Mimi si shabiki wala mwanachama wa chama chochote bali ni shabiki wa kazi nzuri za Rais Magufuli na nafurahia anapokosolewa kwa staha.
Mimi Kama kijana na mwananchi wa kawaida kabisa ninaona Freeman Mbowe anastahili heshima sana kutoka kwa vijana wa taifa hili kama ambavyo wazee wetu wengi wa CCM, serikalini na dini wanavyomheshimu.
Mbowe ana mchango mkubwa katika maendeleo ambayo taifa hili limeyapata katika miaka 15 iliyopita na mingi itakayokuja.
Mbowe ameandaa vijana wengi machachali na kuwa viongozi na baadhi yao sasa wanahudumu katika serikali, bunge na wengine wengi ambao ni wabunge wajao, mawaziri, nk.
Najua Mbowe siku moja ataachia ngazi CHADEMA lakini nawakumbusha wanachadema, wafuasi wa vyama vingine na Watanzania kwa ujumla, tumpe Mbowe heshima anayostahili akiwa hai. Tusimfanye ajutie kwa jasho alilotoa kwa taifa hili. Mbowe ni binadam, na anakosea, lakini tukumbuke mazuri yake zaidi.
Kazi nzuri anayofanya Rais wetu kipenzi imetokana na kuwepo upinzani imara ambao nguzo kuu ni maono na utashi chini ya Mbowe. Rais wetu kipenzi asingepatikana bila Upinzani thabiti kutoka chama kinachoongozwa na Mbowe.
Hatupaswi kumkweza, kumbeza wala kumtesa kwa vijembe au upambe wa kinafiki. Bali tumpe heshima yake amefanya mengi makubwa indirectly kuliko baadhi ya viongozi wakuu wa nchi hii.
TUMPE HESHIMA ZAKE MBOWE AKIWA BADO ANAISHI.
Sent using Jamii Forums mobile app