Tumfanyaje huyu dogo?

Tumewahi kukubaliana namna hii mkuu but kuna sister na anti yetu mmoja kila akitua selo wanamtoa.

Nimewapenda hao ister na aunt...it means karibu kila mtu there's someone behind his back who's not tired of your shit
 
Mnamwendekeza bhana.. Mmemfundsha vya kutosha ni zamu ya ulimwengu kumfunza
 
mi nadhani kumuacha sio suluhisho halafu kumbuka huyu ni ndugu wa damu hivyo likimtokea lolote haijalishi usivyopenda ayatendayo lazima roho ikuume

fanya haya mawili kwa pamoja

  1. maombi juu yake na matendo yake ili Mungu ambadilishe
  2. tafuta askari na hakimu, waweke sawa hakikisha wanamchezesha kifungoni kwa wiki/miezi/miaka kadhaa....yaani kila akija mahakamani kesi inaahirishwa baada ya huo muda kama hajakaa sawa basi kamuombeni msamaha aliyemloga
 
Tumewahi kukubaliana namna hii mkuu but kuna sister na anti yetu mmoja kila akitua selo wanamtoa.

eeeh! labda hamjajua namna ya kudhibiti hiyo mianya ya hao wajinga. mfateni sister mumpe makavu kama hakai sawa mpelekeni kwake akakae (mnamsusia)
 
Mweke kwenye maombi iko roho ambayo inamsumbua. mim kaka yangu ilikuwa ni shida! unajua shida? ni shiiida! lakini hakuna linalo mshinda Mungu, tafuta mafuta ya mzeituni yapeleke yakaombewe then mchanganyie kwenye yakeake kidog tu mwachie Mungu mwenyewe NB. kabla ya kuombewa unayasemea mungu akufanyie nini kasha yanabarikiwa.
 

Hakika, maombi ndio suluhisho la huyu dogo.
Huenda 'anaendeshwa' na mapepo au mizimu ya kwao.
 
uko mkoa gani kama ni hii mikoa ya kaskazini mpeleke kwenye utalii huko mafyatu wanatokaga hata iweje
 
Tumewahi kukubaliana namna hii mkuu but kuna sister na anti yetu mmoja kila akitua selo wanamtoa.

Ndo wannaompa kichwa hao sasa..wanawake wana huruma kupitiliza, mlitakiwa mumuache walau kidogo. Au mtaftieni mahali kijijini mkamtupe uko achunge mbuzi weee adabu ataiona.
 
malezi mabovu au mapepo kichwani,akipata kesi ongea na hakimu apelekwe jela yenye shamba akalime atatia akili akirudi full displin ila asijerudi na kaugonjwa ka kulaw** na magonjwa mengine hatarishi..
Vinginevyo wandugu mtengeni kifedha na muda,akija kwako aishie mlangoni tu au getini,
 
pole ila si bure alichukuaga/kudokoa/kuiba cha mtu na hajawai kwenda kumwomba msamaa.ebu kaa nae muulize
 

akienda jela atajifunza kwa iyo akifanya uhalifu let him go the jail
 
Solution yenye uhakika ya kumsaidi haipo ila atakuja kubadilika mwenyewe kadri umri unavyokwenda au asije kubadilika kabisa

Kuna watu wengine wanakua mwili ambao hauendani na kukua kwa ubongo. Unachosema ni kweli.
 

kama vip mchukue wewe ili arudi kundini maana.
 

Anahitaji ushauri nasaha. Labda niulize aliachwa na wazaziakiwa na umri gani? ( it is not easy). Mnasema labda ninyi mpo je tayari mnafamilia zenu au?. Mnadhani alifit vizuri kwenye famila zenu. Binadamutunatofautiana kupokea matatizo. Matafutenimnasihi/ mwanasaikolojia atamsaidia ikiwa ni kupata njia mahsusi ya yeyekufunguka na kujitambua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…