Tumeshindwa kuoana kwa tofauti ya dini, utatuzi ni nini hapa?

Oct 11, 2015
15
12
Wadau nawasalimu,

Nimekua na huyu msichana kwa miaka 5 sasa, na mimi ndie nilikua wa kwanza kwake, mazungumzo ya kuishi pamoja kama mke na mume tuliyaanza 2 yrs ago, kila tunapoweka mezani mjadala huo tunashindwa kufikia muafaka kwa kila mmoja kutaka mwingine ndie abadili dini ili ndoa ifungwe.

Baada ya 5 yrs ya uhusiano huu na mkwamo huu wa dini, niseme tu kwamba nimechoka na hali hii na nahitaji ku move on ili niendelee na mtu mwingine badala ya kupoteza muda, hivyo nikamuita mwenzangu na kumweleza msimamo huu wa kuachana, ambapo amegoma na kunibembeleza sana kwamba let's give it another chance another trial.

Kinachonishangaza ni kuwa kwa miaka hiyo 2 ya mazungumzo kila tunaposhindwana yeye hukimbilia kusema let's give it another chance another trial huenda one day tukafikia muafaka.

Jambo ambalo nimeona haliwezekaniki
Kwa uelewa wangu and according to tradition mwanamke ndie anaepaswa kubadili dini kumfuata mwanaume, lakini yeye anang'ang'ania mimi ndio nimfuate yeye kwamba wazazi wake hawatakubali, sasa huwa namuuliza kwa hiyo wazazi wangu ndio watakubali?

Na ndoa ya bomani wote hatuitaki maana kama mimi mfano ni muumini mzuri kwenye dini yangu na ninashiriki kila kitu sasa kwa nini nikafungie bomani? Pia yeye hataki bomani.

Sasa wadau hapo pana future kweli?

Si bora tufuate mapendekezo yangu ya kuachana tu? Au?
 
Sasa so utafute mkristo mwenzako, kwani mwanamke ndo huyo tu au ndo mahaba niue
 
hill and portion em njoo pande hizi my dear

Miaka miwili iliyopita mmeanza kuongelea ndoa but hampati muafaka kwa sababu ya dini. Na mtaendelea hivyo hivyo kutopata muafaka hadi miaka 10. Hakuna kitu cha kuwa nacho makini kama "common faith".

Mnapoanza mahusiano mnaona kama kitu cha kawaida but mbeleni wengi kinawaliza. Kama hakuna mmoja wenu atakayeitoa sadaka imani yake aifate ya mwingine, basi hamtofika kokote. And to be honest with you, hakuna kitu kigumu kama mtu kuikana imani yake totally, wengine wanabadilisha tu kisa ndoa, afu akifika kwenye ndoa anaendelea kuishi imani yake ya zamani. Kuna muda mtapishana kwa sababu huyu imani yake inamkataza kufanya hivi while mwingine inamruhusu. Na malezi ya watoto sijui inakuwaje, maana mama atawalea hivi, while baba atawalea vile, confusion tu kwa watoto. Kama madhehebu tu tofauti kuna Vitu tunapishana ( bora ubadilishe dhehebu na sio dini), itakuwaje kwa dini tofauti? Ifike muda uwe na msimamo na maamuzi yako, Kila la kheri
 
Last edited by a moderator:
kuwa na msimamo either you leave her or one of u abadili din thats all............. otherwise mtaendelea kuumizana
 
You've already decided, move on. Kwangu mimi ndoa ni a spiritual matter and you will find that to be true. Kama in spirit you find each other agreeable then dini hata zikiwa tofauti hakuna shida. Ndio maana utakuta watu dini tofauti but hawana kikwazo kati yao lakini kuna watu dini moja lakini wana vikwazo. Spirituality na dini vina utafauti, dini ni njia ya kufikia your spirituality, pray for a partiner ambaye ataku elevate toward that regardless of religion
 
You've already decided, move on. Kwangu mimi ndoa ni a spiritual matter and you will find that to be true. Kama in spirit you find each other agreeable then dini hata zikiwa tofauti hakuna shida. Ndio maana utakuta watu dini tofauti but hawana kikwazo kati yao lakini kuna watu dini moja lakini wana vikwazo. Spirituality na dini vina utafauti, dini ni njia ya kufikia your spirituality, pray for a partiner ambaye ataku elevate toward that regardless of religion

Mkuu haya umeyatoa kwenye maandiko gani ili nami nipate faida!!
 
Hahahahaaa.

Unauuuliza swali zuri sana, je wazazi wako ndio watakubali?

Siku akikujibu hilo swali nadhani mtafikia muafaka wa kuoana.

Oaneni,kisha baada ya ndoa unarudia dini yako ya zamani.
 
Kama kwa miaka miwili hamjafikia mwafaka nahisi kuna bomu la lawama unamwandalia mwenzio hasa wanaume wa kumwoa watakapoisha..... Dini ni ngumu sana kuongelewa vijiweni kwa sababu ndio utashi wa mtu.... Ila kwa tamaduni zetu wanasema mwanamke ana kabila tu lakini siyo dini..... Ila kama mwanamke ni Msabato na mwanamme ni Muislam hapo hata mjaribu mara elfu mia saba sabini hamtopata mwafaka hivyo niwashauri mtafute miunganiko pengine.
 
Yaani hawa wanasema ni waumini wazuri wa dini zao!!
kufanya uasherati wanaona siyo shida, wanafanya hivyo kwa miaka mitano sasa.

Jamani rejeeni kwenye mafundisho ya dini zenu.
 
hill and portion em njoo pande hizi my dear

Miaka miwili iliyopita mmeanza kuongelea ndoa but hampati muafaka kwa sababu ya dini. Na mtaendelea hivyo hivyo kutopata muafaka hadi miaka 10. Hakuna kitu cha kuwa nacho makini kama "common faith".

Mnapoanza mahusiano mnaona kama kitu cha kawaida but mbeleni wengi kinawaliza. Kama hakuna mmoja wenu atakayeitoa sadaka imani yake aifate ya mwingine, basi hamtofika kokote. And to be honest with you, hakuna kitu kigumu kama mtu kuikana imani yake totally, wengine wanabadilisha tu kisa ndoa, afu akifika kwenye ndoa anaendelea kuishi imani yake ya zamani. Kuna muda mtapishana kwa sababu huyu imani yake inamkataza kufanya hivi while mwingine inamruhusu. Na malezi ya watoto sijui inakuwaje, maana mama atawalea hivi, while baba atawalea vile, confusion tu kwa watoto. Kama madhehebu tu tofauti kuna Vitu tunapishana ( bora ubadilishe dhehebu na sio dini), itakuwaje kwa dini tofauti? Ifike muda uwe na msimamo
 
Last edited by a moderator:
Yaani hawa wanasema ni waumini wazuri wa dini zao!!
kufanya uasherati wanaona siyo shida, wanafanya hivyo kwa miaka mitano sasa.

Jamani rejeeni kwenye mafundisho ya dini zenu.

Well said mkuu bagain
 
Last edited by a moderator:
Hawa ni wazinifu kama walivyo wazinifu wengine... dogo mnaendelea kumkasirisha muumba... kuona lazima mkubali kuwa dini moja hayo ya let us try hayafai... na wala msidanganyike eti muoane kila mtu na dini yake hiyo ndo balaa na mess nyingine itaazia kwenu na kwa wanenu na jamii yote ... na wala usidanganyike eti mwanamke hana dini nani kakudanganya dini wanazo sana .... Bi khadija ni mtu wa kwanza kuukubali uislam na mtu wa kwanza kupoteza maisha kwa ajili ya kumkubali Mungu mmoja ni mwanamke....
 
Fungeni NDOA ya kiserikali au ya kimila dini zaliletwa na wazungu acheni ulimbukeni siyo lazma NDOA ifungwe makanisani
 
Mme invest mda mwingi kwenye uhusiano wenu huku mkijua mnatofauti moja kubwa sana ambayo uleta matatizo kwenye mapenzi.

Miaka mitano mingi sana mmepoteza kujenga penzi lenu bila kutatua hili swala la dini. Mlitakiwa kujua msimamo wenu huko wapi mwanzoni kabisa hata kama hamkua na nia ya kuona.

Kama wewe ni muhumini sana na ulijua/unajua kwamba hutaki kuoa msichana wa dini nyingine basi usingejengA uhusiano na msichana huyu. Ni vizuri ungetafuta msichana wa dini yako; hivyo hivyo kwa huyo msichana, kama alijua msimamo wake ni kutobadilisha dini hasingejenga uhusiano na mtu wa dini tofauti.

Ushauri wangu kama mnapendana kweli, dini ni imani, wewe unaweza kukaa na imani yako na yeye akaendelea na imani yake huku mapenzi yenu yanaendelea. Watoto wakizaliwa m-wafundishe dini zote mbili huko baadae wakiwa wakubwa watachagua dini gani waendelee nayo.

Kama haiwezekani na mnahisi kwamba mapenzi yenu hayana nguvu na ni bora mtupilie mbali miaka yenu mitano kisa imani zenu zitabadirika kama mkiendelea, basi kila mtu akatafute wa dini yake muanze upya.

Wakuu wengine kama mnaona dini ni kikwazo kikubwa ni vizuri kujenga uhusiano na mtu wa dini yako hili msipotezeane mda. Wako wengi tu wa dini tofauti wanaishi mke na mme na wanafuraha ndani ya ndoa.
 
Back
Top Bottom