tumetoka mbali!... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tumetoka mbali!...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Mar 14, 2009.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  barua.jpg

  ...ushawahi kumbwa na dhahma ya kuitafutia barua marashi kuipulizia, halafu ukakumbana na tabasamu na vicheko ukikatiza mbele ya mashoga zake walosoma 'gazeti' uloandika?

  those days boarding school :D!!!!!!!! ...hamna cha sms wala email...ha haa..

  ...wikiendi hii share nasi experience zako miaka hiyo
   
 2. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Yes enzi hizo boarding ni barua tu hamna simu za mkononi. Ukipata barua imetoka kwa bf unajisikia kweli.Ukiandika wewe unapulizia unyunyu wako,nilikuwa napenda seduction perfume baada ya kutumia sana cobra!
  ilikuwa lazima nimkumbushie kwenye barua huu msemo
  Love start with a smile
  Grow with a kiss
  and end with tears!
  Ukikosa barua,siku ukitoka nje ya shule kama kwenda kuswali/kusali najitumia barua nionekane nakumbukwa..
  Kuna siku nikakosea kutuma baruaz, ya mdingi nikamtumia bf halafu ya bf nikamtumia baba,niligundua wakati zimeshawafikia! Huwa sisahau hiki kitu,baruaz mambo ya boarding we acha tu!
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ha -ha -haaa! inaonekana BelindaJacob ulikuwa na AUTOGRAPH enzi za primary school,...

  mnazikumbuka Autograph jamani? mnazungusha darasani ma best wana sign

  nyimbo wanazopenda;
  chakula wanachopenda;
  (kazi) career unayoipenda;
  nk nk....?

  kisha unamalizia na Quote! ha ha haaaa...

  leo hii mambo ya AUTOGRAPH yamehamishiwa kwenye FACEBOOK, HI5 nk.... tekinolojia bwana!!!
   
 4. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2009
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yakhe umenikumbusha mbali, hawa wanasemema unyunyu, wengine hatukuwa na uwezo wa kumiliki kobra. Barua ikishaandikwa inachorwa maua kwa kutumia poda nyekundu na nyeupe (tibeti na bint el sudan) zilikuwa zinanukia hizooo. Ama kweli watu wa posta walikuwa na kazi enzi hizo.

  Nakumbuka nikiwa form one siku moja jamaa bwenini kwetu alitumiwa nguo iliyovaliwa. Baada ya parcel kufunguliwa bwenini pakawa hapakaliki. Cha kushangaza jamaa wakawa wanaigombania kama mpira wa kona.
   
 5. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Ni kweli aise teknolojia imetubadilisha sana. Nakumbuka nilisaini autograph ya mdada mmoja mshkaji wangu...yaani lilikuwa daftari nikabandika na picha..sijui sasa hivi..nikiletewa ile picha na yale niliyoaandika how will I feel!

  Life, bana ni safari ya ajabu sana. Ndo maana ni vyema kila sekunde ukaiishi kwa ukamilifu wake. Maana kila kinachotokea katika maisha yako leo..hakitajirudia..
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Yes autography nilikuwa nayo tena kuna moja mpaka leo ninayo,nikiisoma sasa naishia kucheka na kukumbuka enzi hizo.
  kweli teknolojia imekuwa sana siku hizi ni mambo ya social networks kama hizo.
   
Loading...