Tumetoka mbali: Unawakumbuka watu hawa na mambo haya?

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,752
Nikianza na Muziki,kwa kipindi cha nyuma muziki wa Dansi(ya ukweli) ulikuwa umeshamiri sana nchini kwetu kiasi kwamba enzi hizo redioni ilikuwa ni mwendo wa muziki wa Dansi tu.

Kuna baadhi ya wanamuziki ambao kwangu mimi huwa ni vigumu sana kuwasahau kutokana na mchango wao katika kuufanya muziki wetu (enzi hizo) uwe maarufu. Binafsi siwazungumzii wanamuziki wa miaka ya 60 na 70 bali nawazungumzia wanamuziki wa miaka ya 80 mwanzoni mpaka miaka ya 90 ambao daima walinivutia na abado wananivutia kutokana na uzuri wa miziki yao,wanamuziki hawa kwa sasa ni marehemu,hivyo nimeona ni bora niitumie nafasi hii japo kwa uchache kuwashirikisha katika kuwakumbuka mashujaa wangu hawa wa muziki.

Kila mtu anajua kwamba kuna wanamuziki ambao huwezi kuacha kuwataja mara tu uanzapo kuuzungumzia muziki wa Tanzania,wanamuziki hawa ni kama akina Salum Abdallah,Mbaraka Mwinyshehe Mwaruka,Marijani Rajabu n.k(Mungu awarehemu). Mimi leo nimeguswa kuwakumbuka wanamuziki hawa wafuatao:-

1. Hemed Maneti Ulaya:-Mzee mzima mwenyewe wa Vijana Jazz Air Pambamoto, huyu
mkulu kwa kweli alikuwa ananikosha mnoo kwa utunzi na uimbaji wake kiasi kwamba
alipachikwa jina la Chiriku. Baadhi ya nyimbo(ninazozijua) ninazozipenda mpaka leo ni
kama Maria,Tambiko la Pambamoto,Bujumbura,Penzi haligawanyiki sehemu ya 1 na
ya 2 na nyingine nyingi tu.Huyu bwana alikuwa na kipaji kwa kweli.

2.Eddy Sheggy:- Huyu bwana naye alikuwa na kipaji,ukisikiliza nyimbo zake kama
Milima ya kwetu (akiwa na Super Rainbow), Penzi haligawanyiki, Ogopa Tapeli, Mwisho
wa mwezi nk (akiwa na Vijana Jazz), Nelson Mandela, Shakaza(akiwa na Washirika
Tanzania Stars, wimbo wa Shakaza aliurudia pia alipohamia Bima Lee Orchestra) au
Nyimbo za Baba Jenny na Gondoigwe (akiwa na Bantu Group) uatona ni jinsi gani naye
Alikuwa na kipaji cha kuimba.

3. Jerry Nashon Dudumizi:- Mtaalamu mwingine wa Vijana Jazz ambaye daima mimi
namkumbuka kwa nyimbo zake tamu alizotunga na kuimba akiwa na Vijana Jazz,
nyimbo kama VIP,Shoga,Theresa na nyingine nyingi tu…..

4. Suleiman Mbwembwe:- Huyu namkumbuka kwa nyimbo yake tamu ya Mama Chichi
(akiwa Vijana Jazz) na nyingine nyingi akiwa na Juwata/Ottu Jazz/Msondo Ngoma.

5. Francis(Nassir) Lubua, mtaalamu mwenyewe wa Nginde Ngoma ya Ukae

6.Tino Masinge "Arawa"….Sina la kusema hapa jamani…R.I.P

7. Ali Kishiwa Mhoja "TX Moshi William"…Aaargh,kifo jamani.Ukisikia mtu ana kipaji TX alijaliwa hasa, sina haja ya kutaja kazi yake, inajulikana.

8. Athuman Momba:- Kifaa kingine hiki cha Vijana Jazz na Msondo Ngoma…R.I.P

9. Le supreme Fredy Ndala Kasheba:- Mzee wa ZAITA MUSICA wana ZUKE ZUKE
Muselebende,nani atavishau vibao vyake vitamu kama Marashi ya Pemba,Dezodezo
(Tshala Muana aliununua huu wimbo) ama ule wimbo mtamu wa Kesi ya Khanga
(mama nipe nauli nikamfuate Monica,amekimbilia Zambia na Treni ya mizigo, kisa cha
kukimbia madeni yamemzidi, Doti kumi za Khanga alizokopa hajalipa)….dah

10. Suleiman Mwanyiro "Computer": Mtaalamu huy wa gitaa zito (besi) wa Nginde

11. Kalala Mbwembwe:- Huyu bwana alikuwa Tancut Almas baadaye akaanzisha bendi
ya Ruaha International,namkumbuka kwa nyimbo zake kama Lutandila,Safari n.k

12. Kyanga Songa:- Huyu bwana alikuwa na pacha wake tangu Sambulumaa,Tancut na
baadae Ruaha International

Wakuu kwangu mimi hizi ni Hazina zilizotoweka ghafla tukiwa bado twazihitaji.Tuendelee kuwataja wengine ambao nimewasahau…Sasa hivi muziki wa Dansi Bongo ni kama umejifia tu,hakuna kitu,kila kitu vijana wanakopi muziki wa Kikongo tuuuuuuuuu…..Pa1
 
Siku hizi hakuna hata yale Mashindano ya Bendi Bora Tanzania(MASHIBBOTA)
 
Nakumbuka enzi hizo hakukuwa na Redio za FM,kulikuwa na RTD basi,kwa Dar hata studio za kurekodia muziki hazikuwepo ilikuwa bendi ikitaka kurekodi muziki wanaenda RTD ndio wanarekodi,Studio nyingine ilikuwepo Arusha ambayo ilikuwa inarekodi nyimbo za Injili tu,hii ilikuwa ni Studio ya Redio Habari Maalum…Tumnetoka mbali kwa kweli wakuu wangu.

Enzi hizo hakuna cha Bongo Fleva wala nini,ni mwendo wa Dansi tu,nakumbuka hata vipindi vya RTD vilikuwa maarufu sana,vipindi kama Mchana mwema,Jambo,Kombora,
Top Ten Show kila Jumapili saa nne na robo usiku(Na mtangazaji brazameni wa kipindi hicho Uncle J Nyaisangah),Kijaruba kila Ijumaa saa nne na robo usiku na Abdallah Mlawa,Kipindi cha Starehe na BP mtangazaji akiwa Uncle J Nyaisangah,Club Raha Leo Show mtangazaji akiwa Handsome boy Enock Ngomale Mwiru akisaidiana na Geofrey
Erneo.Pia kulikuwa na vipindi kama Mama na Mwana(Deborah Mwenda na Hayati Siwatu Lwanda)…RTD ilikuwa juu kipindi hicho kwa kweli

Pia kulikuwa na wataalamu wa kutangaza mpira bwana,sio hawa akina Nkamia na wenzake wa siku hizi,enzi hizo bwana kuna wataalam kama Omar Jongo,Ahmed Jongo,Salim Mbonde,Ahmed Kipozi(mechi za Dodoma),Abdallah Majura,Mikidad Mahmoud,Charles Hilary,bila kumsahau mtaalamu mwenyewe Dominick Chilambo mzee wa kanda ya ziwa Mwanza amabaye alikuwa anaipenda timu ya Pamba ya Mwanza kiasi kwamba akwa anawaita TP(Tout Puissant) Lindanda Kawekamo,ilikuwa raha kwa kweli enzi zile.

Nwakumbuka sana watanmgazaji kama Abdul Ngalawa,Sekione Kitojo,Sarah Dumba
Halima Kihemba,Idrisa Sadallah,Chisunga Steven,Abisai Steven,Angalieni Mpendu,Hendrick Michael Libuda.Benjamin Kikoroma(BEN KIKO),Rosemary Mkangara,Edah Sanga,Nkwabi Ng’wanakilala,Dunstan Tido Mhando,Malima Ndelema,Richard Leo,Nathan Rwehabura na wengine wengi ttu..Pia Sauti ya Tanzania kulikuwa na mzee mmoja mtaalamu wa methali na nahau akiitwa Yusuph Omar Chunda…Ilikuwa raha sana kipindi kile.

Kipindi hicho hakuna cha TV wala nini,siku ya mpira wa Simba na Yanga watu mwakaa vilingeni chini kuna redio mkulima mnawasikiliza akina Jongo wanavyofanya vitu vyao kututangazia moja kwa moja kutok auwanja wa Taifa..Pia mtu ukikosa kusikiliza mchezo wa maigizo wa akina mzee Jangala,au wa akina mzee Jongo ama vichekeso vya akina Pwagu na Pwaguzi unaonekana bonge la mshamba yaani…Tumetoka mbali kwa kweli
 
Pia mambo ya mashindano ya kucheza Disko ndiyo yalikuwa mahali pake(sasa hivi naona yamedorora sana).Enzi hizo kulikuwa na wataalamu kama Mussa Simba(Black Moses),
Bosco Cool J,Savy Pops,Cadet Bongoman,Hussein Shadrack Guga a.k.a Kokoliko,Maneno Super Ngedere,Sabbah A. Jackson na wengine kibao.Pia alikuwepo motto mmoja toka Kenya akiitwa Kanda Kid,dogo alikuwa mbaya sana,alichukua ubingwa Afrika Mashariki miaka hiyo
 
Halafu kipindi hicho hakukuwa na cha Kwa Fujo DJs wala Nyuki DJs..Disko lilikuwa lapigwa na maDJ wataalamu(mabitozi wa enzi hizo)baadhi yao ni kama DJ Chriss Phaby,
Young Millionaire(Jacob Usungu wa RFA),Nigger J(Masoud Masoud),DJ Joe Kusaga,DJ
Kalikali,DJ Kim,Choggy Sly,Hayati Deo Kiduduye(Super Deo???) na wengine ambao nimewasahau…Ilikuwa raha iliyoje kwa kweli wakuu
 
Halafu kuna Timu za miaka ya 90 hata sijui ziishia wapi kwa sasa:-

.Kulikuwa na wakali Pamba bwana,hawa jamaa walikuwa wanatisha kiasi kwamba kuna
siku waliichapa timu moja ya Gabon(nadhani ni Mbilinga fc) kwenye mashindano ya
vilabu Afrika magoli 12..Nawakumbuka wachezaji wakali wa PAMBA kama akina Beya
Simba,Hamza Mponda,Fumo Felician,Kitwana Suleiman,Madata Lubigisa,Deo Mkuki,
Paul Rwechungura,David Mwakalebela,Hussein Aman Marsha,George Magere Masatu
Na wengine,sasa umkute Hayati Dominick Chilambo anawataja hawa ilikuwa raha.

.Tanga walikuwepo African Sports wana Kimanumanu,sijui wamefia wapi hawa jamaa
na wenzao Coastal Union wagosi wa kaya

.Shinyanga kulikuwa na timu za Mwadui na Biashara,Hii Biashara ndo iliwatoa Edibily
Lunyamila na mtaalamu Suleiman Kingsley Malwilo.

.Kagera ilikuwepo RTC Kagera sijui imeishia wapi hii

.Arusha ilikuwepo NDOVU na Moshi ilikuwepo Ushirika(Namkumbuka Julius Kalambo
na Abeid Kasabalala).Sijui zimefia wapi hizi timu

. Dodoma zilikuwepo Kurugenzi,Waziri Mkuu na CDA Watoto wa nyumbani…dah

.Rukwa ilikuwepo Ujenzi Rukwa na Katavi Rangers na Iringa ilikuwepo Lipuli bwana.

.Mbeya zilikuwepo Mecco(ya akina Rshid Mandanje) na Tukuyu Stars(hawa ni bwana
walikuwa mabingwa wa mwaka 1986 walipanda daraja na kuchukua ubingwa).Hapa
ndipo walitoka akina Mbwana Makata,Justin Mtekele,Godwin Aswile,Jimy Mored,
Salum Kussi,Stephen Mussa,Joshua Kilale,Godfrey Katepa na wengine wengi tu.

.Lindi ilikuwepo Kariakoo na Mtwara ilikuwepo Bandari,zote hizi kwishnee

.Moro walikuwepo Reli bwana,Kiboko ya vigogo,hapa Simba na Yanga walikuwa
wakigusa lazima wale kichapo.Nawakumbuka wakali wa Reli kama Duncan Mwamba,
Mohamed Mtono,Fikiri Magoso,Abdallah Mkali,Duncan Butinini,David Mihambo na
Mbui Yondani,hawa jamaa walikuwa wanatisha sanaaaaaaa.

.Tabora walikuwepo Milambo bwana wakiwa na wachezaji wao wakali kama Peter Poka,
Wastara Baribari,Mikidadi Jumanne,Mussa Msangi,Mrisho Moshi,Idd Moshi n.k

.Kwa Zanzibar nazikumbuka Small Simba,Malindi na Jamhuri.Nakumbuka Malindi
mwaka 1994/95 walikuwa na mfadhili wao Naushad Mohamed alimwaga pesa kiasi
kwamba Malindi wakasjaili wachezaji wa kimataifa kama Modorn Malitoli na Alfred
Mapataki(Zambia) na Mbulgaria(ni Julian Albetov kama sikosei),pia waliwachukua
Wabara kama Nico Bambaga na Edy Lunyamila.Jamaa walitisha mnoooooooo katika
Ukanda huu wa Afrika Mashariki.Timu hizi sijui zimeishia wapi kwa sasa.

Pia nawakumbuka waamuzi maarufu wa enzi hizo kama Gwaza Mapunda,Joseph Mapunda,Musa Lyaunga wa Rukwa,Nassor Hamduni wa Kigoma,Hafidh Ali na
Juma Ali David wa Zanzibar bila kuwasahau wachezaji wataalamu na wenye vipaji kama akina Hamis Thobias Gaga,Athumani China,Issa Athuma Mgaya na mdogo wake Kasongo Athuman,Damian Morisho Kimti,William Fahnbuller,Sahau Kambi,Idd Pazi,Stephen Nemes,Mackenzie Ramadhan,Idd Selemani Meya,Ngandou Ramadhan,Kimanda Constantine,Celestine Sikinde Mbunga,Mchunga Bakari,Bakari Tutu,Victor Mkanwa,Juma Burhani,Innocent Haule,Salum Kabunda(Ninja/Msudan au Baba Semeni),Dua Said,Said Mrisho(Zico wa Kilosa),Zamoyoni na Method Mogella,Hassan Afif.Lance Evance Ponera,Victor John Bambo,Aboubakar Salum(Sure Boy) Fred Felix Majeshi Kataraiya Minziro(Baba Issaya),Mwanamtwa Kihwelo,Jamhuri Kihwelo,Mussa Kihwelo,Mhehe Kihwelo,Nicodemus Njohole,Deo Njohole(OCD)….Zamani tulikuwa na vipaji kwa kweli,sijui tulikuwa tunashindwa wapi tu.
 
Mkuu unakumbuka mambo sana tena kwa usahihi hongera sana,mie nakumbuka mechi yangu ya kwanza kwenda kuangalia nikiwa dogo baada ya mdingi kunitoa bushi ilikuwa kati ya nyota nyekundu na Pamba ccm kirumba hiyo mwana.Unamkumbuka Frank kasanga bwalya.Na mechi yangu ya kwanza kuuona uwanja wa ccm kirumba umejaa na kutapika ilikuwa kati ya ghana na Taifa stars,mechi ambayo Michael Paul "Nylon" alipiga mpira wa uhakika.Kwa jinsi mtoto alivyokuwa akiseleleka mpaka marehemu Chilambo akawahawezi kutamka jina lote,anasema MAIKOPO.AAAAAH HAPO ZAMANI
 
Yeah,pamoja mkuu..nawe umenikumbusha mbali sana ulipomtaja Frank Kasanga Bwalya na Michael Paul...Pia walikuwepo Raphael Paul(RP),Mavumbi Omari,Khalfan Ngasa,Issa Kihange,Abdul Ramadhan Mashine na wengine...Soka ya kipindi hicho ilikuwa tamu bwana,acha tu
 
dah miaka ya 80 soka wadau ilikuwa noma mnamkumbuku peter tino international alitupeleka lagos na bao lake kwenye african cup of nation? yanga enzi hizo akina isihaka hassan chuku, allan shomari, charles boniface mkwasa, juma mkambi, makumbi juma homa ya jiji, abedi mziba, ahmed amasha, aboubakar salum sure boy, lawrence mwalusako, athumani juma chama na wengineo simba akina lila shomari, zuberi magoha, zamoyoni mogela golden boy, idd pazi father. hawa jamaa walitisha sana. kuna majimaji fc walikwepo akina isihaka majaliwa, samli ayoub, sijaona tena mido yenye control km octavian mrope, hamis fande, mzee wa kiminyio madaraka suleiman, celestine sikinde mbunga,peter tino hawa walishakuwa mabingwa bara na muungano. nakumbuka timu zilizokuwa zikija na kushinda pale majimaji ni simba ya ramadhani leny, hussein amani masha na pamba ya kina joram mwakatika, mwakalebela na uzi wao mweupe kuanzia soksi bukta na jezi ya juu halafu kifuani zimeandikwa pamba kwa thiodane. nyota nyekundu akina john manyama, steven chibichi, aziz nyoni.
 
Balantanda we ni Noma..

Kwa hakika mambo haya walio wengi tumeyafaidi sana, lakini ni vigumu sana kuyaandika kwa usahihi kama ulivyofanya wewe Mkulu!-Hongera tena.

Nafananisha uchambuzi huu na wa bwana mmoja kwenye RFA anayealikwa kwenye kipindi cha -ENZI HIZO-Kinachorushwa kila alhamisi kuanzia saa4.00usiku, huyu bwana akiitwa Zomboko!

NILIPOSOMA HII KITU, NIMEKUMBUKA kote nilikochemsha kimaisha, huenda hata hv sasa nisingalikuwa hapa...Acha tu mambo haya bana!...Ama kweli ujana haurudi na siku hazigandi!
 
Mechi yangu ya kwanza wakuu ilikuwa ya ligi kuiona (984 kati ya majimaji na cda ya dodoma pale songea my bro alikuwa kamaliza frm 4 basi akanipeleka uwanjani, peter tino alikuwa anacheza namba tisa, mdogo wake anaitwa gebo pete alikuwa namba tisa ya cda basi majimaji walianza wao mpira, wakati peter tino amekanyaga mpira kir
 
enzi za mwalimu kulikuwa na wababe. kulikuwa kunajulikana kabsaa mtemi wa mtaa ni nani, ukienda shule utasikia flani anapiga darasa zima kuna wa pili hapo, watatu na kuendelea, haya kuna mbabe wa shule nzima, huyo mpaka walimu walikuwa wanamuogopa. mwingine utasikia anapiga mkoa mzima tehe kwenye madisco haguswi huyo. miaka ya mwisho ya themanini na mwanzo mwanzo wa miaka ya tisini kuna jamaa pale iringa alikuwa anaitwa cool nine ndo alikuwa anaaminika pale iringa town yote alikuwa mbabe
 
magazeti yalikuwepo ya uhuru mzalendo na sunday news nakumbuka matangazo ya ma disco venues wakati huo utakuta disco ymca, mbowe oceanic, motel agip, new africa hotel, kilimanjaro hotel pool side, ma dj akina chriss phaby, joe pantalakis, jerry koto, nigger j, majumba ya sinema kulikuwa na new chox sinema, avalon cinema, empress cinema, pale drive in cinema sasa hivi ubalozi wa marekani
 
dah miaka ya 80 soka wadau ilikuwa noma mnamkumbuku peter tino international alitupeleka lagos na bao lake kwenye african cup of nation? yanga enzi hizo akina isihaka hassan chuku, allan shomari, charles boniface mkwasa, juma mkambi, makumbi juma homa ya jiji, abedi mziba, ahmed amasha, aboubakar salum sure boy, lawrence mwalusako, athumani juma chama na wengineo simba akina lila shomari, zuberi magoha, zamoyoni mogela golden boy, idd pazi father. hawa jamaa walitisha sana. kuna majimaji fc walikwepo akina isihaka majaliwa, samli ayoub, sijaona tena mido yenye control km octavian mrope, hamis fande, mzee wa kiminyio madaraka suleiman, celestine sikinde mbunga,peter tino hawa walishakuwa mabingwa bara na muungano. nakumbuka timu zilizokuwa zikija na kushinda pale majimaji ni simba ya ramadhani leny, hussein amani masha na pamba ya kina joram mwakatika, mwakalebela na uzi wao mweupe kuanzia soksi bukta na jezi ya juu halafu kifuani zimeandikwa pamba kwa thiodane. nyota nyekundu akina john manyama, steven chibichi, aziz nyoni.
Mukulu, sasa hii ndio ilikuwa PAMBA YA MWANZA original ,nayo ilikuwa hivi.
Madatta Lubigisa/Juma mhina, Yusuf Ismail"Bana",Athman Juma "Chama",Khamis Magongo,Joram Mwakatika, James Ng'ong'a,Idd watchee, Antony Nyembo,Khalid Bitebo,Abuu Juma.
Hapo wanapambana na PAMBA ya Shinyanga golini yupo Khamis Maftaha, Khasim Nadhar, Hashim Liseki, Sululu mrisho, Bakar Kulewa, Abbas Magongo(hii mechi alionyeshwa red card kwa kugombana na kaka yake then akakimbilia Kenya-Gor Mahia),Anatoly Safari,Issa Mohamed na winga la kushoto alikuwepo Nasib Hussein.
Hapo ni KAMBARAGE stadium nimeruka ukuta nikiwa bado kinda, them days men.
 
heshima kwako mkuu Balantanda..duuuh umenikumbusha mbalii mie miaka hiyo nikiwa na bibi yenu
 
Mukulu, sasa hii ndio ilikuwa PAMBA YA MWANZA original ,nayo ilikuwa hivi.
Madatta Lubigisa/Juma mhina, Yusuf Ismail"Bana",Athman Juma "Chama",Khamis Magongo,Joram Mwakatika, James Ng'ong'a,Idd watchee, Antony Nyembo,Khalid Bitebo,Abuu Juma.
Hapo wanapambana na PAMBA ya Shinyanga golini yupo Khamis Maftaha, Khasim Nadhar, Hashim Liseki, Sululu mrisho, Bakar Kulewa, Abbas Magongo(hii mechi alionyeshwa red card kwa kugombana na kaka yake then akakimbilia Kenya-Gor Mahia),Anatoly Safari,Issa Mohamed na winga la kushoto alikuwepo Nasib Hussein.
Hapo ni KAMBARAGE stadium nimeruka ukuta nikiwa bado kinda, them days men.
Dah mauza uza umenikumbusha huyo jamaa anaitwa abass hamis magongo alipokuja na gor mahia dar kucheza na yanga hapa dah jamaa alituua vibaya mno, hivi zile timu zimeishia wapi gor mahia na afc leapard?
 
Daaaaaah huyu Abbas Magongo alikuwa mbaya sana kwa kucheka na nyavu alitokea Pamba ya Shinyanga kabla ya kwenda Gor Mahia na kuchukua kabisa uraia wa Kenya pamoja na Abdallah Shebe(wote hawa ni watanzania walong'ara na timu ya taifa ya Kenya-Harambee star).Kaka yake wa Pamba ya Mwanza alikuwa ni Ibrahim Magongo,jamaa wa Mwanza hawa ukoo mkubwa ndo unawaunganisha wote na akina Khalfan Ngassa na Juma Amir Maftah.
 
mi nakumbuka miaka ya mwisho mwisho ya 80 tulikkuwa tunasikiliza mpira kwenye radio kulikuwa na mtangazaji mmoja akiitwa Charles Hilary, yaani akitangaza mpira utadhani unaona live vile

pia michezo ya redio naimiss sana sana
 
miaka hiyo pia kulikuwa na kipindi cha mama na mwana, kulikuwa na hadithi ya ua jekundu nilikuwa naipenda sana ile hadithi, yaani mama na mwana ikianza tu au pwagu na pwaguzi tunazunguka redio ...watu kimyaa, hakuna hata kukohoa
 
Nikianza na Muziki,kwa kipindi cha nyuma muziki wa Dansi(ya ukweli) ulikuwa umeshamiri sana nchini kwetu kiasi kwamba enzi hizo redioni ilikuwa ni mwendo wa muziki wa Dansi tu.Kuna baadhi ya wanamuziki ambao kwangu mimi huwa ni vigumu sana kuwasahau kutokana na mchango wao katika kuufanya muziki wetu(enzi hizo) uwe maarufu.Binafsi siwazungumzii wanamuziki wa miaka ya 60 na 70 bali nawazungumzia wanamuziki wa miaka ya 80 mwanzoni mpaka miaka ya 90 ambao daima walinivutia na abado wananivutia kutokana na uzuri wa miziki yao,wanamuziki hawa kwa sasa ni marehemu,hivyo nimeona ni bora niitumie nafasi hii japo kwa uchache kuwashirikisha katika kuwakumbuka mashujaa wangu hawa wa muziki.Kila mtu anajua kwamba kuna wanamuziki ambao huwezi kuacha kuwataja mara tu uanzapo kuuzungumzia muziki wa Tanzania,wanamuziki hawa ni kama akina Salum Abdallah,Mbaraka Mwinyshehe Mwaruka,Marijani Rajabu n.k(Mungu awarehemu). Mimi leo nimeguswa kuwakumbuka wanamuziki hawa wafuatao:-

1.Hemed Maneti Ulaya:-Mzee mzima mwenyewe wa Vijana Jazz Air Pambamoto ,huyu
mkulu kwa kweli alikuwa ananikosha mnoo kwa utunzi na uimbaji wake kiasi kwamba
alipachikwa jina la Chiriku.Baadhi ya nyimbo(ninazozijua) ninazozipenda mpaka leo ni
kama Maria,Tambiko la Pambamoto,Bujumbura,Penzi haligawanyiki sehemu ya 1 na
ya 2 na nyingine nyingi tu.Huyu bwana alikuwa na kipaji kwa kweli.

2.Eddy Sheggy:- Huyu bwana naye alikuwa na kipaji,ukisikiliza nyimbo zake kama
Milima ya kwetu(akiwa na Super Rainbow),Penzi haligawanyiki,Ogopa Tapeli,Mwisho
wa mwezi nk(akiwa na Vijana Jazz),Nelson Mandela,Shakaza(akiwa na Washirika
Tanzania Stars,wimbo wa Shakaza aliurudia pia alipohamia Bima Lee Orchestra) au
Nyimbo za Baba Jenny na Gondoigwe(akiwa na Bantu Group) uatona ni jinsi gani naye
Alikuwa na kipaji cha kuimba.

3.Jerry Nashon Dudumizi:- Mtaalamu mwingine wa Vijana Jazz ambaye daima mimi
namkumbuka kwa nyimbo zake tamu alizotunga na kuimba akiwa na Vijana Jazz,
nyimbo kama VIP,Shoga,Theresa na nyingine nyingi tu…..

4.Suleiman Mbwembwe:- Huyu namkumbuka kwa nyimbo yake tamu ya Mama Chichi
(akiwa Vijana Jazz) na nyingine nyingi akiwa na Juwata/Ottu Jazz/Msondo Ngoma.

5.Francis(Nassir) Lubua,mtaalamu mwenyewe wa Nginde Ngoma ya Ukae

6.Tino Masinge "Arawa"….Sina la kusema hapa jamani…R.I.P

7.Ali Kishiwa Mhoja "TX Moshi William"…Aaargh,kifo jamani.Ukisikia mtu ana
kipaji TX alijaliwa hasa,sina haja ya kutaja kazi yake,inajulikana.

8.Athuman Momba:-Kifaa kingine hiki cha Vijana Jazz na Msondo Ngoma…R.I.P

9.Le supreme Fredy Ndala Kasheba:- Mzee wa ZAITA MUSICA wana ZUKE ZUKE
Muselebende,nani atavishau vibao vyake vitamu kama Marashi ya Pemba,Dezodezo
(Tshala Muana aliununua huu wimbo) ama ule wimbo mtamu wa Kesi ya Khanga
(mama nipe nauli nikamfuate Monica,amekimbilia Zambia na Treni ya mizigo,kisa cha
kukimbia madeni yamemzidi,Doti kumi za Khanga alizokopa hajalipa)….dah

10.Suleiman Mwanyiro "Computer": Mtaalamu huy wa gitaa zito(besi) wa Nginde

11.Kalala Mbwembwe:-Huyu bwana alikuwa Tancut Almas baadaye akaanzisha bendi
ya Ruaha International,namkumbuka kwa nyimbo zake kama Lutandila,Safari n.k

12.Kyanga Songa:-Huyu bwana alikuwa na pacha wake tangu Sambulumaa,Tancut na
baadae Ruaha International

Wakuu kwangu mimi hizi ni Hazina zilizotoweka ghafla tukiwa bado twazihitaji.Tuendelee kuwataja wengine ambao nimewasahau…Sasa hivi muziki wa Dansi Bongo ni kama umejifia tu,hakuna kitu,kila kitu vijana wanakopi muziki wa Kikongo tuuuuuuuuu…..Pa1

Mkuu heshima mbele...
Kweli umenikumbusha mbali saaana, lakini inawezekana vipi ukamzungumzia marehemu Momba kisha ukamsahau Hassan Rehani?
Au ukamzungumzia kalala mbwembwe ukawaacha watu kama dr remmy, bushoke, na Cosmas?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom