Tumetoka mbali: Unawakumbuka watu hawa na mambo haya?

Neema ya Bima lee nayo hii hapa, tupate burudani na ujumbe


Nimesimama kwenye Mnara wa Bismin

Barabara kuu iendayo Bandari ya Salama

Majonzi yamenijaa machozi yanidondoka

Naiwaza sura ya Neema

Naiwaza sura ya Malaika wangu eeee eee

Nitoe nitoe kizimbani niwe huru ooo niwe huru


Usiniache pweke Neema

Nitasema na nani Mama (Nitalia na nani Mama )


Usifuate wasemayo Wafitini

Hao wako mbelembele kuharibu mapenzi yetu mimi nawe


Maneno mengi sana nilishasema

Usifuate ya wambea watakuja kutuvurugia

Unayaona sasa yametufika Mpenzi

Tumetengana bado tunapendana

Fanya hima.............

Usiniache pweke Neema

Nitasema na nani Mama

Usifuate ya wasemayo wafitini

Hao wako mbelembele kuharibu Mapenzi yetu mimi nawe

Ulipotamka Adios Amigo

Uliniacha Mama ninateseka Mpenzi

Sina mwingine Neema ooooo

Sina mwingine mama

Fanya uje ....

Usiniache pweke Neema...............
 
Visa vya mesenja ya Max nayo hii hapa wakuu

Wee Mesenjaa..........,
Hallo sekretari ...... Ah be,
Eheee Mesenja yuko wapi? ...... sijui bosi,
Mara mesenja anaibuka na kusema ..... ,
Naam bosi nilikuwa uani tumbo linaniletea matatizo mie,
Ee bosi akasema nenda posta ofisi kachukue barua za ofisini na za nyumbani,
Za ofisini lete ofisini na za nyumbani peleka nyumbani,

Mesenja kaleta balaa nyumbani kwa meneja bila kufahamuuu uuh uuh,

Mesenja kaleta balaaa nyumbani kwa meneja bila kufahamuu uuuuh,

Wakati anatoka posta ofisi anawaza moyoni,
Mzee mie darasa la tatu la mkoloni,
Mke wangu na wanangu wamelalia ugali wa muhogo na chunga la kuchemsha jana,
Akaingia Kariakooo anaikimbiza mia wakati siku hizi mia imeota matairi,
Kutoka posta ofisi akakuta ofisi imefungwa,
Na mlangoni yupo mlinzi,
Akajaribuuu kumbembeleza apokee zile barua akakataa,
Akazipeleka nyumbani kwa bosi wake akamkuta mkewe,
Mke wa bosi akabidi azichambue kwa kuwa si desturi barua za ofisini kufika nyumbani,

Siri imefichuka siriiiii imefichuka,
Kosa la mesenja kaleta balaa,
Kosa la mesenja kaleta aibu,

Siri imefichuka siiri imefichuka,
Kosa la mesenja kaleta balaa,
Kosa lamesenja kaleta aibuuuuuuu.....

Akaanza kuzichambua,
Kachukua ya kwanza kaweka kando,
Kachukua nyingine kaweka kando,
Kuchukua nyingine akaona mwandiko umelalia kushoto
Hati kama ya kike,
Akaifungua kichwa cha habari haloo darling,
Akazimia nusu saa masikini,

Siri imefichuka siri imefichuka,
Kosa la mesenja kaleta balaa,
Kosa la mesenja kaleta aibuuu...........

Alipozinduka kamkuta mwanae mdogo amemuegemea,
Anasema mama nasikia njaa,

Mimi sipiki akija baba yako mwambie aje apike,
Kuna anawajengea majumba na kuwanunulia magari,

Mimi nimekosa nini jamaniii?,

Aliporudi bosi anagonga mlango anaambiwa,
Akalale huko huko kwa anaowajengea majumba na kuwanunulia magari,
Akabembeleza akafunguliwa mlango,
Ile kuingia ndani zogo kubwa likaanza,
Mara maneno,

Mara kavuliwa koti,
Mara kachaniwa shati,
Mesenja kaleta aibu nyumbani kwa meneja bila kufahamuuu,

siri imefichuka,

Siri imefichuka,
Kosa la mesenja kaleta balaa,
Kosa la mesenja kaleta aibuu.......


 
Mzuzu unatisha mkuu,kweli unadhihirisha kwamba wewe ulikuwa ni Nginde damu,safi sana kaka


Mkuu mie mkereketwa wa bendi zetu na nyimbo zinanikuna sana hadi leo mzee. Kila ninapokaa na PC yangu nasikiliza hizi nyimbo tu ndugu yangu na kavasha zinanikuna sana!
 
kweli Balantanda umenikumbusha mbali sanakipindi hicho
BOXING
Paul Sizza, Samwel Pataul (Okapi), Charles Mhilu (Spinkx),Isangura, Habibu Kinyogoli, Stanley mabesi, Abdala Mgeni, Emmanuel Mlundwa,Matumla Rashidi na wengineo

MIELEKATX
Chaka, Benard, Bukuku, Iranda, na wengineo

waganga wa kienyeji maarufu
Dr Majura, Prof Vulata, Sheick Yahaya, Bi Hawa Nyamwicha

Kipindi hicho kwa wale wa Dar watakumbuka kuanzia Ijumaa mpaka jumapili Uswahilini ni Midundiko na Ngoma za kimakonde tu
kwenye mamboa ya muziki, naomba jamani mwenye nyimbo za Zairi Ally Zorro, aniwekee hapa
KISA CHA FOTO ALBAMU
"wamenieleza mambo yako ee mamaa
wamenieleza matatizo ya mume wako
japo ukutaka waniambie
photo albamu imeleta maneno
katikati ya Dar es salama
picha iliyopigwa zamani ee
katkati ya jiji la mwanza

Pia naomba mashairi ya huu wimbo
Tulikuwa tupo Arua wazazi wetu
kwenye mipaka ya Uganda na nchi ya Sudan
kwenye Mipaka ya uganda na nchi ya Zaire
kwenye kijiji cha Koboko
 
Enzi hizo kila mzazi anadai alikuwa wa kwanza darasani...
Teh teh teh sasa sijui kila mzazi alikuwa anasoma shule yake kila mmoja au?
 
kumbuka kikosi cha Taifa Star hiki 1-Juma Mensah (Pondamali) 2-Leopord Tasso Mukebenzi 3-Mohamed Kajole Machela 4-Salim Amir Mtaalam 5-Jella Mtagwa 6-Mohamed Rishard Adolf 7-Omar Hussein Keegan 8-Hussein Ngurungu 9-Peter Tino 10-Mohamed Salum 11-Thueni Ally
Kocha Slow Work toka Poland, 1-Msaidizi Joel Bendera 2-Msaidizi Elija Katigile
 
wazee hakuna aliyehifadhi sauti hizi adimu katika video ama kasseti?.maana zinashinda hata halua kwa utamu
 
Nawakumbuka wapiga solo mahili Duncan Njilima wakati akiwa na western Jazz na marehemu King Enock wakati akiwa na Dar.Jazz na wimbo wao : Ah simu yako nimepata na hayo maneno yako yote; ........mimi ni mkubwa kwako....mtoto acha kupiga mayowe wacha watu waone wenyewe!!
 
Balamtanda, katika watangazaji mahili wa mpira ninaowakumbuka waliokuwa RTD ni Mshindo Mkeyenge, Barthlomeo Komba na Abdul Ngalawa. Nadhani hawa inawezekana walikutangulia sana!!
 
Balamtanda, katika watangazaji mahili wa mpira ninaowakumbuka waliokuwa RTD ni Mshindo Mkeyenge, Barthlomeo Komba na Abdul Ngalawa. Nadhani hawa inawezekana walikutangulia sana!!

Bwana weee mpira ni chaz hillary na omary Jongo...
hao wengine ndioo walikuwepo lakini hawa jamaa walikuwa ni noma.
 
Hiyo Simba na Villa shamba la bibi kwenye redio chaz anataja list ya villa...
Golikipa ni charles simbwa
Nambari mbili poul hasule
Nambari tatu geofrey yigenyi
Halfback 4 ni willy mkemba
Sentahalf ni adam semugabi.....

Aaah kweli zamani ilikuwa rrrrraha.
 
Wazee mumeandika mengi sana ya enzi zetu, ila mmesahau mambo ya "Club Raha Leo Show", "Mikingamo", "Mbiu ya Mkoa", "Gurudumu la Maendeleo" nk.

Haya mambo ya utandawazi yameharibu kabisa nidhamu ya nchi. Bia zilikuwa haziuzwi madukani kama ilivyo sasa. Guest zilikuwa ni mahali ambapo pana bar.
 
Chief, Nimekukubali, nakumbuka nikiwa form six kuna ndugu yangu mmoja alikuwa ananitoa pale GOGO hotel na kule sigara TCC changombe kwa MK beats. (Wana - Sukumambesaa)

Kwa muziki -wimbo wangu wa kwanza kuujua ulikuwa Milima ya kwetu - niliupenda sana enzi hizo. nikiwa vidato vya chini.

Hongera kwa collection yako - imetulia papamukulu
 
Bwana weee mpira ni chaz hillary na omary Jongo...
hao wengine ndioo walikuwepo lakini hawa jamaa walikuwa ni noma.

Duh kaka Omary Jongo alikuwa kiboko mpira upo mbaliii utamsikia eeeeeeheeeee mambo yameivaaa hapa uwanja wa taifa - amini usiamini kilitokea kizaazaa langoni mwa ........... chaz hebu elezea.....
 
Wazee mumeandika mengi sana ya enzi zetu, ila mmesahau mambo ya "Club Raha Leo Show", "Mikingamo", "Mbiu ya Mkoa", "Gurudumu la Maendeleo" nk.

Haya mambo ya utandawazi yameharibu kabisa nidhamu ya nchi. Bia zilikuwa haziuzwi madukani kama ilivyo sasa. Guest zilikuwa ni mahali ambapo pana bar.

Nakumbuka wimbo uliokuwa unapigwa kufungua kipindi cha mikingamo --- tuimbe wote

Mikingaamo sauti ya wasemakweli iyooo nitasema tuuu....iyooo nita....... kiitikia: nitasema kweli daima fitna kwangu mwikooo

huyu ni yule Keptain wetu - J.komba Mzee wa numberiONE ni ........ nambariwani eeeeee.....

mmhh tumetoka mbali sana - Mnakumbuka pia kipindi cha mama na mwana cha Halima Kihemba? na chei chei shangazi....

Nilikipenda sana hasa zile hadithi tamu alizokuwa anatuhadithia. aaaa bora ubakie mtoto tu kuliko uwe mkubwa na tanzania yetu hii ya ufisadi mtupu.
 
Pia mambo ya mashindano ya kucheza Disko ndiyo yalikuwa mahali pake(sasa hivi naona yamedorora sana).Enzi hizo kulikuwa na wataalamu kama Mussa Simba(Black Moses),
Bosco Cool J,Savy Pops,Cadet Bongoman,Hussein Shadrack Guga a.k.a Kokoliko,Maneno Super Ngedere,Sabbah A. Jackson na wengine kibao.Pia alikuwepo motto mmoja toka Kenya akiitwa Kanda Kid,dogo alikuwa mbaya sana,alichukua ubingwa Afrika Mashariki miaka hiyo


Umemsahau Queen Clouds lol

Enzi zile wa TZ walikua hakuna TV ,so wakawa hawajui nini kinaendelea nje ya TZ na ni mitindo gani ina chezwa . Siku ambayo mashindano ya East Africa yalifanyika, kuingia kundi la TZ ,Wakenya wakabaki mdomo wazi kwa mshagao, maana watu wan vunja ma breka, wakati ilikua imesa pitwa na wakati, Wakenya waka hojiwa wakasema wanashangaa kuona watu wan cheza Break Dance ...
 
Kwa Manguli waliotajwa hapo juu ambao wametangulia mbele ya haki ewe Mola zipumzishe roho zao mahali pema peponi,Amen.
 
Ukweli ni kuwa hivyo vipindi vya RTD vyote vipo ila watangazaji ni tofauti lakini waliovaa viatu vya wale wakongwe...

Kwa mfano mimi majuzi nilikisikia kipindi cha misitu ni uhai na kawimbo kake ndo kalinifanya nisimame na kukasikiliza kwa makini, kaliimba hivi...

John Komba:
Watanzaniaaa bara na visiwaniii
Tuyahifadhii mazingira yeetuuu
Tangu zamaniii tulipewa urithii
Tuikumbukeee misitu ni uhai haya...

jama mnakakumbuka hako kawimbo?
Kalikuwa kanaunguruma majira ya saa kumi na moja furani hivi jioni..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom