mwambie hivi; Mapenzi ya mbali ni kama upepo na moto!! Kama moto umejishika vizuri kwenye mkaa upepo ukipunga utakolea zaidi lakini kama haukushika vizuri basi pindi upepo ukipunga tu moto utazimika.
Inamaana: Umbali unaweza kuimarisha zaidi mapenzi yao kama kuna penzi la kweli kati yao, kama kuna anayezuga kati yao basi wajue hamna kitu hapo!!
Mwambie airuhusu nafsi yake iamini kuwa hakuna nayemega kwasababu hajawahi kumfumania. Lakin kama angewahi kumfumania basi angeweza kuwa na waswas juu ya hlo. Akiumiza sana kichwa atakonda na atashindwa kufanya mambo ya maana
It is ok,kama wanapendana inawezekana! Iam talking out of experience..cha msingi wajikite ktk kuimarisha na kujenga maisha yao ya baadae wakiwa pamoja...Distance is nothing infront of Love,they can do it..True love is always so Powerful (japo sikuhizi true love is rare).
the way ulivyoelezea ni kuwa hao jamaa zako wanamawasiliano mazuri,mi sioni tatizo hapo chamsingi mwambie huyo rafikiyo afanye taratibu za kufunga ndoa ili mmoja wao amfate mwenzake apate amani ya moyo wake,full stop !!!!
it works kama kweli wana nia na mapenzi ya dhati...kama wameshavumiliana all these years kwann waone tatizo sasa???mshauri jamaa apunguze wivu au atakufa na kijiba cha roho!!
Mtu moja wa hapa alisemaga "distance is made to see how far love can travel"...so acwe na waswas japo smtimes waswas ndo akili na jamaa kuhis anaibiwa nadhan ni pale anapomuuliza mdada "uko wap??" na yey anajibu "mlimani city" bas jamaa anaona anaibiwa duuh wivu bhana