Curious gal
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 3,200
- 4,010
Hahahahahhaahaaaa nilivurugwa nikasema sitaki utani kabisa!!!! Nashukuru niliipata hela yanguAsante sana, wana mambo ya ajabu na kwa ishu kama yako ya kulipia fees unaweza vurugukiwa na tumbo ukahisi unakufwaa!![emoji23]
nilikuwa na mizunguko zaidi ya wiki moja sasa imeisha, nawaza zikifika siku 14 nikatoe taarifa polisi maana hili ni suala la kibiashara. uzuri zimetumika namba zangu binafsi, na tin namba ya hilo jina la kibiashara inalitaja jina langu. sijui kama nitakuwa sahihi. wajuvi wa masuala ya sheria naombeni msaada tafadhali.Kuna mengi yamewakuta watumiaji wa mpesa mtawasikia
Hii mambo inachanganya sana, kwa hiyo mpaka leo hii bado hujapata token?nami nagongelea hapo hapo kama mhanga sugu wa transactions/miamala ya ki-elektroniki.
19.10.2017 nimenunua umeme kwaajili ya mashine ya kusaga kupitia MOBISTOCK. nikakatwa 20,000 na meseji yao ikatumwa kwamba salio limetumwa TANESCO na kwamba token zitatumiwa kwenye simu yangu.
nimezoea meseji ya arifa kuwa pesa imekatwa huambatana na ya tokeni (namba zinazojazwa kwenye mita). siku hiyo ikapita hadi zaidi ya dk 30. nikapiga simu. tena hii huduma ya mobistock unapiga simu kwa gharama halisi. sio bure km zilivyo huduma nyingine. nikajibiwa tatizo liko tanesco. kesho yake 20.10.17 nikapiga, 21.10.17 hadi 25.10.17 hadi leo hii sijapokea tokeni na salio halijarejeshwa.
wahudumu sasa wamebaki kunifokea kwamba tufanyeje sasa hali tatizo liko tanesco?
nami nahoji, nimuulize nani sasa endapo ninyi ndio watoa huduma, basi nipeni namba ya tanesco nishughulikie mwenyewe, wao hukata simu.
ebu fikirieni 20,000/= ya kununua lau 56kwh ingeshazunguka mara ngapi. imeshikiliwa kwa siku 12+ sasa.
hii ndiyo Tanzania na maisha yanasogea tu!
Wapuuzi sana mimi walirudisha baada ya kuwaanzishia kizaa zaa kwenye page yao FB, na hapo nishakaa zaidi ya siku ishirini wanarudisha pesa tayari nishatatua ishu yangu. Hovyo sana tena hao customer ni vihiyo waliotukuka!sita wasahu hawa watu....walikula hela hivihvi...nilifanya transactio ikakaa hewani kwa week tatu eakaniambia itarudishwa kwangu bt kitu cha ajabu kabisa ni kwamba baafa ya week tatu ile transaction ilifanikishwa. Wakati huo nilishamaliza shida yangu kwa kutumia Mtandao mwingine. M pesa ni wezi hakuna mfano
Hutakiwi kuchoka bro hilo ni jasho lako how come useme umechoka? Mie pamoja na kukaa siku kibao sikukata tamaa kila nilipopata muda niliwapigia kuwakumbusha. Katika pita pita zangu huko FB nikakutana na page yao aisee nliwavuruga hadi pesa yangu ikarudi hapana chezea pesa kizembe zembe arifu.Mi mwemyewe nilifanya manunuzi ya mpesa kwao ilikuwa usiku. Huduma sikupata na pesa sijarudishiwa hadi leo. Kila ukipiga wanakwambia baada ya 24hrs sasa ni wiki tatu hadi nimechoka
Next time nafanya hivi maana pia nishachezewaPeleka malalamiko yako tume ya mawasiliano (TCRA), ukiwa na barua rasmi yenye maelezo yako na nakala za vielelezo kutoka Mpesa. TCRA ndiye regulator wa mitandao ya simu. Pia kwa sababu mtandao wao unajihusisha na mambo ya pesa peleka malalamiko yako Benki kuu ambao ndio hutoa leseni ya kufanya biashara ya pesa kukomesha uhuni unaofanywa na hawa viumbe.
kina uzi wao humu wenye sticky lakini waliutelekeza utadhani jamaa walianzisha ujenzi wakaishia msingi kisha mwenye nyumba akapata kesi na kufungwa jela. msingi hauna hata wa kung'olea magugu.Ni wizi tuu huo mbona kipindi cha nyuma Voda mlikua mnarudisha pesa haraka sana pindi mtu akikosea sasa hivi watu hawakosei ninyi ndio mnawaibia ni hatari sana kwa kweli kutumia mitandao yenu kutuma fedha...