Tumpe muda Rais Magufuli aweze kuyatekeleza aliyoahidi

accused

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,496
2,743
Huwa napita humu wakati mwingine nafarijika na Mara nyingine nasikitika sana. Jf wakati wa usahili wa members wake kuna vigezo muhimu hawakuzingatia ili wote wanaokuwemo wawe ni great thinkers! Baadhi ya topic/comments zinazonishangaza humu ni hizi.

1. Rais Magufuli alituahidi viwanda pindi tu aingiapo madarakani, sasa yamemshinda ". Hivi kweli ndani ya miezi 5 Rais ndan ya ikulu angewezaje fufua viwanda? Kwaninitusimpe muda? Mbona bado sana. Acheni uelewa Mdogo viwanda vina mlolongo mrefu na vtafunguliwa tu.

2. "Magufuli anateua watu baki kua CEO's wa mashirika makubwa nchini". Kwahiyo hata kama waliopo ndani ya shirika siyo competent Rais awateue tu kwasababu ni wazoefu? Dawa ya jino bovu ni kuling'oa wakuu.

3. "Magufuli hafuati katiba ya nchi,anatumia Pesa bila kuidhinishwa na binge".
Nani kasema Haya, sote kwa wale wenye uelewa, nchi yetu imepata mtu tuliemhitaji kwa muda mrefu sana, let him work for us!

4. "Magufuli anatumbua vipele majibu kayaacha".
Think, ukitaka uangusha mbuyu huezi anzia katikati, lazima uuzunguke na mwishoe wakuta wamalizia kiini kirahisi sana.

5. "Magufuli hafanyi gender balance katika teuzi zake"
Kwahyo hawa mama zetu hata kama siyo competent tuwape tu kisa ni wanawake? Hizi siyo zama za JK na Hawa Ghasia tena .

Nb. Tusubiri, tumuombee na kumtia nguvu Rais na watendaji wote ili watufikishe pale tulipotaraji. Kutimiza yote at once siyo rahisi but let's hope the man will do!
 
Mbaya zaidi wote mliokuja changia ndio team ile ile ya kukosoa utendaji wa mh. JPM!! Kuna wengine humu huchangia vitu hadi unajiuliza hivi hawa ni standard one au four.

Mshana Jr wewe lazima umchukie sana JPM maana ile janja janja ya kukwepa kodi kushnei.
 
rais unaenda kutishia kutaja majina ya wafanyakazi hewa!what a shame
 
Back
Top Bottom