Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Tanzania tangu mwanzo imekuwa ikifuata tahadhari za kujikinga na corona huku yenyewe ikiziangalia tahadhari hizo kwa umakini sana.
Kwa kiasi kikubwa Tanzania imeibuka shujaa katika vita hivi hata kama bado hakujatolewa tangazo rasmi ya kwisha kwa janga hili.
Hata Trump wa Marekani na mganga wake mkuu wa maradhi ya maambukizi Dkt Fauci jana walitoa tamko la kukoma kuwafungia watu ndani tena kama kinga ya corona.
Kwa msimamo huu Tanzania haiko peke yake japokuwa imekuwa mbele kueleza msimamo wake.La kushangaza ni kuwa kila siku ukifuatilia vyombo vya habari vya nje utakuta hawachoki kutilia shaka maelezo ya Tanzania na kama kwamba wanahamu kusikia watanzania wengi wanakufa kwa corona.
Sisi mitaani na mahospitalini kwetu hatujaiona korona na tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutukinga na janga hili,kwanini mabeberu wanashangilia majanga ya wenzao.